Remove ads
From Wikipedia, the free encyclopedia
Liturujia ya Canterbury ni madhehebu yanayoendeleza mambo bora ya Anglikana ndani ya Kanisa la Kilatini.
Mwaka 2011 na 2012 Papa Benedikto XVI alianzisha majimbo matatu kwa Waanglikana walioamua kujiunga na Kanisa Katoliki kama makundi.
La kwanza lilianzishwa kwa wale wa Uingereza na Wales (lakini pia Uskoti), la pili kwa wale wa Marekani (baadaye liliongezewa wale wa Kanada)[1][2], la tatu kwa wale wa Australia (halafu pia Japani). Jumla ya waamini ni 10,000 hivi, chini ya mapadri 190, wengi wao wakiwa na ndoa.
Kila mojawapo linaongozwa na padri mwenye ndoa aliyewahi kuwa askofu wa Kianglikana, isipokuwa lile la Marekani ambalo limepewa askofu wa kwanza ambaye ni mseja.
Kabla ya hapo kulikuwa na parokia tu za namna hiyo huko Marekani na Kanada, zikifuata hati maalumu ya Papa Yohane Paulo II ya tarehe 20 Juni 1980,[3][4][5]
Tarehe 9 Desemba 2009, Benedikto XVI alitoa hati Anglicanorum Coetibus, iliyoweka taratibu za uanzishaji wa majimbo yasiyopakana na majimbo ya kawaida ya Kilatini kwa Wakristo wa namna hiyo[6], na kufikia mwisho wa mwaka 2015 parokia zote zilizoanzishwa kabla ya hapo isipokuwa 2 zimejiunga na jimbo la Kimarekani. Mkutano maalumu kwa ajili hiyo ulifanyika tarehe 8-10 Novemba 2012[7].
Kwa niaba ya Papa, Idara ya Ibada ya Kimungu ilipitisha the Book of Divine Worship kwanza kwa muda mwaka 1984, halafu moja kwa moja mwaka 1987.[4] Kuanzia tarehe 29 Novemba 2015 nafasi yake imeshikwa na "Divine Worship: The Missal".
Ibada nyingine kwa ajili ya ndoa na mazishi zilipitishwa na idara hiyo tarehe 22 Juni 2012[8].
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.