Arusi ya Kana
From Wikipedia, the free encyclopedia
Arusi ya Kana iliyo maarufu ni ile ambayo waliihuduria Bikira Maria na Yesu Kristo pamoja na wanafunzi wake [1] kama inavyosimuliwa na Injili ya Yohane (2:1-11) [2].
Maelezo zaidi Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu, Mazingira ya Yesu ...
Funga
Divai ilipokwisha, Bikira Maria alimhimiza mwanae ajihusishe, ikawa hivyo kwamba Yesu alifanya muujiza wake wa kwanza [3] kwa kugeuza mapipa ya maji kuwa divai bora akidhihirisha utukufu wake hata wanafunzi wake wakamuamini [4][5].
Umuhimu wa tukio hilo ni hasa kwamba ni ishara ya Yesu kuwa bwanaarusi anayemleta Roho Mtakatifu kwa wingi kuwe na furaha katika utimilifu wa Agano Jipya (divai) badala ya hatua ya maandalizi ya Agano la Kale (maji).