Hasira ni ono linalowapata binadamu na wanyama mbele ya kipingamizi. Katika hali hiyo mtu hughadhibika, hata kuchukia kwa kupatwa na kitu ambacho yeye mwenyewe hapendi.

Hasira ya Akile dhidi ya Agamemnon ilivyochorwa na Giovanni Battista Tiepolo.
Maelezo zaidi Vilema vikuu ...
Funga

Mtu mwenye hasira ya mara kwa mara, hushauriwa ajaribu kuepuka mambo au vitu vinavyomuudhi, kwa mfano, anaweza kuondoka mahali penye maudhi, na kama ni kubishana aweze kunyamaza ili kuepukana na ugomvi.

Pia inashauriwa kuwa, kama unajua mwenzio hukasirishwa na kitu fulani, bora usimchokoze, kwa sababu ni hatari kwa maisha yako maana kwa hasira yake anaweza kufanya kitu chochote kibaya.

Isiporatibiwa na mhusika inaweza ikasababisha madhara makubwa, inavyofundisha mithali ya Kiswahili, "Hasira, hasara". Hasira hupelekea mtu kuvunja sheria kwa kujichukulia hatua mkononi na mwishowe kufanya jambo la hatari.

Ndiyo sababu inahesabiwa kati ya vilema vikuu ambavyo ni mizizi ya dhambi nyingine.

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.