Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ilikuwa vita iliyopigwa kuanzia mwaka 1914 hadi 1918. Mataifa wapiganaji yalikuwa Ujerumani, Austria-Hungaria, Bulgaria na Uturuki (ziliitwa "Mataifa ya Kati", ing.central powers) kwa upande mmoja dhidi ya Ufaransa, Urusi, Uingereza, Italia, Marekani na nchi mbalimbali zilizoshirikiana nazo (zilitwa "Mataifa ya Ushirikiano", ing. allied powers).
Sababu yake ilikuwa mashindano makali kati ya mataifa ya Ulaya kuhusu kushika nafasi ya kipaumbele barani Ulaya na duniani kote.
Matokeo yake yalikuwa mwisho wa kipaumbele cha Ulaya duniani na kupanda ngazi kwa Marekani, mapinduzi katika nchi mbalimbali, mwisho wa falme za Ujerumani, Austria na Urusi pamoja na mwanzo wa utawala wa kikomunisti katika Urusi, mwisho wa Dola la Austria-Hungaria na wa Milki ya Osmani pamoja na mwisho wa ukoloni wa Kijerumani duniani.
Katika Ulaya nchi mpya zilijitokeza kama vile Chekoslovakia, Ufini, Latvia, Estonia, na Yugoslavia pamoja na nchi za zamani zilizotokea tena katika uwanja wa kimataifa ndizo Austria, Hungaria, Lithuania na Poland. Katika Mashariki ya Kati Uturuki ilianzishwa kama nchi mpya, ilhali kipindi kifupi cha ukoloni wa Uingereza na Ufaransa kilianza huko Syria, Iraq na Lebanoni.
Shirikisho la Mataifa liliundwa kama chombo cha kwanza kilicholenga kuunganisha nchi zote za Dunia na kuzuia vita mpya. Koloni za awali za Ujerumani na majimbo ya Kiarabu ya Milki ya Osmani zilidhaminiwa kwa Uingereza na Ufaransa kwa niaba ya Shirikisho, hatua iliyoweka maeneo haya chini ya uangalizi wa kimataifa, tofauti na koloni za kawaida.
Hali kabla ya vita
Sehemu kubwa ya Ulaya iliwahi kuwa na kipindi kirefu cha amani tangu vita kati ya Ufaransa na Ujerumani mnamo 1870-1871. Mataifa ya Ulaya yalikuwa na mfumo wa mikataba na mapatano kati yao yaliyolenga kuhakikisha uwiano wa mataifa. Mataifa makubwa ya Ulaya yalikuwa Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Urusi na Italia pamoja na milki ya Austria-Hungaria.
Hali ilikuwa tofauti katika Kusini-Mashariki mwa bara hilo. Hadi nusu ya pili ya karne ya 19 sehemu kubwa ya Balkani ilitawaliwa na Milki ya Osmani iliyokuwa milki ya Kiislamu ya kutawala Wakristo wengi. Milki hii iliendelea kudhoofika wakati wa karne ya 19. Nchi mbalimbali zilijitenga na kupata uhuru, kama vile Ugiriki, Serbia, Bulgaria na Romania. Nchi hizi mpya zilipigana kivita kati yao na Milki ya Osmani hadi mwaka 1912.
Mwanzo wa vita
Vita Kuu ilianza kutokana na ugomvi kati ya Austria-Hungaria na Serbia. Kutokana na muundo wa mikataba ya kusaidiana kati ya nchi za Ulaya mwanzo huo ulisababisha mfululizo wa hali ya vita kati ya mataifa, na mengine ya Balkani yaliyotafuta uhuru wao.
Tarehe 28 Juni1914 katika mji wa Sarayevo, Bosnia, mwana wa Kaizari wa Austria aliyekuwa mfalme mteule aliuawa pamoja na mke wake na mgaidiMserbia mwanachama wa kundi la "Mkono Mweusi" lililopinga utawala wa Austria-Hungaria katika Bosnia. Austria iliamuru Serbia ifuate masharti makali katika uchunguzi wa tendo lile. Serbia ilipokataa sehemu ya mwisho ya masharti, Austria ilitangaza hali ya vita dhidi ya Serbia tarehe 28 Julai1914.
