Mitazamo ya Agano Jipya juu ya Yesu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Mitazamo ya Agano Jipya juu ya Yesu

Mitazamo ya Agano Jipya juu ya Yesu inatofautiana kadiri ya waandishi, lakini bila kuvunja umoja wa imani yuu yake kama Kristo na Mwana wa Mungu.

Mchoro wa Lodovico Carracci (1594) unaoonyesha kugeuka sura kwa Yesu mbele ya mitume wake Petro, Yakobo Mkubwa na Yohane.

Mitazamo muhimu zaidi ni ile ya Mtume Paulo na Mtume Yohane, ambao ndio wanateolojia hasa, lakini ipo mingine kama ile ya Injili ya Marko, Injili ya Mathayo, Mwinjili Luka, Waraka kwa Waebrania n.k.

Pengine mwandishi yuleyule anatushirikisha mitazamo tofautitofauti katika vitabu vyake, kwa mfano kutokana na maendeleo ya uelewa wake. Hivyo jinsi Yesu Kristo anavyoonekana katika Waraka kwa Waefeso imeendelea kuliko ilivyo katika Waraka wa kwanza kwa Wathesalonike ulioandikwa na Paulo yuleyule zaidi ya miaka 10 kabla yake.

Kristolojia inakusanya mitazamo hiyo yote na kujitahidi kuelewa zaidi tena fumbo la Kristo.

Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mitazamo ya Agano Jipya juu ya Yesu kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.