1 Pamoja na Kimandarini kile cha Kikantoni ni lugha rasmi katika Hong Kong na Macau. Kiingereza ni pia lugha rasmi katika Hong Kong na Kireno huko Macau. Vilevile kuna lugha za kieneo yanayotumiwa rasmi kama vile Kiuyghur huko Xinjiang, Kimongolia katika jimbo la Mongolia ya Ndani, Kitibet huko Tibet na Kikorea katika mkoa wa Yanbian.
Kuna mito mikubwa; mrefu zaidi ni Yangtse (km 6,300), Hwangho au Mto Njano, Xi Jiang au mto wa Magharibi, Mekong, Mto wa Lulu, Brahmaputra na Amur. Mito hiyo yote ina vyanzo vyake katika milima mikubwa yenye usimbishaji mwingi, ikibeba maji kwenda tambarare pasipo mvua nyingi.
Kutokana na madawa ya kilimo na maji machafu ya viwanda, mito na maziwa ya China hupambana na machafuko makali; mwaka 2007ziwa Tai lilisafishwa kwa gharama kubwa mno kwa sababu maji hayakufaa tena kwa mahitaji ya binadamu (maji ya bomba).
Hali ya hewa
Kuna kanda 18 za hali ya hewa zinazoonyesha tofauti kubwa kati yake. Upande wa magharibi, kaskazini na kaskazini-mashariki huwa na majira yenye joto kali na baridi kali. Upande wa kusini ina tabia ya tropiki au nusutropiki. Tibet huwa na hali ya hewa kulingana na kimo chake juu ya mita 4,000.
Ramani ya usimbishaji inaonyesha ya kwamba kilimo kinawezekana katika nusu ya kusini na kusini-mashariki ya nchi tu. Upande wa kaskazini na magharibi mvua ni chache mno. Mstari mwekundu unaonyesha mpaka na juu yake usimbishaji ni chini ya milimita 390 kwa mwaka.
Wakati wa vita kuu ya pili ya dunia sehemu kubwa ilitwaliwa na Japani. Wakati huo Chama cha Kikomunisti cha China kiliandaa jeshi kikapambana na serikali ya Kuomintang na Japani pia.
Baada ya mwisho wa vita kuu Wakomunisti waliendelea kupingana na serikali na mwaka 1949 Kuomintang ilishindwa. Wakomunisti chini ya Mao Zedong walianza kutawala China Bara kama Jamhuri ya Watu wa China na Kuomintang walikimbilia kisiwa cha Taiwan walipoendelea kutawala kama "Jamhuri ya China".
Siasa
Serikali ya China inatawala kwa mfumo wa udikteta chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti ya China. Kuna vyama vidogo pia, lakini hivi havina umuhimu wowoteː vinasimamiwa na Wakomunisti, hivyo hali halisi ni mfumo wa chama kimoja.
Kikatiba chombo kikuu ni Bunge la umma la China linalomchagua rais, serikali, mahakama kuu, kamati kuu ya kijeshi na mwanasheria mkuu. Lakini hali halisi maazimio yote ya bunge ni utekelezaji tu wa maazimio ya uongozi wa chama cha Kikomunisti.
Uongozi huo ni kundi dogo la wakubwa wa chama na jeshi. Mwanasiasa muhimu ni Xi Jinping. Kwa sasa yeye anaunganisha vyeo vya Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti, Rais wa Jamhuri ya Watu wa China na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi. Kwa jumla katika mapokeo ya Kikomunisti vyeo vya chama ni muhimu kuliko vyeo vya serikali ingawa katiba na sheria inasema tofauti.
Kuna pia "maeneo yenye utawala wa pekee" ambayo ni Hongkong na Macau. Katika miji hiyo miwili, iliyokuwa makoloni ya Uingereza na Ureno, kuna uhuru wa kisiasa na wa uandishi, uchaguzi huru na upinzani kwa kiasi fulani, lakini maeneo yana tu madaraka kadhaa ya kujitawala kwa mambo ya ndani.
Watu
China ikiwa na wakazi milioni 1,400 (Januari 2020) ni nchi yenye watu wengi zaidi duniani. Historia yake yote iliona tena na tena vipindi vya njaa kutokana na idadi kubwa ya watu wake. Msongamano wa watu kwa wastani ni wakazi 145 kwa kilomita ya mraba. Lakini tofauti ziko kubwa kati ya miji mikubwa ambako milioni 115 wanakaa kwenye eneo la km² 50,000 na Tibet yenye watu 2 tu kwa kilomita ya mraba.
