From Wikipedia, the free encyclopedia
Ukomunisti ni njia ya kisiasa ya kufikiri na dhana ya jinsi gani jamii inapaswa kufanya kazi na kupanga mambo yake.
Ukomunisti ni aina ya ushoshalisti ambao unasema haipaswi kuwa na tofauti za matabaka katika jamii.
Ukomunisti unasema watu wa kila sehemu ya dunia wanapaswa kumiliki zana, viwanda, na mashamba ambayo yanatumiwa kuzalishia bidhaa na vyakula. Mchakato huu wa kijamii hujulikana kama umiliki wa kawaida. Katika jumuia ya wakomunisti, hakuna mali binafsi.
Mwanzo wa mafundisho haya uko kwenye maandiko ya Karl Marx na Friedrich Engels tangu kutolewa kwa "Ilani ya Kikomunisti" mwaka 1847[1].
Kwa mujibu wa waandishi na wafikiri wa Ukomunisti, lengo la Ukomunisti ni wafanyakazi kuchukua udhibiti wa viwanda na biashara na kusimamia uchumi kidemokrasia.
Baada ya wafanyakazi wa serikali kuimarisha maslahi yao wangeweza polepole kuleta zana zote za uzalishaji chini ya udhibiti wao, mpaka hapo mfumo wa bila matabaka na hali ya kutokuwa na serikali katika jamii imeumbwa.
Hili ni wazo la kizamani, lakini limeanza kuwa maarufu baada ya Mapinduzi ya Ufaransa na harakati nyingine maarufu za huko Ulaya mwanzoni mwa miaka ya 1800.
Pamoja na hoja ya kufikia hali ya usawa bila utawala kati ya wanadamu wanaitikadi wa ukomunsti waliona ni lazima kuwa na kipindi cha udikteta ambako wakomunisti wanashika utawala na kukandamiza upinzani dhidi ya mabadiliko waliyoona ya lazima kufikia shabaha yao.
Vladimir Lenin alipanua nadharia ya ukomunisti akidai lazima kuwa na chama cha kikomunisti kinachopanga mapinduzi na kushika utawala katika kipindi alichoita "udikteta wa wafanyakazi".
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.