Remove ads
From Wikipedia, the free encyclopedia
Msalaba ni ishara inayotokana na mistari miwili kukutana katikati yake.
Hiyo ni mojawapo kati ya ishara maarufu na ya zamani zaidi duniani kote, katika sanaa, utamaduni na dini, hasa Ukristo unaoheshimu kama ukumbusho wa kifodini cha mwanzilishi wake, Yesu Kristo, aliyekufa kwa njia ya usulubisho.
Msalaba ulikwishatumiwa na Wakristo wa kale sana. Mwanzoni mwa karne ya 3 Tertullianus, katika kitabu "De Corona", alisema kwamba walikuwa na desturi ya kujifanyia ishara hiyo katika paji la uso.
Lakini alama ya msalaba au za kufanana na msalaba zinapatikana pia katika tamaduni mbalimbali tangu kale bila uhusiano wowote na Ukristo.
Misalaba iliyotumiwa kwa adhabu ya kifo iliweza kuwa na maumbo mbalimbali, hata kuwa ubao mmoja tu bila mikono ya kando.
Picha | Jina la Msalaba | Maelezo |
---|---|---|
Msalaba wa Misri ya Kale |
Ankh au msalaba wa Misri; ni ishara kutoka utamaduni wa Misri ya Kale na ni ya kale zaidi kuliko msalaba wa Kikristo. Kwa Wamisri ilikuwa ishara ya uhai na uzao. Baadaye ilitumiwa pia katika sanaa ya Wakristo. Unajulikana pia kwa jina la Kilatini crux ansata ("msalaba wenye mikono"). | |
Msalaba wa Kikristo |
Umbo hili linajulikana pia kama msalaba wa Kilatini. Ni ishara itumiwayo na Wakristo wengi kama kumbukumbu ya Yesu Kristo na kifo chake kwa njia ya usulubisho na pia ufufuko wake. | |
Msalaba wa Jua , Msalaba wa Kibulgaria |
Huu ni ishara ya kale kabisa inayopatikana tangu zamani za zama za mawe. Unaaminika kumaanisha jua. Katika sanaa ya Kikristo ulipatikana hasa Bulgaria kama ishara ya Kanisa la Bulgaria. Siku za nyuma imetumiwa pia na Wapagani wa kisasa. | |
Msalaba wa Kikelti |
Unapatikana katika sanaa ya Wakristo Wakelti hasa Eire na pia katika sehemu kadhaa za kisiwa cha Britania kama msalaba juu ya makaburi na katika makanisa. | |
Msalaba wa Canterbury |
Unapatikana hasa katika makanisa ya Kianglikana. | |
Msulubiwa |
Ni msalaba wenye sanamu ya mwili wa Yesu juu yake. | |
Msalaba wa Kiserbia (Msalaba wenye herufi nne kandokando) |
Unatokana na bendera ya Konstantino Mkuu na kupatikana katika sarafu za Bizanti kuanzia karne ya 6. Kuanzia Karne za kati umetumiwa na nchi ya Serbia na Kanisa lake la Kiorthodoksi. Hadi leo ni kitambulisho cha taifa hilo. | |
Msalaba wa Mt. Floriano |
Unatumiwa na zimamoto kutokana na msimamizi wao Floriani. Unafanana na ule wa Malta isipokuwa ncha za mikono yake ni za mviringo. | |
Msalaba wa Mashariki |
Unatumika katika Makanisa ya Kiorthodoksi. Mkono wa kushoto unainuka, kutokana na dhana ya kuwa ndio upande wa mhalifu aliyetubu msalabani karibu na Yesu: hivyo unamaanisha ushindi wa wema dhidi yas ubaya. Herufi IC XC (C inasomeka S) ni za kawaida katika Ukristo wa Mashariki zikiwa na maana ya jina la Yesu, kwa Kigiriki Ιησούς Χριστός, Iesus Khristos. | |
Msalaba wa Mt. Birgita |
Msalaba huu unapatikana kote nchini Ireland. Inasemekana Brigit (au Brigid, Brìghde, Brìde na Bríde) alikuwa mungu jike wa moto katika dini ya Waselti kabla ya Ukristo kuenea. | |
Chi-Rho |
Ishara ya Konstantino Mkuu, Chi-Rho inatokana na herufi mbili ya alfabeti ya Kigiriki. | |
Msalaba wa Lorraine |
Unatumika katika ngao ya Lorraine, Ufaransa. Inasemekana ulikuwa kwanza ishara ya Yoana wa Arc, msichana aliyeongoza mapigano dhidi ya Waingereza waliovamia nchi yake. | |
Msalaba wa Kimaria |
Ukiwemo katika ngao ya Papa Yohane Paulo II, unasisitiza heshima ya Wakatoliki kwa Bikira Maria aliyesimama chini ya msalaba wa Mwanae huko Golgota. | |
