Kanisa Katoliki la Kisiria la Malabar

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kanisa Katoliki la Kisiria la Malabar

Kanisa Katoliki la Kisiria la Malabar ni mojawapo kati ya madhehebu ya Ukristo wa mashariki yenye ushirika kamili na Papa na Kanisa Katoliki lote.

Mar Thoma Sliva, yaani Msalaba wa Mt. Thomas, ni ishara ya Kanisa la Kisiria la Malabar.
Kardinali Mar George Alencherry, askofu mkuu kabisa wa Kanisa hilo.
Kanisa la Mt. Maria huko Arakuzha, Kerala lilijengwa mwaka 999.
Undani wa kanisa mojawapo la Kerala, ukionyesha Patakatifu pa Patakatifu palipo msalaba wa Mtume Thoma uliofunikwa na kitambaa chekundu.

Linafuata mapokeo ya Mesopotamia na kutumia liturujia ya Mesopotamia, lakini linapatikana hasa India na katika nchi mbalimbali ambapo waamini wake wamehamia, kama vile Marekani, ambako lina majimbo mawili, na Kanada, Australia na Britania ambako kuna jimbo mojamoja.

Kwa jumla lina waumini milioni 4-5, wakiongozwa na askofu mkuu kabisa wa Ernakulam-Angamaly na maaskofu wengine 63, mapadri 9,121 katika parokia 3,224.

Kanisa hilo ndiyo madhehebu kubwa kuliko yale yote yanayosisitiza kuwa yametokana na kazi ya Mtume Thoma.

Kati ya waamini wake, sista Mfransisko Alfonsa Matathupadathu alitangazwa mtakatifu na Papa Benedikto XVI tarehe 12 Oktoba 2008. Baada yake wametangazwa watakatifu wengine watatu: padri Kuriakose Elias Chavara na masista Roza Eluvathingal na Maria Teresa Chiramel.

Kwa sasa Kanisa hilo lina masista 35,000 hivi na mabruda 6,836.

Kalenda ya kiliturujia

Kanisa hilo lina kalenda maalumu kwa mwaka wa liturujia inayofuata mwendo wa historia ya wokovu na kiini chake kikiwa maisha ya Yesu.[1] Majira ya pekee ni tisa:

  1. Kupashwa habari (Suvara)
  2. Kuzaliwa kwa Yesu
  3. Epifania (Denha)
  4. Mfungo Mkuu (Sawma Rabba)
  5. Ufufuko (Qyamta)
  6. Mitume (Slihe)
  7. Majira ya joto (Qaita)
  8. Eliya-Msalaba-Mose (Elijah-Sliba-Muse)
  9. Kutabarukiwa kwa Kanisa (Qudas-Edta)

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.