Agosti ya 1914 iliona kupanuka kwa vita hiyo: Warusi walikuwa na mkataba wa usaidizi na Serbia wakatangaza hali ya vita dhidi ya Austria-Hungaria. Hapo wakaingia Wajerumani waliokuwa na mapatano ya usaidizi na Austria-Hungaria wakitangaza hali ya vita dhidi ya Urusi. Urusi kwa upande wake ulikuwa na mkataba wa kusaidiana na Ufaransa, kwa hivyo hali ya vita ikajitokeza pia kati ya Ufaransa na Ujerumani. Ujerumani ilishambulia Ufaransa kwa kuingia Ubelgiji na kupigana na jeshi la nchi hiyo. Mashambulio hayo yalisababisha Uingereza kujiunga na vita dhidi ya Ujerumani.
Japan iliyokuwa na mkataba wa kusaidana na Uingereza tangu mwaka 1902 iliona nafasi ya kukamata koloni za Ujerumani katika Bahari Pasifiki ikaingia upande wa maadui wa Ujerumani.
Kuanzia Oktoba 1914 Milki ya Osmani (Uturuki) ilijiunga na vita kufuatana na mkataba wake wa siri na Ujerumani.
Mwaka 1915 Italia ilijiunga na Wafaransa na Waingereza kwa kushambulia Austria-Hungaria iliyotawala bado maeneo katika kaskazini ya rasi ya Italia, ingawa awali ilikuwa na mkataba na dola hilo.
Vita katika nchi mbalimbali
Vita ilipigwa kwa ukali miaka ya 1914-1918. Wajerumani waliingia ndani ya Ufaransa lakini walikwama kabla ya kufikia jiji kuu la Paris. Kwa muda mrefu mstari wa mapambano ulibaki palepale.
Katika Mashariki Wajerumani na Waaustria walifaulu kurudisha mashambulio ya Kirusi na kuteka sehemu za Urusi.
Katika Kusini mwa Ulaya Waustria walifaulu kwa shida kubwa kuteka Serbia na Montenegro pamoja na Albania. Mapigano dhidi ya Italia yalikwama kwenye milima ya Alpi.
Waosmani walishindwa kwa ujumla katika mashambulio yao dhidi ya Warusi katika eneo la Kaukazi na dhidi ya Waingereza katika Misri. Lakini walifaulu kuzuia Waingereza wasifike Uturuki penyewe. Waingereza walipeleka jeshi katika Irak ya kusini wakafaulu kuwarudisha Waosmani hadi kaskazini ya nchi hii.
Vita ilienea haraka baharini na katika koloni za Ujerumani zilizovamiwa na Waingereza, Wafaransa, Afrika Kusini na Japani. Koloni hizo zilikuwepo Afrika na kwenye visiwa vya Pasifiki pamoja na China. Ujerumani ilikuwa na vikosi vya kijeshi katika koloni za Afrika na pia huko Qingdao nchini China.
Kwa ujumla koloni zote zisizokuwa na jeshi zilitekwa na mataifa ya ushirikiano bila mapigano.
Kamerun ilivamiwa na Ufaransa na Uingereza kutoka koloni zao za Nigeria na Afrika ya Kati ya Kifaransa. Wajerumani wakajisalimisha katika Februari 1916.
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani ilikuwa mahali pa mapigano yaliyoendelea kwa miaka yote ya vita. Jeshi la Ulinzi la Kijerumani lililoitwa Schutztruppe chini ya uongozi wa Paul von Lettow-Vorbeck lilifaulu kutetea eneo la koloni dhidi ya mashambulio ya kwanza ya Waingereza kutoka Kenya hadi 1916. Kwenye Novemba 1914 jeshi la askari 8,000 kutoka Uhindi lilishindwa kwenye mapigano ya Tanga. Hadi mwanzo wa 1916 Waingereza walikusanya jeshi kubwa kutoka Afrika Kusini na Uhindi wakafaulu kutwaa sehemu kubwa ya koloni hadi Agosti 1916. Jeshi la Schutztruppe likaendelea kushika sehemu ya kusini ya koloni hadi 1917 ilipopaswa kuhamia eneo la Kireno katika Msumbiji. Waingereza na Wareno walishindwa kulishika kundi la Kijerumani. Mwaka 1918 Lettow-Vorbeck alirudi Tanganyika akaingia Rhodesia ya Kaskazini alipoambiwa na Waingereza mnamo Novemba 1918 ya kwamba vita ya Ulaya ilikwisha tayari.
