From Wikipedia, the free encyclopedia
Flevoland ni moja kati ya mikoa ya nchini Uholanzi. Mkoa upo katikati ya nchi, katika eneo la zamani la Zuiderzee. Mkoa ulianzishwa mnamo tar. 1 Januari 1986; ukiwa kama mkoa wa kumi na mbili nchini Uholanzi, na Lelystad ukiwa kama mji mkuu wake. Mkoa huu una wakazi takriban 370,000 ([ripoti] 2005) ikiwa na pamoja na manispaa zipatazo 6.
Jimbo lote la Flevoland ni nchi mpya; hadi 1936 eneo lake lilikuwa eneo la hori kubwa ya Bahari ya Kaskazini yenye umbo la kidaka iliyoitwa Zuidersee. Baada ya mafuriko ya mwaka wa 1916, ikaamuliwa ya kwamba Zuiderzee iliyoungana na Bahari ya Kaskazini kwa mdomo mwembamba itatengwa na bahari kuu kwa lambo. Mwaka wa 1932, lambo la "Afsluitdijk" ikakamilika, ambayo ilifunga bahari kabisa. Zuiderzee baadaye ikaitwa IJsselmeer (ziwa mwishoni kabisa mwa mto IJssel).
Eneo la hori ya awali liligawiwa kwa malambo ya ndani na maeneo kati ya malambo ya ndani yasiyo na kima kikubwa yalikaushwa kwa njia ya pampu nyingi zilizovuta maji kutoka ndani ya malambo. Kwa njia hii sehemu za bahari ya awali zilikuwa nchi kavu. Mifereji mingi ilisaidia kuondoa maji zaidi kwenye adhi. Baada ya kupanda manyasi na na mazao maalumu kwa miaka mfululizi kiasi cha chumvi katika ardhi ilipungua hadi kufa kwa kilimo cha kawaida.
Tangu 1930 nyumba za kwanza kwa wakulima zilijengwa juu ya nchi mpya. Mji wa kwanza tangu 1966 ulikuwa Lelystad iliyoendelea kuwa makao makuu ya jimbo jipya.
Mikoa ya Uholanzi | |
---|---|
Drenthe | Flevoland | Friesland | Gelderland | Groningen | Limburg | Noord-Brabant | Noord-Holland | Overijssel | Utrecht | Zeeland | Zuid-Holland | |
+/- |
Makala hii kuhusu maeneo ya Uholanzi bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Flevoland kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.