Msalaba wa Kaskazini |
Unatumika katika bendera za nchi za Skandinavia kama ishara ya Ukristo; nchi asili ni Denmark. | |
Msalaba wa Occitania |
Ukitokana na ngao ya mtawala wa Toulouse, Ufaransa, umekuwa ishara ya Ufaransa Kusini nzima. | |
Msalaba wa Kipapa |
Mbao tatu zinazokatisha mhimili wa msalaba zinamaanisha mamlaka ya Papa kama Askofu wa Roma, Patriarki wa Magharibi na mwandamizi wa Mtume Petro, mkuu wa Mitume wa Yesu. | |
Msalaba wa Kipatriarki |
Mbao mbili zinazokatisha mhimili wa msalaba zinamaanisha mamlaka ya askofu mkuu na Patriarki katika Makanisa ya Kiorthodoksi. | |
Msalaba wa Kipresbiteri | Unatumiwa na madhehebu ya Wakalvini. | |
Msalaba Mwekundu |
Unatumika katika sehemu kubwa ya dunia kumaanisha shughuli za kitabibu. | |
Msalaba wa Sadaka |
Msalaba wa Kilatini ukiwa na upanga juu yake, ncha yake ikielekea chini, unatumika katika shamba la Mungu la askari wa Jumuia ya Madola waliouawa vitani. | |
Msalaba wa Salem |
Unachukuliwa pengine mbele ya Papa, ukiwa na ubao mmoja kuliko msalaba wa Kipatriarki, lakini upande wa chini, si wa juu kama katika msalaba wa Kipapa. | |
Msalaba wa Georgia |
Unatumika nchini Georgia kama bendera ya taifa. | |
Msalaba wa Shada, Msalaba wa Mt. Nino |
Unajulikana pia kama "Msalaba wa mzabibu"; inasemekana ulitumiwa kwanza na Mt. Nino, mwanamke wa karne ya 4 aliyeingiza Georgia katika Ukristo. Ni ishara ya Kanisa la Kiorthodoksi la Georgia. | |
Msalaba wa Nasrani Menorah Msalaba wa Mt. Thoma |
Unasemekana kutumiwa kwanza na Mtume Thoma, aliyeeneza Ukristo hadi India, na unatumiwa na Kanisa Katoliki la Kisiria la Malabar kama ishara yake, pamoja na kwamba inaheshimiwa na Wakristo wote wa Mashariki wa nchi hiyo.[1] | |
Msalaba wa Mt. Andrea |
Unapatikana katika bendera ya Scotland na kuitwa kwa Kilatini crux decussata. Inasemekana Mtume Andrea aliuacha juu ya msalaba wa namna hiyo. | |
Msalaba wa Mt. Joji | ||
Msalaba wa Mt. Petro, Msalaba uliopinduliwa |
Unaitwa kwa jina la Mtume Petro kutokana na mapokeo ya kwamba alitaka kusulubiwa kichwa chini, miguu juu. Siku hizi unatumiwa na wafuasi wa dini ya Shetani kama ishara ya kumpinga Kristo. | |
Msalaba wa Tau, crux commissa |
Unajulikana pia kama msalaba wa Antony Abati, kwa hiyo pia kama Msalaba wa Misri; unakosa upande wa juu ya msalaba, hivyo ni kama herufi T. Fransisko wa Asizi aliutumia kama saini. | |
Msalaba wa Wezi |
Una sura ya msalaba uliotumika zamani kuua wezi ukifanana kama herufi Y. | |
Msalaba wa Baharia |
Unafanana na nanga, hivyo unatumiwa na mabaharia. Unaitwa pia kwa jina la Papa Klementi I kutokana na namna alivyouawa kwa ajili ya imani yake. | |
Msalaba wa Shirika la Kristo |
Umekuwa kitambulisho cha Ureno, kutokana na shirika la zamani la nchi hiyo lililoitwa Shirika la Kristo. | |
Mikono ya Mungu |
Ni ishara iliyotumiwa katika Ulaya ya Kati kabla Ukristo haujaingia. | |
Swastika |
Ni msalaba ambao mbao zake zinalingana kwa ukubwa, halafu zina matawi 4 ya ziada kuelekea kulia au kushoto. Ulitumika tayari katika Zama za mawe na mpaka leo hasa nchini India na katika dini zilizotokea huko. Ulitumiwa pia na Adolf Hitler, na tangu hapo unachukiwa na wengi. | |
Fuvu la Kichwa na Mifupa |
Si msalaba, ila ni ishara iliyowekwa mara nyingi upande wa chini wa msalaba. | |
Bendera nyingi zinabeba ishara ya msalaba.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.