Zaidi ya asilimia 90 za wakazi wote wanakaa katika theluthi ya kusini-mashariki ya nchi yenye mvua ya kutosha. Ndani ya theluthi hiyo ni nusu ya Wachina wote wanaosongamana kwenye asilimia 10 za China yote, maana yake katika 10% hizi kuna msongamano wa watu 740 kwa km².
Baada ya Urusi na Kanada ambazo ni nchi mbili kubwa zaidi, China na Marekani ni karibu sawa; kama maeneo yanayodaiwa na China bila kukubaliwa na majirani yanahesabiwa upande wake basi China ni kubwa kidogo kuliko Marekani
Marejeo
Meng, Fanhua (2011). Phenomenon of Chinese Culture at the Turn of the 21st century. Singapore: Silkroad Press. ISBN978-981-4332-35-4.
Farah, Paolo (2006). "Five Years of China's WTO Membership: EU and US Perspectives on China's Compliance with Transparency Commitments and the Transitional Review Mechanism". Legal Issues of Economic Integration. Kluwer Law International. Volume 33, Number 3. pp.263–304. Abstract.
Jacques, Martin (2009).When China Rules the World: The End of the Western World and the Birth of a New Global Order. Penguin Books. Revised edition (28 August 2012). ISBN 978-1-59420-185-1.
Craig, Edward (1998), Routledge Encyclopedia of Philosophy, Volume 7, Taylor & Francis, ISBN9780415073103
Fan Lizhu, Chen Na. Revival of Confucianism and Reconstruction of Chinese Identity. Paper presented at: The Presence and Future of Humanity in the Cosmos, ICU, Tokyo, 18–23 March 2015. (a)
Fan Lizhu, Chen Na. The Religiousness of "Confucianism" and the Revival of Confucian Religion in China Today. On: Cultural Diversity in China 1: 27-43. De Gruyter Open, 2015. ISSN 2353-7795, DOI: 10.1515/cdc-2015-0005
Pas, Julian F. Historical Dictionary of Taoism. Part of: Historical Dictionaries of Religions, Philosophies, and Movements Series. Scarecrow Press, 2014. ASIN: B00IZ9E7EI
Ruokanen, Miikka, Paulos Zhanzhu Huang. Christianity and Chinese Culture. William B. Eerdmans Publishing, 2011. ISBN 0802865569
Sautman, Barry. Myths of Descent, Racial Nationalism and Ethnic Minorities in the People's Republic of China. In: Frank Dikötter. The Construction of Racial Identities in China and Japan: Historical and Contemporary Perspectives. Honolulu, University of Hawai'i Press, 1997, pp.75–95. ISBN 9622094430
Shahar, Meir, Robert Paul Weller. Unruly Gods: Divinity and Society in China. University of Hawaii Press, 1996. ISBN 0824817249
Shen, Qingsong, Kwong-loi Shun. Confucian Ethics in Retrospect and Prospect. Council for Research in Values & Philosophy, 2007. ISBN 1565182456
Shi, Yilong. The Spontaneous Religious Practices of Han Chinese Peoples — Shenxianism (中国汉人自发的宗教实践 — 神仙教). On: Journal of South-Central University for Nationalities (Humanities and Social Sciences) (中南民族大学学报 — 人文社会科学版), Vol. 28, No. 3, 2008.
Teiser, Stephen F.The Chinese Cosmos: Basic Concepts, extracts from: Stephen F. Teiser. The Spirits of Chinese Religion. In: Religions of China in Practice. Princeton University Press, 1996.
Thien Do. Vietnamese Supernaturalism: Views from the Southern Region. Series: Anthropology of Asia. Routledge, 2003. ISBN 0415307996
Wang, Robin R. Chinese Philosophy in an Era of Globalization. State University of New York Press, 2004. ISBN 0791460061
Yang, Fenggang, Graeme Lang. Social Scientific Studies of Religion in China. Brill, 2012. ISBN 9004182462
Yang, Mayfair Mei-hui (2007). Ritual Economy and Rural Capitalism with Chinese Characteristics(PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo(PDF) mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2015-10-16.{{cite book}}: Invalid |ref=harv (help) Chapter of: David Held, Henrietta Moore. Cultural Politics in a Global Age: Uncertainty, Solidarity and Innovation, Oxford: Oneworld Publications. ISBN 1851685502
Bays, Daniel H. Christianity in China from the Eighteenth Century to the Present. (Stanford, CA: Stanford University Press, 1996). ISBN 0804726094.
Ch'en, Kenneth K. S. Buddhism in China, a Historical Survey. (Princeton, N.J.,: Princeton University Press, The Virginia and Richard Stewart Memorial Lectures, 1961, 1964).
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.
Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Jamhuri ya Watu wa China kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Wikiwand in your browser!
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.