From Wikipedia, the free encyclopedia
Neema ni jambo lolote jema ambalo binadamu anapata katika maisha yake.
Neno hilo kwa Kiswahili ni pana, lenye maana mbalimbali, kama vile mema ya kiroho na ya kiuchumi, lakini zote zinaelekeza kumfikiria Mwenyezi Mungu kama asili yake kuu. Ni huruma ya Mungu kwa wanadamu inayoambatana na baraka.
Teolojia katika dini mbalimbali inatumia neno hili kadiri ya imani yake maalumu.
Kwa namna ya pekee neno linatiwa mkazo katika Ukristo unaosisitiza kwamba mambo yote ni neema (kwa Kigiriki: χάρις, kharis; kwa Kilatini: gratia, yaani deso, kitu cha bure).
Hata hivyo madhehebu yake yanatofautiana sana katika kutafsiri tamko hilo.
Neema ni msaada wowote tunaopewa bure na Mungu ili tupate kufika mbinguni. (Lk 1:30; Rum 5:2,20; Fil 2:13)
Kanisa Katoliki linasadiki kwamba Mungu anawapa watu wote neema za kutosha ili wapate kuokoka (Mdo 10:34-35; 1Pet 4:10-11) na kwamba Yesu Kristo ndiye aliyetustahilia neema zote kwa njia ya mateso, kifo na ufufuko wake. (Mdo 15:11)
Vilevile linasadiki kwamba Roho Mtakatifu ndiye anayetugawia neema hizo kwa ajili ya Kanisa. (Yoh 1:16; 3:3-8) na kwamba mtu anaweza kujipatia neema kwa njia ya sakramenti, sala na matendo mema. (Yak 5:16-20)
Neema ni za aina mbalimbali:
Neema za msaada ni fadhili mbalimbali ambazo Roho Mtakatifu anasaidia akili na utashi wa mtu kuanza, kuendeleza na kutimiza kazi ya wokovu wake kwa kutenda mema na kuepuka mabaya. (Yoh 15:5; Fil 2:13; 1Tim 2:4)
Neema ya utakaso ndiyo muhimu zaidi kwa sababu ni uzima wa Mungu unaotiwa rohoni mwa mtu aweze kutenda kwa upendo wake na kujiandaa kuishi naye milele. (Yoh 1:16; 3:3-8; Ef 3:4-7; 2Pet 1:3-4)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.