Mwisho wa vita
Wakati 1917 mataifa ya Ulaya yalionyesha dalili za uchovu. Katika hali hiyo mabadiliko mawili makubwa yalitokea: Marekani ilijiunga na vita dhidi ya Wajerumani na Urusi ilikuwa na mapinduzi yaliyolazimisha serikali mpya kutia sahihi mapatano ya kumaliza vita dhidi ya Ujerumani iliyoteka maeneo makubwa ya Urusi.
Nguvu ya Marekani ilionekana haraka na bahati ya Ujerumani ilipungua sana. Austria-Hungaria ilidhoofishwa vilevile.
Mwaka 1918 iliona mwisho wa vita. Jeshi la Kiosmani lilishindwa hadi serikali ya milki kuomba kusimamishwa kwa vita. Mataifa ya ushirikiano yalikaribia mipaka ya Ujerumani na hapo mgomo wa wanamaji ilifuatwa na migomo ya wafanyakazi katika viwanda vikubwa iliyosababisha mapinduzi yaliyoangusha serikali ya Kaisari Wilhelm II. Migomo ya wanajeshi ililazimisha Austria-Hungaria kuomba kusimamisha vita.
Milki za Austria na Uturuki zilikwisha zikagawiwa na sehemu zao zilikuwa nchi mpya au nchi zilizoundwa upya.
Mkutano wa Paris
Mwaka 1919 mataifa washindi walikutana Paris (Ufaransa) wakikubaliana masharti ya kumaliza hali ya vita dhidi ya Mataifa ya Kati. Mikataba mbalimbali iliandaliwa kati ya washindi na kuwekwa mbele ya nchi zilizoshindwa.
Mkutano wa Paris ulitoa masharti makali dhidi ya Ujerumani katika Mkataba wa Versailles. Ujerumani uliondolowa makoloni yote yaliyokabidhiwa kwa niaba ya Shirikisho la Mataifa kama maeneo ya kukabidhiwa kwa Uingereza, Ufaransa, Ubelgiji, Japani, Afrika Kusini na Australia.
Mkutano wa Paris ulikuwa jaribio la kuunda utaratibu mpya duniani uliotakiwa kulindwa na Shirikisho la Mataifa. Lakini ukosefu wa nguvu kwa upande wa Shirikisho la Mataifa pamoja na kuanza na kupanuka kwa mwendo mpya wa Kifashisti iliyochukua utawala katika Italia na Ujerumani vilishinda nia hiyo.
Ni kwamba Wajerumani na wakazi wa nchi nyingine zilizoshindwa walijiona wamekosewa haki, lakini pia Waitalia walioshinda kwa gharama kubwa ya damu walijiona wamedanganywa kwa kutotimiziwa ahadi walizopewa ili wasaliti Ujerumani na Austria-Hungaria na kuingia vitani upande wa pili. Hivyo vyama vya mrengo wa kulia viliweza kupata nguvu na hatimaye kupanga kisasi.
Vita ya kwanza ya Dunia?
Vita hii ilitwa "Vita ya Dunia" kwa sababu mapigano yalisambaa kote duniani. Sehemu kubwa ya mapigano yalitokea Ulaya na Asia ya Magharibi lakini pia katika makoloni ya Afrika, Asia na Pasifiki. Nchi za Amerika hazikuona mapigano kwenye nchi kavu lakini manowari za Ujerumani zilipigana na mataifa ya ushirikiano mbele ya pwani za Marekani na Amerika Kusini.
Ilikuwa pia vita ya kwanza iliyopigwa kote duniani ilhali habari zake ziliweza kufika katika muda wa masaa au siku chache kwa mataifa yote kutokana na upatikanaji wa vyombo vya mawasiliano hasa simu za kimataifa na redio.
Lakini kwa kweli haikuwa vita ya kwanza ya "Dunia" maana vita ya miaka saba (1756-1762) ilipigwa tayari kwenye mabara yote ya Dunia baina ya nchi zenye koloni, hasa Uingereza, Ufaransa na Hispania.
