Schutztruppe
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Schutztruppe (tamka shuts-tru-pe; Kijerumani kwa "Jeshi la Ulinzi") ilikuwa jina la jeshi la kikoloni la Ujerumani hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.
Ilifanywa na askari Waafrika chini ya amri wa maafisa Wajerumani. Ilianzishwa katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (hasa Tanganyika ya baadaye) ikaendelea kupanuliwa pia katika makoloni ya Afrika ya Kusini-Magharibi ya Kijerumani (Namibia ya leo) na Kamerun.
Katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani jeshi hilo lilikuwa na vikosi 14 vyenye askari 2,500 kwa jumla. Chini ya mkuu Paul von Lettow-Vorbeck Schutztruppe ilipiga Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ikaweza kuendelea hadi mwisho wa vita na kusalimu amri siku chache baada ya mwisho wa vita.
Chanzo cha jeshi hili kilikuwa kikosi kilichoajiriwa na Hermann von Wissmann mwaka 1889 kwa niaba ya Dola la Ujerumani kwa kusudi la kukomesha vita ya Abushiri kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki. Hapa wakazi wa pwani ya Tanzania ya leo walipinga majaribio ya Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki ya kushika utawala juu ya pwani. Wissmann aliajiri maafisa 21 na maafande 40 kutoka Ujerumani akaelekea Afrika. Njiani alipita Misri akawaajiri askari Wasudan 600 kutoka jeshi la Misri (walioachishwa kazi wakati ule kutokana na kupungukiwa kwa jeshi la Misri baada ya vita ya Mahdi). Wakati huohuo alimtuma afisa moja, luteni Hans von Ramsay, kwenda Hori ya Inhambane, Msumbiji alipoajiri askari 150 Wazulu kama nyongeza[1]. Jeshi hili lilijulikana kama "Wissmanntruppe" (kikosi cha Wissmann). Kwa kutumia silaha za kisasa kama bombomu walifaulu kushinda upinzani dhidi ya utawala wa Kijerumani.
Mwaka 1891 kikosi hiki kiliajiriwa na serikali yenyewe na kwa sheria maalumu kuwa sehemu ya jeshi la Ujerumani, ikipangwa mwanzoni iwe chini ya usimamizi wa jeshi la majini na kuitwa "Schutztruppe für Ostafrika" yaani jeshi la ulinzi kwa Afrika ya Mashariki.
Katika miaka iliyofuata vikosi vilivyoitwa "Schutztruppe" viliundwa pia katika koloni za Afrika ya Kusini-Magharibi ya Kijerumani (Namibia) na Kamerun. Mwaka 1896 vikosi hivyo katika koloni viliunganishwa kama mkono wa pekee wa jeshi la Ujerumani chini ya amri kuu ya Kaisari mwenyewe; Schutztruppe ndani ya kila koloni ilikuwa chini ya mamlaka ya gavana wa koloni.
Askari wa vikosi katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani na Kamerun walikuwa Waafrika walioajiriwa, wakitekeleza shughuli chini ya maafisa na maafande Wajerumani; kulikuwa pia na maafisa na maafande wachache Waafrika wenye cheo cha "efendi"[2]. Katika Afrika ya Kusini-Magharibi hapakuwa na askari Waafrika, hata askari wa kawaida walikuwa Wajerumani.
Mnamo mwaka 1913 jeshi la Schutztruppe lilikuwa na maafisa 69 Wajerumani, maafisa waganga Wajerumani 42, wafanyakazi Wajerumani wa ofisini 12, maafande wa kijeshi Wajerumani 60, maafande wa kiganga 66 na askari Waafrika 2,472.
Hao waligawiwa katika vikosi 14 pamoja na ofisi kuu ya utawala Dar es Salaam na kituo cha kufunza askari wapya.
Kila kikosi kilikuwa na askari 160-200, waliopangwa kwa platuni 3 za askari 50-60. Kila platuni ilikuwa na vikundi 2 vya bombomu. Kila kikosi kilikuwa pia na kundi la wapagaji takriban 250.
Vikosi hivi vilipangwa mahali pafuatapo:
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.