Japani
nchi ya visiwani katika Asia Mashariki From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Japani, ni nchi ya visiwa katika Asia ya Mashariki, iliyoko kwenye Bahari ya Pasifiki. Inapakana kwa maji na China, Korea Kusini, Korea Kaskazini, na Urusi. Ina idadi ya watu takriban milioni 123, ikiwa ya 11 duniani. Jiji lake kubwa zaidi na mji mkuu ni Tokyo, moja ya miji yenye watu wengi zaidi duniani. Japani imegawanyika katika mikoa 47, Inajulikana kwa teknolojia yake ya hali ya juu, utamaduni wake wa kale na wa kisasa kama anime na samurai, pamoja na miundombinu ya kisasa kama treni za mwendo kasi (Shinkansen).
Japani ni mojawapo ya nchi zilizoendelea zaidi kiuchumi duniani, ikiwa na mojawapo ya pato la taifa kubwa zaidi kwa viwango vya kimataifa. Uchumi wake unaegemea hasa katika viwanda vya teknolojia ya hali ya juu, magari, vifaa vya kielektroniki, na roboti. Makampuni makubwa kama Toyota, Sony, na Panasonic yanatoka Japani na yana ushawishi mkubwa duniani. Licha ya rasilimali chache za asili, Japani imefanikiwa kukuza uchumi wake kupitia ubunifu, elimu ya juu, na nidhamu ya kazi miongoni mwa wananchi wake.
Katika historia, Japani iliwahi kuwa milki ya kifalme iliyojitenga na mataifa ya nje kwa karne nyingi, hadi ilipofunguka kwa dunia wakati wa kipindi cha Meiji mnamo karne ya 19. Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, ambapo ilishambuliwa vikali ikiwemo mabomu ya atomiki mjini Hiroshima na Nagasaki, Japani ilijengwa upya na kuwa taifa la kidemokrasia. Leo, ni mwanachama wa mashirika makubwa kama Umoja wa Mataifa, G7, na G20, na ina ushawishi mkubwa katika siasa, uchumi, na utamaduni wa kimataifa.
Remove ads
Jiografia
Japani ni funguvisiwa lenye visiwa 14,125 mbele ya pwani ya Uchina, Korea na Urusi (Siberia).
Visiwa vikubwa na muhimu zaidi ni vinne tu; ndivyo Honshu, Hokkaido, Shikoku na Kyushu. Safu ya milima inapita visiwa vyote vikubwa na kusababisha msongamano mkubwa wa wakazi katika miji kutokana na uhaba wa ardhi ya kukalia. Hali halisi Japani yote ni safu ya milima tu inayopanda juu kutoka sakafu ya bahari na vilele vya milima yake huonekana juu ya uso wa bahari kama visiwa vikubwa au vidogo.
Kijiolojia eneo hili liko kwenye mstari ambako mabamba ya gandunia ya Ulaya-Asia, Pasifiki na Ufilipino hukutana. Hii ni sababu ya kuwepo kwa volkeno 240 katika Japani na takriban 40 kati ya hizo ni hai pia kutokea kwa matetemeko ya ardhi ya mara kwa mara. Hivyo Japani ni sehemu ya pete ya moto ya Pasifiki inayozunguka bamba la Pasifiki.
Japani inapatwa kila mwaka na dhoruba kali aina ya taifuni. Hata tsunami (ni neno la Kijapani) ni kawaida. Nchi inajikinga na mitambo mengi ya kutoa taarifa ya tsunami kuanza pia mitambo ya kufunga milango ya mabandari.

Miji
Wajapani wengi hukalia sehemu ndogo ya 10% za nchi. Kuna miji kumi yenye wakazi zaidi ya milioni moja. Miji mikubwa ni Tokyo, Yokohama, Nagoya, Osaka, Kyoto, Kobe, Hiroshima, Fukuoka, Kitakyushu, Sendai na Sapporo. Usafiri ndani ya Japani ni hasa kwa treni, mabasi na ndege. Treni ya Shinkansen visiwani Honshu na Kyushu ni kati ya treni zenye mkasi mkubwa duniani.
Mikoa

Japan ina mikoa arubaini na saba. Kila mkoa unasimamiwa na gavana mmoja, bunge na urasimu utawala. Kila mkoa umegawanyika katika miji na vijiji.
1. Hokkaidō |
2. Aomori |
8. Ibaraki |
15. Niigata |
Kansai
24. Mie |
31. Tottori |
|
Kyūshū and Okinawa
40. Fukuoka |
Kwa sasa manispaa za Japani zinaundwa upya kwa kuunganisha mikoa, miji na baadhi ya vijiji. Mabadiliko hayo yatapunguza idadi ya miji nchini Japani.[1]
Historia
Visiwa vilikaliwa na binadamu tangu miaka 30,000 KK.
Wakazi wa sasa wametokana na mchanganyiko wa makabila asili (kama Waainu) na Wakorea waliovamia visiwa hivyo.
Uchumi
Dini
Wajapani wanaweza kushiriki ibada za dini mbalimbali kadiri wanavyojisikia, lakini asilimia 60 hawana dini maalumu. Wabuddha ni asilimia 34, wafuasi wa madhehebu ya Shinto ni asilimia 4, Wakristo sanasana ni asilimia 2.3.
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads