Remove ads
asasi au shirika linalotambuliwa kisheria ambalo limeundwa kwa ajili ya kuunda au kuuza bidhaa na / au huduma kwa wateja na linashughulika na aina yoyote ya biashara From Wikipedia, the free encyclopedia
Kampuni (kutoka Kiingereza "company") ni asasi au shirika linalotambuliwa kisheria ambalo limeundwa kwa ajili ya kuunda au kuuza bidhaa na / au huduma kwa wateja[1] na linashughulika na aina yoyote ya biashara.
Ufafanuzi wa neno na taratibu za sheria hutofautiana nchi kwa nchi. Kwa ujumla, kampuni shirika la biashara linalotengeneza bidhaa kwa namna iliyopangwa na kuziuza kwa umma ili kupata faida.
Kampuni inaweza kuajiri watu kuwa wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Kampuni zinapatikana sana katika uchumi wa kibepari, nyingi zikiwa zinamilikiwa na watu binafsi kwa ajili ya kupata faida ambayo itaongeza mali ya wamiliki wake na kuikuza biashara yenyewe. Wamiliki na wahudumu wa biashara huwa na lengo mojawapo kuu kama kupata mapato ya kifedha kutokana na kazi wanayoifanya napia kwa sababu ya kukubali kujiingiza kwenye hatari ya kufanya biashara. Baadhi ya kampuni ambazo malengo yake siyo kama yale yaliyosemwa hapo juu ni kama vyama vya ushirika na kampuni zinazomilikiwa na serikali.
Biashara pia inaweza kuanzishwa bila kusudi la kupata faida au biashara inayomilikiwa na serikali.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.