Utukufu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Utukufu (kwa Kiebrania הוד, hod, na כבד, kabod, "uzito"; kwa Kigiriki δόξα, doxa, "tathmini"; kwa Kiingereza glory kutoka Kilatini gloria, "umaarufu") ni hasa sifa ya Mungu anapojitokeza kwa viumbe.
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/c/c1/Saint_Catherine%27s_Transfiguration.jpg/320px-Saint_Catherine%27s_Transfiguration.jpg)
Katika Biblia na Ukristo utukufu ni muhimu sana, kwa sababu unatazamwa kuwa ndio lengo la uumbaji[1] ili kwa njia hiyo watu waokoke.[2]
Katika Kut 33:20, Musa aliambiwa mtu yeyote hawezi kuona utukufu huo na kuendelea kuishi.
Yesu aliwafundisha wafuasi wake kutenda mema, ili watu wakiona wamtukuze Baba wa mbinguni (Math 5:16).
Kadiri ya Injili Ndugu, Yesu alionekana na wanafunzi watatu akiwa katika utukufu pamoja na Musa na Elia (Lk 9:29-32).
Utukufu utashirikishwa kwa binadamu waadilifu watakapofufuliwa siku ya mwisho
Kinyume cha kulenga utukufu huo kutoka kwa Mungu, mara nyingi watu wanajitafutia sifa kutoka kwa wenzao (Yoh 12:43). Ndiyo dhambi ya majivuno inayozuia imani.[3]