Army Art of World War I, United States Army Center of Military History: Smithsonian Institution, National Museum of American History, 1993, OCLC28608539
Bade, Klaus J; Brown, Allison (tr.) (2003), Migration in European History, The making of Europe, Oxford: Blackwell, ISBN0-631-18939-4, OCLC52695573 (translated from the German)
Baker, Kevin (Juni 2006), "Stabbed in the Back! The past and future of a right-wing myth", Harper's Magazine{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Ball, Alan M (1996), And Now My Soul Is Hardened: Abandoned Children in Soviet Russia, 1918–1930, Berkeley: University of California Press, ISBN978-0-520-20694-6, reviewed in Hegarty, Thomas J (Machi–Juni 1998). "And Now My Soul Is Hardened: Abandoned Children in Soviet Russia, 1918–1930". Canadian Slavonic Papers. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-05-09. Iliwekwa mnamo 2014-07-29. {{cite journal}}: Unknown parameter |= ignored (help); Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link) (via Highbeam.com)
Bass, Gary Jonathan (2002), Stay the Hand of Vengeance: The Politics of War Crimes Tribunals, Princeton, New Jersey: Princeton University Press, ku.424pp, ISBN0-691-09278-8, OCLC248021790
Blair, Dale (2005), No Quarter: Unlawful Killing and Surrender in the Australian War Experience, 1915–1918, Charnwood, Australia: Ginninderra Press, ISBN1-74027-291-9, OCLC62514621
Brands, Henry William (1997), T. R.: The Last Romantic, New York: Basic Books, ISBN0-465-06958-4, OCLC36954615
Brown, Judith M. (1994), Modern India: The Origins of an Asian Democracy, Oxford and New York: Oxford University Press, ISBN0-19-873113-2
Chickering, Rodger (2004), Imperial Germany and the Great War, 1914–1918, Cambridge: Cambridge University Press, ISBN0-521-83908-4, OCLC55523473
Cockfield, Jamie H (1997), With snow on their boots: The tragic odyssey of the Russian Expeditionary Force in France during World War 1, Palgrave Macmillan, ISBN0-312-22082-0
Conlon, Joseph M, The historical impact of epidemic typhus(PDF), Montana State University, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo(PDF) mnamo 2010-06-11, iliwekwa mnamo 21 Aprili 2009{{citation}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Cook, Tim (2006), "The politics of surrender: Canadian soldiers and the killing of prisoners in the First World War", The Journal of Military History, 70 (3): 637–665, doi:10.1353/jmh.2006.0158
Cross, Wilbur L (1991), Zeppelins of World War I, New York: Paragon Press, ISBN978-1-55778-382-0, OCLC22860189
Djokić, Dejan (2003), Yugoslavism: histories of a failed idea, 1918–1992, London: Hurst, OCLC51093251
Duffy, Michael, Somme, First World War.com, ISBN0-297-84689-2, iliwekwa mnamo 25 Februari 2007{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Dupuy, R. Ernest and Trevor N. (1993), The Harper's Encyclopedia of Military History, 4th Edition, Harper Collins Publishers, ISBN978-0-06-270056-8
Encyclopaedia Britannica (12th ed. 1922) comprises the 11th edition plus three new volumes 30-31-32 that cover events since 1911 with very thorough coverage of the war as well as every country and colony. partly online and list of article titles
Fromkin, David (2001), A Peace to End All Peace: The Fall of the Ottoman Empire and the Creation of the Modern Middle East, New York: Owl Books, uk.119, ISBN0-8050-6884-8, OCLC53814831
Fromkin, David (2004), Europe's Last Summer: Who Started the Great War in 1914?, New York: Alfred A. Knopf, ISBN0-375-41156-9, OCLC53937943
Gelvin, James L (2005), The Israel-Palestine Conflict: One Hundred Years of War, Cambridge: Cambridge University Press, ISBN0-521-85289-7, OCLC59879560
Grant, R.G. (2005), Battle: A Visual Journey Through 5,000 Years of Combat, DK Publishing, ISBN978-0-7566-5578-5
Gray, Randal; Argyle, Christopher (1990), Chronicle of the First World War, New York: Facts on File, ISBN978-0-8160-2595-4, OCLC19398100
Gilbert, Martin (1994), First World War, Stoddart Publishing, ISBN978-0-7737-2848-6
