From Wikipedia, the free encyclopedia
Kirgizia (pia Kirgizstan, Kirigizistani au Kigistani; kwa Kikirgizi: Кыргызстан (Kyrghyzstan); kwa Kirusi: Киргизия (Kirgizia)) ni nchi ya Asia ya Kati.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: -- | |||||
Wimbo wa taifa: Wimbo la Taifa la Kirgizia | |||||
Mji mkuu | Bishkek | ||||
Mji mkubwa nchini | Bishkek | ||||
Lugha rasmi | Kikirgizi, Kirusi | ||||
Serikali | Jamhuri Sadyr Japarov Akylbek Japarov | ||||
Uhuru ilitangazwa Ilikamilishwa |
31 Agosti 1991 25 Desemba 1991 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
199,951 km² (ya 87) 3.6 | ||||
Idadi ya watu - 2020 kadirio - 2009 sensa - Msongamano wa watu |
6,586,600 (ya 110) 5,362,800 27.4/km² (ya 176) | ||||
Fedha | Som ya Kirgizia (KGS ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
KGT (UTC+6) (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .kg | ||||
Kodi ya simu | +996
- |
Imepakana na Kazakhstan, Uzbekistan, Tajikistan na China.
Neno "Kirgizia" linamaanisha "nchi ya makabila 40" kwa lugha ya Kikirgizi. Ukweli ni kwamba kwa sasa yako 80 na zaidi.
Hadi mwaka 1991 Kirgizia ilikuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyet, ikijulikana kwa jina la "Jamhuri ya Kisovyeti ya Kikirgizi".
Ilipata uhuru wake katika mwendo wa kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti.
Kabla ya uhuru yalitokea mabadiliko katika uongozi wa chama cha kikomunisti. Viongozi wapya waliotafuta njia bila udikteta mkali walishika uongozi na rais Askar Akayev alirudishwa madarakani katika uchaguzi wa kwanza na wa pili.
Lakini uchaguzi wa mwaka 2005 ulionekana haukuwa huru, hivyo hasira ya wananchi ikalipuka katika mapinduzi. Uchaguzi mpya ukamteua mpinzani wa awali Kurmanbek Bakiyev.
Hii ni orodha ya mikoa ya Kirgizia pamoja na makao makuu yake:
Idadi ya wakazi ilihesabiwa 2005 kuwa watu 5,264,000. Takriban 72.6 % kati yao ni Wakirgizi wenyewe, ambao ni jamii ya Waturuki halafu kuna Wauzbeki (14.4 %) hasa kusini na Warusi (6.4 %) hasa kaskazini, mbali na makundi madogo zaidi.
Lugha ya kawaida ni Kikirgizi, ambacho ni lugha rasmi pamoja na Kirusi. Angalia pia orodha ya lugha za Kirgizia.
Takriban 64% ni Waislamu, lakini kuna uhuru wa dini. Wakristo wako hasa katika ya wakazi wenye asili ya Ulaya, wakiwemo kwanza Waorthodoksi, halafu Waprotestanti na Wakatoliki wachache.
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China. |
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kirgizia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.