jiji katika Jimbo la New York, Marekani From Wikipedia, the free encyclopedia
New York (Kiing.: "New York City") ni jiji kubwa kabisa Marekani na kati ya miji mikubwa duniani. Iko kwenye pwani la kaskazini-mashariki ya Marekani katika jimbo la New York.
Jiji la New York City | |
Mahali pa mji wa New York City katika Marekani |
|
Majiranukta: 40°42′15″N 73°55′5″W | |
Nchi | Marekani |
---|---|
Jimbo | New York |
Wilaya | New York Kings Queens Bronx Richmond |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 8,336,697 |
Tovuti: www.nyc.gov |
Mji uko kwenye mdomo wa pamoja ya mito Hudson na East River inapoishia katika Atlantiki kwa 40°42N 74°00W.
Kitovu cha mji kipo kwenye kisiwa cha Manhattan kilichopo kati ya Hudson na East River. Eneo la jiji ni funguvisiwa kwenye mdomo huo na visiwa vyake pamoja na Manhattan ni Staten Island, Long Island na visiwa vingine vidogo kwa mfano kisiwa cha Ellis na kisiwa cha Sanamu ya Uhuru (statue of liberty).
Jiji limepanuka kutoka kando za mito hadi barani. Eneo lote la jii ni kilomita za mraba 831.4.
Ndani ya jiji kuna mitaa au wilaya tano zinazoitwa boroughs ambazo ni:
Jina la Manhattan lakumbuka wakazi asilia waliokuwa Maindio wa Lenape na "manhattan" ni neno la lugha yao "Manna-hata" lililomaaanish a "kisiwa cha milima mingi". Mzugu wa kwanza aliyefika alikuwa nahodha Mwitalia Giovanni da Verrazano mwaka 1524 halafu Mwingereza Henry Hudson mwaka 1609.
Mji mwenyewe ulianzishwa na Waholanzi kwa jina la "Nieuw Amsterdam" (Amsterdam Mpya). Mwaka 1626 kisiwa cha Manhattan kilinunuliwa kwa 60 gulder kutoka wenyeji kikawa mji mkuu wa koloni ya Nieuw Nederland (Uholanzi Mpya).
Mwaka 1664 baada ya vita kati ya Uholanzi na Uingereza koloni yote ilihamishwa upande wa Uingereza pamoja na mji mwenyewe ikapewa jina jipya la "New York".
Katika karne ya 18 New York ilikuwa sehemu ya uasi dhidi ya Uingereza
Kipindi kikubwa cha mji kulitokea katika karne ya 19 wakati wahamiaji wengi sana walipofika MArekani. Idadi kubwa walifika kwenye bandari la New York.
Baada ya fitina kati ya watu wa kusini na wenyeji wa kaskazini serikali ya Kiingereza ilifunga kambi hilo.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.