Uholanzi
nchi katika Ulaya Kaskazini Magharibi From Wikipedia, the free encyclopedia
Uholanzi ni nchi ya Ulaya ya Magharibi. Imepakana na Ujerumani upande wa mashariki, Ubelgiji upande wa kusini na Bahari ya Kaskazini (North Sea) upande wa magharibi na kaskazini. Uholanzi ni sehemu ya "Ufalme wa Nchi za Chini" (Kingdom of the Netherlands) pamoja na visiwa vya Aruba, Curaçao na Sint Maarten, mbali ya visiwa vingine vitatu vya Karibi vya Uholanzi.Lugha rasmi ni Kiholanzi, na Kifrisia cha Magharibi kama lugha rasmi ya pili katika jimbo la Friesland
Nederland (Kiholanzi) | |||
![]() |
![]() |
||
Kauli Mbiu "Je maintiendrai" (Kifaransa) ("Nitadumisha") |
|||
Wimbo wa taifa Wilhelmus (Kiholanzi) |
|||
Eneo la Uholanzi katika Umoja wa Ulaya |
|||
Jiji kubwa (na mji mkuu) |
Amsterdam | ||
---|---|---|---|
Lugha rasmi | Kiholanzi | ||
Kabila |
|
||
Dini | |||
Utaifa | Mholanzi | ||
Aina ya Serikali | Ufalme wa kikatiba wa bunge la umoja | ||
Mfalme | Willem-Alexander | ||
Waziri Mkuu | Dick Schoof | ||
Ukubwa wa eneo | |||
Jumla | 41,865 km² | ||
Asilimia ya maji | 18.41 % | ||
Idadi ya watu | |||
Kadirio (2025) | 18,270,300 | ||
Sensa (2011) | 16,655,799 | ||
Msongamano | 520 /km² | ||
Pato la taifa PPP (2024) | |||
Jumla | $1.460 Trilioni [1] (ya 9) | ||
Capita | $81,494 [1] | ||
Pato la taifa (2024) | |||
Jumla | $1.218 Trilioni [1] (ya 7) | ||
Capita | $67,984 [1] | ||
Kiashiria cha maendeleo ya watu (2022) | 0.946 [2] (11) Maendeleo ya Juu Sana |
||
Kiashiria cha ukosefu wa usawa (2022) |
38.7
Ukosefu wa usawa wa kati |
||
Sarafu | Euro Dola ya Marekani |
||
Eneo la saa | TC+01:00 (CET)UTC−04:00 (AST) | ||
Nambari ya mwito | +31 +599 |
||
Upande wa gari | Kulia | ||
Jina la kikoa | .nl .bq |
Jina la Uholanzi limetokana na “Holland”, eneo la magharibi la nchi hii. Watu wengi hutumia jina hilo, lakini wakazi wenyewe wanaiita nchi yao “Nederland” inayomaanisha "nchi ya chini". Kwa kweli, sehemu kubwa ya Uholanzi iko chini ya usawa wa bahari. Waholanzi wamejenga maboma kuzuia maji yasienee yakifurika.
Jiografia
Akifika Uholanzi kwa uwanja wa ndege wa Schiphol, msafiri anastaajabu nchi ilivyo tambarare. Kwa kweli, kuna sehemu zenye vilima, lakini sehemu kubwa zaidi ya Uholanzi ni tambarare.
Mahali pa juu kabisa nchini ni Kilima cha Vaals, upande wa kusini wa mkoa wa Limburg, kwa 322 m. Mahali pa chini kabisa ni karibu na Nieuwerkerk aan de IJssel, mkoa wa Zuid Holland, kwa -6.76 m (mita 6.76 chini ya usawa wa wastani wa bahari).
Vipande vikubwa vya nchi vimepatikana kutoka ziwa au bahari. Ili kufanya hivyo boma linajengwa kuzunguka ziwa au sehemu ya bahari, kisha maji yanavutwa kwa bomba. Mahali kati ya boma huitwa “polder”. Mkoa mmoja mzima, Flevoland, umepatwa kwa maji ya “Zuiderzee” (Bahari ya Kusini). Kwa sababu hiyo watu husema: “Mungu aliumba dunia lakini Waholanzi waliumba Uholanzi.” Hata sasa sehemu muhimu ya Uholanzi ni maji: 18%.

