From Wikipedia, the free encyclopedia
Mfumo wa Misimbo ya Posta ya Tanzania (postikodi Tanzania) umeanzishwa tangu mwaka 2012. Msimbo wa posta ni namba iliyochaguliwa kwa kila kata nchini. Kila kata ina msimbo wa tarakimu tano.
Nia ni kuwa kila barua inayotumwa nchini Tanzania ionyeshe namba hiyo juu ya bahasha yake kama sehemu ya anwani ya barua au kifurushi ili kurahisisha na kuharakisha usafirishaji.
Namba ya msimbo wa posta ni tofauti na namba ya sanduku la posta; msimbo wa posta unahusu mahali au eneo, ilhali sanduku la posta linamhusu mpokeaji wa barua.
Msimbo wa posta nchini Tanzania huwa na tarakimu tano zilizopangwa kufuatana na ngazi za utawala wa nchi:
Mfano:
6 5 4 0 1 ni msimbo wa posta kwa Kilwa Masoko.
• 6 ni tarakimu kwa Kanda ya Pwani
• 6 5 inaonyesha Mkoa wa Lindi
• 6 5 4 inataja Wilaya ya Kilwa (651 ni Lindi mjini, 563 Nachingwea, 655 Liwale, na kadhalika)
• Tarakimu za mwisho 0 1 ni za kata ya Kilwa Masoko.
Ilhali wilaya ya Kilwa huwa na kata 21, misimbo ya kata za Kilwa inaendelea kuanzia 6 5 4 0 1 (Kilwa Masoko) hadi 6 5 4 2 1 (Kibata).
Maana yake kama barua inaonyesha anwani ya „65421 Kibata“ inaweza kusafirishwa, si lazima mfanyakazi aulize Kibata iko wapi? Inatosha akijua ni barua kwenda pwani („6“) na Mkoa wa Lindi („65“). Pale Lindi wanajua wilaya zao na 654 ni Kilwa, vivyo hivyo hao wanajua kata katika eneo lao.
Utaratibu huo unatunza nafasi kwa kuanzishwa kwa vitengo vipya; kanda linaweza kuongezwa mikoa hadi 10, kila mkoa wilaya hadi 10, na kata hadi 100 kila wilaya. Kuna pia nafasi kwa kanda mpya 2.
Kanda ni hizi zifuatazo, na kila mkoa wa Tanzania ni sehemu ya kanda fulani:
Eneo | Tarakimu | Mfano wa msimbo wa kata |
---|---|---|
Mkoa wa Dar es Salaam | 11 | |
Manisipaa ya Ilala | 11, 12 | Kivukoni 11101 |
Manisipaa ya Kinondoni | 14 | Magomeni 14101 |
Manisipaa ya Temeke | 15 | Temeke 15101 |
Manisipaa ya Ubungo | 16 | Mburahati 16101 |
Manisipaa ya Kigamboni | 17 | Kimbiji 17101 |
Eneo | Tarakimu | Mfano wa msimbo wa kata |
---|---|---|
Mkoa wa Pwani | 61 | |
Mji wa Kibaha | 611 | Mailimoja 61102 |
Wilaya ya Kibaha | 612 | Mlandizi 61201 |
Wilaya ya Bagamoyo | 613 | Yombo 61306 |
Wilaya ya Kisarawe | 614 | |
Wilaya ya Mkuranga | 615 | Kiparang'anda 61502 |
Wilaya ya Rufiji Wilaya ya Kibiti | 616 | Utete 61601 Kibiti 61610 |
Wilaya ya Mafia | 617 | |
Mkoa wa Mtwara | 63 | |
Manisipaa ya Mtwara | 631 | |
Wilaya ya Mtwara | 632 | |
Wilaya ya Tandahimba | 633 | |
Wilaya ya Newala | 634 | |
Wilaya ya Masasi | 635 | Mwenge Mtapika 63529 |
Wilaya ya Nanyumbu | 636 | Nangomba 63601 |
Mkoa wa Lindi | 65 | |
Manisipaa ya Lindi | 651 | Makonde 65101 |
Wilaya ya Lindi | 652 | Nachunyu 65201 |
Wilaya ya Nachingwea | 653 | |
Wilaya ya Kilwa | 654 | Kilwa Masoko 65401 |
Wilaya ya Liwale | 655 | Liwale Mjini 65501 |
Wilaya ya Ruangwa | 656 | Ruangwa 65601 |
Mkoa wa Morogoro | 67 | |
Manisipaa ya Morogoro | 671 | |
Wilaya ya Morogoro | 672 | |
Wilaya ya Mvomero | 673 | |
Wilaya ya Kilosa | 674 | |
Wilaya ya Kilombero | 675 | |
Wilaya ya Ulanga | 676 | Mahenge 67601 |
Wilaya ya Gairo | 677 | Gairo 67701 |
Eneo | Tarakimu | Mfano wa msimbo wa kata |
---|---|---|
Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja | 71 | |
Wilaya ya Mjini | 711 | |
Wilaya ya Magharibi Unguja | 712 | Mwanakwerekwe 71201 |
Mkoa wa Kusini Unguja | 72 | |
Wilaya ya Kusini | 721 | |
Wilaya ya Kati | 722 | Dunga 72201 |
Mkoa wa Kaskazini Unguja | 73 | |
Wilaya ya Kaskazini A | 731 | |
Wilaya ya Kaskazini B | 732 | Mahonda 73201 |
Mkoa wa Kusini Pemba | 74 | |
Wilaya ya Mkoani | 741 | |
Wilaya ya Chake Chake | 742 | Chanjaani 74201 |
Mkoa wa Kaskazini Pemba | 75 | |
Wilaya ya Wete | 751 | |
Wilaya ya Micheweni | 752 | Micheweni 75201 |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.