Wayahudi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Wayahudi (kwa Kiebrania יְהוּדִים, Yehudim) ni kundi la kikabila na la kidini lenye asili yake katika eneo la Israeli ya Kale (Mashariki ya Karibu). Kabila la Kiyahudi, taifa la Kiyahudi na dini ya Kiyahudi, yote yana uhusiano wa karibu sana, kwa sababu Uyahudi ndio dini ya jadi ya watu wa taifa la Kiyahudi
Ukweli wa haraka Native label, Lugha zinazozungumzwa, zilizoandikwa au zilizotiwa sahihi ...
Funga
Katika utamaduni wa Kiyahudi, ukoo unarudi nyuma hadi kwa mababu wa Biblia kama vile Abrahamu, Isaka, Yakobo na wanae 12 katika milenia ya 2 KK. Lakini tangu kale wanaogeuka kuwa Wayahudi na kuingizwa ndani ya kundi lao, hadhi yao ni sawa na wale ambao wamezaliwa ndani ya kabila hilo.