From Wikipedia, the free encyclopedia
Nchi huru ni zile ambazo hazitawaliwi na nchi nyingine. Kauli hiyo haimanishi kwamba wananchi wake ni huru, kwa sababu pengine mfalme au rais ni mwenyeji, lakini anawanyima haki zao kwa kiasi hata kikubwa (ambacho kinaitwa udikteta).
Mara nyingi nchi inajitangaza huru, halafu inatambuliwa na nchi nyingine kuwa hivi. Kama si nchi zote zinatambua rasmi uhuru wake, hali ya kisheria inabaki tata.
Siku hizi duniani kuna nchi huru karibu 200, ya mwisho kutambulika ikiwa Sudan Kusini (2011) na ndogo zaidi ikiwa Mji wa Vatikano (km2 0.44 na wakazi 600 hivi tu).
Hii haiuzii nchi kuingiliwa kwa namna moja au nyingine kama vile katika ukoloni mamboleo.
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.