From Wikipedia, the free encyclopedia
Wilaya ya Newala ni moja ya wilaya za Mkoa wa Mtwara. Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 205,492.
Wilaya hii imepakana na Wilaya ya Masasi upande wa magharibi na kaskazini, wilaya ya Tandahimba upande wa mashariki na kaskazini, mto Ruvuma na Msumbiji kwa kusini. Newala imepakana kwa karibu kabisa na nchi ya Msumbiji ambapo mto Ruvuma ndio unaotenganisha wilaya ya Newala na nchi ya Msumbiji.
Wakazi walio wengi ni Wamakonde, pamoja na Wayao.
Idadi kubwa ya wakazi wa wilaya ya Newala ni wakulima na zao kuu la biashara ni korosho.
Mnamo mwaka 2015 maeneo ya Newala mjini yalipewa halmashauri ya pekee na hivyo kutengwa na Wilaya ya awali[1].
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.