Remove ads
From Wikipedia, the free encyclopedia
Bhutan ni nchi ndogo ya Bara Hindi katika milima ya Himalaya.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: "Nchi moja, taifa moja" | |||||
Wimbo wa taifa: Druk tsendhen | |||||
Mji mkuu | Thimphu | ||||
Mji mkubwa nchini | Thimphu | ||||
Lugha rasmi | Kidzongkha | ||||
Serikali | Ufalme Jigme Khesar Namgyal Wangchuck (འཇིགས་མེད་གེ་སར་རྣམ་རྒྱལ་དབང་ཕྱུག) Tshering Tobgay (ཚེ་རིང་སྟོབས་རྒྱས) | ||||
Ufalme wa kikatiba Wangchuk Dynasty |
17 Desemba 1907 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
38,394 km² (ya 133) 1.1 | ||||
Idadi ya watu - 2021 kadirio - 2022 sensa - Msongamano wa watu |
777,486 (ya 159) 727,145 20.3/km² (ya 210) | ||||
Fedha | Ngultrum (BTN ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
BTT (UTC+6:00) (haitumiki) (UTC+6:00) | ||||
Intaneti TLD | .bt | ||||
Kodi ya simu | +975
- |
Nchi imepakana na Uhindi na jimbo la Tibet la China.
Imetawaliwa na mfalme Jigme Khesar Namgyel Wangchuck tangu 2006.
Kuna wakazi takriban lakhi saba unusu.
Mji mkuu unaitwa Thimphu.
Bhutan ni nchi ya milima, na zaidi ya 80% za eneo la Bhutan ziko juu ya kimo cha mita 2,000. Mpakani kwa China kuna milima ya juu ya Lunana. Kula Kangri ni mlima mkubwa wenye kimo cha mita 7,553. Kusini tu kuna kanda nyembamba ya tambarare ya Duar.
Watu walio wengi hukalia eneo la milimani kati ya mita 2,000 hadi 3,000 juu ya UB.
Bhutan ilianzishwa mwaka 1644 na mmonaki Mbuddha Shabdrung Ngawang Namgyel.
Nchi iliweza kutunza uhuru wake hadi leo, lakini ililazimishwa kukubali maeneo ya kusini yatwaliwe na Waingereza na kuunganishwa na Uhindi wa Kiingereza. Uingereza ilishughulikia pia mahusiano ya nje ya Bhutan.
Uhusiano huu umeendelea na India kulingana na mkataba wa urafiki wa tarehe 8 Agosti 1949.
Tarehe 12 Februari 1971 Bhutan ikapokewa kama nchi mwanachama wa UM.
Wabhutan walio wengi huishio mlimani wako karibu kiutamaduni na kilugha na watu wa Tibet na Burma. Hao hufuata dini ya Ubuddha (74.7%) ambayo ndiyo dini rasmi. Lugha za jamii hiyo zinazotumika nchini humo ni 23. Mojawapo, Kidzongkha, ndiyo lugha rasmi.
Watu wa kusini wanafanana zaidi na watu wa Nepal na hutumia Kinepali, mojawapo ya lugha za Kihindi-Kiulaya. Wanafuata dini ya Uhindu (22.6%).
Bhutan inajitahidi kutunza utamaduni wake. Hadi mwaka 1974 watalii hawakuruhusiwa kutembelea nchi. Baadaye imewezekana lakini si rahisi kupata kibali.
{{cite web}}
: Unknown parameter |deadurl=
ignored (|url-status=
suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link){{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link){{cite book}}
: External link in |title=
(help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China. |
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Bhutan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.