From Wikipedia, the free encyclopedia
Koloni ni neno linalotumiwa kwa kutaja:
Asili ya neno koloni ni Kilatini "colonia" kutokana na kitenzi "colere" (kulima, pia kuabudu). Colonia ilikuwa makazi ya Waroma wa Kale nje ya eneo lao la awali. Chanzo chake kilikuwa mji mpya uliokaliwa na wanajeshi wastaafu waliopewa ardhi kwa ajili ya mashamba kama pensheni yao.
Makoloni ya aina hiyo yalianzishwa hasa mpakani mwa maeneo mapya yaliyotwaliwa karibuni na kungizwa katika Dola la Roma. Walowezi walipewa mashamba yao kwa masharti ya kuwa tayari kutetea mipaka kama vita inatokea.
Makoloni yalienea hasa tangu upanuzi wa nchi za Ulaya kuanzia karne ya 15 kwa maana ya maeneo yaliyo chini ya nchi nyingine ambayo iko mbali. Makoloni hayo yalianzishwa kwa njia mbalimbali:
Hasa mwisho wa karne ya 19 nchi za Ulaya zilitwaa maeneo na kuyafanya makoloni kwa hofu ya kwamba nchi nyingine itayachukua. Kuwa na koloni kulikuwa kama dalili ya kuwa nchi yenye maana inayoheshimiwa. Mwisho wa karne hiyo takriban 80% za maeneo yote duniani yalitawaliwa kama koloni la namna moja au nyingine.
Kipindi hiki cha ukoloni kiliporomoka baada ya vita kuu ya pili ya dunia, ila kukawa na mwendelezo wake katika ukoloni mamboleo.
Hali za nchi chini ya utawala wa kikoloni zilitofautiana.
Kuna mifano ambapo hali ya kuwa nchi lindwa ilidumu muda mfupi tu kabla ya kumezwa kabisa na kuwa sehemu ya koloni kamili. Mfano wake mmojawapo ni usultani wa Witu ulioingizwa katika koloni la Kenya bila kujali mawazo ya mtawala mwenyeji au ya watu wake.
Lakini kuna pia mifano ambapo mikataba asilia na wenyeji iliheshimiwa na mwisho wa ukoloni maeneo haya yamekuwa nchi huru. Kati ya mifano yake ni Falme za Kiarabu na Botswana iliyokaa nchi ya pekee nje ya Afrika Kusini ingawa serikali ya Afrika Kusini ilitaka iwe chini yake.
Kwa jumla Uingereza ulipendelea mara nyingi kutawala kupitia wenyeji kuliko kuwatawala moja kwa moja. Utawala wa moja kwa moja ulipendelewa kwa mfano na Ufaransa katika makoloni yake.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Koloni kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.