Gilbert, Martin (2004), The First World War: A Complete History, Clearwater, Florida: Owl Books, uk.306, ISBN0-8050-7617-4, OCLC34792651
Goodspeed, Donald James (1985), The German Wars 1914–1945, New York: Random House; Bonanza, ISBN978-0-517-46790-9
Gray, Randal (1991), Kaiserschlacht 1918: the final German offensive, Osprey, ISBN978-1-85532-157-1
Green, John Frederick Norman (1938), "Obituary: Albert Ernest Kitson", Geological Society Quarterly Journal, 94, Geological Society
Halpern, Paul G (1995), A Naval History of World War I, New York: Routledge, ISBN1-85728-498-4, OCLC60281302
Harris, J. P. (2008), Douglas Haig and the First World War (tol.la2009), Cambridge: CUP, ISBN978-0-521-89802-7
Hartcup, Guy (1988), The War of Invention; Scientific Developments, 1914–18, Brassey's Defence Publishers, ISBN0-08-033591-8
Havighurst, Alfred F (1985), Britain in transition: the twentieth century (tol.la4), University of Chicago Press, ISBN978-0-226-31971-1
Heyman, Neil M (1997), World War I, Guides to historic events of the twentieth century, Westport, Connecticut: Greenwood Press, ISBN0-313-29880-7, OCLC36292837
Hickey, Michael (2003), The Mediterranean Front 1914–1923, The First World War, juz.la4, New York: Routledge, ku.60–65, ISBN0-415-96844-5, OCLC52375688
Hinterhoff, Eugene (1984), Young, Peter (mhr.), "The Campaign in Armenia", Marshall Cavendish Illustrated Encyclopedia of World War I, juz.laii, New York: Marshall Cavendish, ISBN0-86307-181-3
Hooker, Richard (1996), The Ottomans, Washington State University, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1999-10-08, iliwekwa mnamo 30 Desemba 2008{{citation}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Horne, John; Kramer, Alan (2001), German Atrocities, 1914: A History of Denial, Yale University Press, OCLC47181922
Hovannisian, Richard G. (1967), Armenia on the Road to Independence, 1918, Berkeley: University of California Press, ISBN0-520-00574-0
Hull, Isabel Virginia (2006), Absolute destruction: military culture and the practices of war in Imperial Germany, Cornell University Press, ISBN978-0-8014-7293-0
Humphries, Mark Osborne (2007), Hayes, Geoffrey; Iarocci, Andrew; Bechthold, Mike (whr.), Vimy Ridge: A Canadian Reassessment, Waterloo: Wilfrid Laurier University Press, ku.65–85, ISBN0-88920-508-6
Isaac, Jad; Hosh, Leonardo (7–9 Mei 1992), Roots of the Water Conflict in the Middle East, University of Waterloo, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-09-28, iliwekwa mnamo 2014-07-29{{citation}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: location missing publisher (link)
Jenkins, Burris A (2009), Facing the Hindenburg Line, BiblioBazaar, ISBN978-1-110-81238-7
Johnson, James Edgar (2001), Full Circle: The Story of Air Fighting, London: Cassell, ISBN0-304-35860-6, OCLC45991828
Jones, Howard (2001), Crucible of Power: A History of US Foreign Relations Since 1897, Wilmington, Delaware: Scholarly Resources Books, ISBN0-8420-2918-4, OCLC46640675
Kaplan, Robert D (Februari 1993), "Syria: Identity Crisis", The Atlantic, iliwekwa mnamo 30 Desemba 2008{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Karp, Walter (1979), The Politics of War (tol.la1st), ISBN0-06-012265-X, OCLC4593327, Wilson's maneuvering US into war
Keegan, John (1998), The First World War, Hutchinson, ISBN0-09-180178-8, general military history
Keene, Jennifer D (2006), World War I, Daily Life Through History Series, Westport, Connecticut: Greenwood Press, uk.5, ISBN0-313-33181-2, OCLC70883191
Kernek, Sterling (Desemba 1970), "The British Government's Reactions to President Wilson's 'Peace' Note of December 1916", The Historical Journal, 13 (4): 721–766, doi:10.1017/S0018246X00009481, JSTOR2637713{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Kitchen, Martin (2000) [1980], Europe Between the Wars, New York: Longman, ISBN0-582-41869-0, OCLC247285240
Lehmann, Hartmut; van der Veer, Peter, whr. (1999), Nation and religion: perspectives on Europe and Asia, Princeton, New Jersey: Princeton University Press, ISBN0-691-01232-6, OCLC39727826
