![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/3/39/Unknown_French_Master_-_Allegory_of_the_Vanity_of_Earthly_Things_-_2.jpg/640px-Unknown_French_Master_-_Allegory_of_the_Vanity_of_Earthly_Things_-_2.jpg&w=640&q=50)
Majivuno
From Wikipedia, the free encyclopedia
Majivuno ni tabia ya mtu kujipongeza mno kutokana na sifa alizonazo[1][2][3].
![](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/3/39/Unknown_French_Master_-_Allegory_of_the_Vanity_of_Earthly_Things_-_2.jpg/640px-Unknown_French_Master_-_Allegory_of_the_Vanity_of_Earthly_Things_-_2.jpg)
Maelezo zaidi Vilema vikuu ...
Funga
Yanatokana na kiburi na kufikia hatua ya majigambo ya uongo ambayo ni chukizo kwa wengine.
Katika dini mbalimbali yanatazamwa kama aina ya kujiabudu badala ya Mungu.
Katika maadili ya Ukristo (Lk 14:11; 1Pet 5:5), majivuno ni mmojawapo kati ya mizizi ya dhambi (au vilema vikuu au vichwa vya dhambi) inayozaa dhambi nyingine nyingi (1Kor 5:6-7).
Jina la Kilatini (vanitas au vanagloria, kwa Kiingereza: vanity[4] au vainglory[5]) linahusisha tabia hiyo na ubatili.