Maboma mengine makubwa yamejengwa upande wa kusini magharibi wa nchi ili ya kuzuia maji yasienee mikoa ya Zeeland na Zuid Holland. Mradi huu huitwa “Deltawerken” au Ujenzi wa Delta. “Oosterscheldekering” au boma la mto wa Oosterschelde ni jengo linaloshangaza. Urefu wake ni 9 km na katikati yake kuna malango makubwa 62 ambayo hujifunga wenyewe kila wakati ambapo maji ya bahari yakifura zaidi ya 3 m. Barabara kuu inapitia juu ya boma hili.
Mito
Mito mikubwa kadhaa inaingia Uholanzi na kutiririka katika Bahari ya Kaskazini. Mto Rijn (Mto Rhine) unaingia kwa Tolkamer upande wa mashiriki, na karibu na Nijmegen Mto Waal unajitenga ambao unachukua 70% ya maji. Mto IJssel unajitenga karibu na Westervoort na kwenda upande wa kaskazini. Mto Maas (Mto Meuse) unaingia Uholanzi upande wa kusini wa Limburg, na karibu na Mook unageuka upande wa magharibi. Mto Schelde unaingia upande wa kusini wa Zeeland.
Mikoa

Uholanzi umegawanyika katika mikoa 12. Kila mkoa unatawaliwa na gavana ambaye huitwa “Commissaris van de Koningin” isipokuwa yule wa Limburg ambaye huitwa “Gouverneur”. Mikoa na miji mikuu yao ni :

Miji mikubwa
Mji | Wakazi |
---|---|
Amsterdam | 742,011 |
Rotterdam | 600,000 |
Den Haag | 476,000 |
Utrecht | 281,569 |
Eindhoven | 209,399 |
Trafiki
Katika Uholanzi barabara daima zina msongamano wa magari. Hii ni kwa sababu watu wanakwenda kazini asubuhi hadi kurejea jioni, na wanaoishi Uholanzi ni wengi, na kufanya kazi nyingi sana.
Historia
Kisha kutekwa na Julius Caesar katika karne ya 1 KK, kusini mwa nchi ikawa mpaka wa kaskazini wa Dola la Roma hadi lilipokoma (karne ya 5).
Baadaye nchi ilivamiwa na makabila mbalimbali ya Wagermanik: Wasaksoni, Wabatavi, Wafrisi na Wafaranki.
Katika karne ya 8 nchi ilikuwa sehemu ya dola la Karolo Mkuu, na katika karne ya 10 ya Dola Takatifu la Kiroma.
Baadaye mfumo wa ukabaila ulitawala nchi sehemu sehemu.
Katika karne ya 16 nchi ilikuwa chini ya familia ya makaisari (Absburg), lakini ilipokea Matengezo ya Kiprotestanti kinyume cha matakwa ya kaisari Karolo V.
Mwanae Filipo II wa Hispania alipomrithi hakukubali jambo hilo na kusababisha uasi ulioenea kote (1566-1581) hadi wilaya saba zilipounda jamhuri iliyotambuliwa na Hispania mwaka 1648 tu, katika amani ya Westfalia.
Karne ya 17 ndipo nchi ilipofikia kilele cha ustawi wake, ikiwa na makoloni mengi huko India, Indonesia, Afrika na Amerika, pamoja na biashara kubwa ya kimataifa duniani kote.
Karne iliyofuata Uingereza ulishika nafasi hiyo ya Uholanzi.
Baada ya mapinduzi ya Kifaransa (1789) nchi ilitekwa na Wafaransa hadi Amani ya Vienna (1814-1815) iliyopanua Uholanzi huru tena, lakini kwa mfumo wa ufalme.
Hata hivyo mwaka 1830 Ubelgiji ulijitenga na mwaka 1890 Luxemburg ilifanya vilevile.
Uholanzi haukutaka kushiriki Vita vikuu vya kwanza vya dunia, lakini katika vita vikuu vya pili ulivamiwa na Ujerumani (1940-1945).
Baadaye Uholanzi umejitahidi sana kushiriki katika mahusiano ya kimataifa na ni kati ya nchi waanzilishi wa Umoja wa Ulaya.
Watu
Wakazi wengi wana asili ya makabila ya Kijerumani, lakini kuna wahamiaji wengi pia kutoka nchi nyingi. 22% za wakazi wana walau mzazi mmoja kutoka nchi za nje.
Lugha ya kawaida ni Kiholanzi.
Upande wa dini, takwimu za serikali zinaonyesha kwamba mwaka 2015, 50.1% ya wakazi hawakuwa na dini yoyote, 43.8% walikuwa Wakristo (23.7% Wakatoliki, 21.1% Waprotestanti, hasa Wakalvini, 4.9% Waislamu, 1.1% Mabanyani, Wabuddha n.k.
Tazama pia
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.