Lewy, Guenter (2005), The Armenian Massacres in Ottoman Turkey: A Disputed Genocide, Salt Lake City, Utah: University of Utah Press, ISBN0-87480-849-9, OCLC61262401
Lyons, Michael J (1999), World War I: A Short History (tol.la2nd), Prentice Hall, ISBN0-13-020551-6
Ludendorff, Erich (1919), My War Memories, 1914–1918, OCLC60104290 also published by Harper as "Ludendorff's Own Story, August 1914– November 1918: The Great War from the Siege of Liège to the Signing of the Armistice as Viewed from the Grand Headquarters of the German Army" OCLC 561160 (original title Meine Kriegserinnerungen, 1914–1918)
Magliveras, Konstantinos D (1999), Exclusion from Participation in International Organisations: The Law and Practice behind Member States' Expulsion and Suspension of Membership, Martinus Nijhoff Publishers, ISBN90-411-1239-1
Martel, Gordon (2003), The Origins of the First World War, Pearson Longman, Harlow
Mawdsley, Evan (2008), The Russian Civil War (tol.laEdinburgh), Birlinn location, ISBN1-84341-041-9{{citation}}: Invalid |ref=harv (help)
Meyer, Gerald J (2006), A World Undone: The Story of the Great War 1914 to 1918, Random House, ISBN978-0-553-80354-9
Millett, Allan Reed; Murray, Williamson (1988), Military Effectiveness, Boston: Allen Unwin, ISBN0-04-445053-2, OCLC220072268
Moon, John Ellis van Courtland (Julai 1996), "United States Chemical Warfare Policy in World War II: A Captive of Coalition Policy?", The Journal of Military History, 60 (3), Society for Military History: 495–511, doi:10.2307/2944522, JSTOR2944522{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Morton, Desmond (1992), Silent Battle: Canadian Prisoners of War in Germany, 1914–1919, Toronto: Lester Publishing, ISBN1-895555-17-5, OCLC29565680
Mosier, John (2001), "Germany and the Development of Combined Arms Tactics", Myth of the Great War: How the Germans Won the Battles and How the Americans Saved the Allies, New York: Harper Collins, ISBN0-06-019676-9
Northedge, FS (1986), The League of Nations: Its Life and Times, 1920–1946, New York: Holmes & Meier, ISBN0-7185-1316-9
Page, Thomas Nelson, Italy and the World War, Brigham Young University, Chapter XI cites "Cf. articles signed XXX in La Revue de Deux Mondes, 1 and 15 March 1920"
Phillimore, George Grenville; Bellot, Hugh HL (1919), "Treatment of Prisoners of War", Transactions of the Grotius Society, 5: 47–64, OCLC43267276
Pitt, Barrie (2003), 1918: The Last Act, Barnsley: Pen and Sword, ISBN0-85052-974-3, OCLC56468232
Price, Alfred (1980), Aircraft versus Submarine: the Evolution of the Anti-submarine Aircraft, 1912 to 1980, London: Jane's Publishing, ISBN0-7106-0008-9, OCLC10324173 Deals with technical developments, including the first dipping hydrophones
Prior, Robin (1999), The First World War, London: Cassell, ISBN0-304-35256-X
Raudzens, George (Oktoba 1990), "War-Winning Weapons: The Measurement of Technological Determinism in Military History", The Journal of Military History, 54 (4), Society for Military History: 403–434, doi:10.2307/1986064, JSTOR1986064{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Rickard, J (27 Agosti 2007), The Ludendorff Offensives, 21 March-18 July 1918, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-10-10, iliwekwa mnamo 2021-10-02{{citation}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Roden, Mike, "The Lost Generation– myth and reality", Aftermath– when the boys came home, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-12-01, iliwekwa mnamo 6 Novemba 2009{{citation}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Saadi, Abdul-Ilah, Dreaming of Greater Syria, Al Jazeera, iliwekwa mnamo 17 Novemba 2009{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Sachar, Howard Morley (1970), The emergence of the Middle East, 1914–1924, Allen Lane, ISBN0-7139-0158-6, OCLC153103197
Schindler, J (2003), "Steamrollered in Galicia: The Austro-Hungarian Army and the Brusilov Offensive, 1916", War in History, 10 (1): 27–59, doi:10.1191/0968344503wh260oa
Shanafelt, Gary W (1985), The secret enemy: Austria-Hungary and the German alliance, 1914–1918, East European Monographs, ISBN978-0-88033-080-0
Shapiro, Fred R; Epstein, Joseph (2006), The Yale Book of Quotations, Yale University Press, ISBN0-300-10798-6
Souter, Gavin (2000), Lion & Kangaroo: the initiation of Australia, Melbourne: Text Publishing, OCLC222801639
Sisemore, James D (2003), The Russo-Japanese War, Lessons Not Learned, US Army Command and General Staff College, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-03-04, iliwekwa mnamo 2021-01-17{{citation}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
Smele, Jonathan, "War and Revolution in Russia 1914–1921", World Wars in-depth, BBC, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-11-10, iliwekwa mnamo 12 Novemba 2009{{citation}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Speed, Richard B, III (1990), Prisoners, Diplomats and the Great War: A Study in the Diplomacy of Captivity, New York: Greenwood Press, ISBN0-313-26729-4, OCLC20694547{{citation}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
Stevenson, David (1996), Armaments and the Coming of War: Europe, 1904–1914, New York: Oxford University Press, ISBN0-19-820208-3, OCLC33079190
Stevenson, David (2004), Cataclysm: The First World War as Political Tragedy, New York: Basic Books, ku.560pp, ISBN0-465-08184-3, OCLC54001282
Strachan, Hew (2003), The First World War: Volume I: To Arms, New York: Viking, ISBN0-670-03295-6, OCLC53075929
Taylor, Alan John Percivale (1963), The First World War: An Illustrated History, Hamish Hamilton, ISBN0-399-50260-2, OCLC2054370
Taylor, Alan John Percivale (1998), The First World War and its aftermath, 1914–1919, Century of Conflict, 1848–1948, London: Folio Society, OCLC49988231
Taylor, John M (Summer 2007), "Audacious Cruise of the Emden", The Quarterly Journal of Military History, 19 (4): 38–47, doi:10.1353/jmh.2007.0331, ISSN0899-3718{{citation}}: Unknown parameter |doi_brokendate= ignored (|doi-broken-date= suggested) (help)CS1 maint: date and year (link) CS1 maint: date auto-translated (link)
Terraine, John (1963), Ordeal of Victory, Philadelphia: J. B. Lippincott, ku.508pp, ISBN0-09-068120-7, OCLC1345833
Tschanz, David W, Typhus fever on the Eastern front in World War I, Montana State University, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-06-11, iliwekwa mnamo 12 Novemba 2009{{citation}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Tuchman, Barbara Wertheim (1966), Zimmermann Telegram (tol.la2nd), New York: Macmillan, ISBN0-02-620320-0, OCLC233392415
Tucker, Spencer C; Roberts, Priscilla Mary (2005), Encyclopedia of World War I, Santa Barbara: ABC-Clio, ISBN1-85109-420-2, OCLC61247250
Tucker, Spencer C; Wood, Laura Matysek; Murphy, Justin D (1999), The European powers in the First World War: an encyclopedia, Taylor & Francis, ISBN978-0-8153-3351-7
von der Porten, Edward P (1969), German Navy in World War II, New York: T. Y. Crowell, ISBN0-213-17961-X, OCLC164543865
Westwell, Ian (2004), World War I Day by Day, St. Paul, Minnesota: MBI Publishing, ku.192pp, ISBN0-7603-1937-5, OCLC57533366
Wilgus, William John (1931), Transporting the A. E. F. in Western Europe, 1917–1919, New York: Columbia University Press, OCLC1161730
Willmott, H.P. (2003), World War I, New York: Dorling Kindersley, ISBN0-7894-9627-5, OCLC52541937
Winter, Denis (1983), The First of the Few: Fighter Pilots of the First World War, Penguin, ISBN978-0-14-005256-5
Wohl, Robert (1979), The Generation of 1914 (tol.la3), Harvard University Press, ISBN978-0-674-34466-2
Zieger, Robert H (2001), America's Great War: World War I and the American experience, Lanham, Maryland: Rowman & Littlefield, uk.50, ISBN0-8476-9645-6
"History in brief (Israel)", The Economist, 28 Julai 2005, iliwekwa mnamo 30 Desemba 2008{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Israeli Foreign Ministry, Ottoman Rule, Jewish Virtual Library, iliwekwa mnamo 30 Desemba 2008{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link)