From Wikipedia, the free encyclopedia
Mtume Mathia (kwa Kigiriki Matthias kutokana na Mattathias, kwa Kiebrania Mattithiah, maana yake "Zawadi ya Mungu") kadiri ya Matendo ya Mitume 1:21-22 alikuwa mfuasi wa Yesu Kristo tangu alipobatizwa na Yohane Mbatizaji hadi alipopaa mbinguni mwaka 30 (au 33).
Mitume wa Yesu |
---|
|
Kabla ya Pentekoste wa mwaka huo, Mtume Petro alipendekeza kwamba mmoja kati ya wafuasi wa kwanza wa Yesu ashike nafasi ya marehemu mtume Yuda Iskarioti, na kura ya bahati ilimuangukia Mathia awe shahidi wa ufufuko wake.
Ingawa Biblia haina habari zaidi juu yake, inasemekana alifia dini na tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu, hasa tarehe 14 Mei (Kanisa Katoliki[1] na Anglikana), tarehe 9 Agosti (Waorthodoksi wa Mashariki) na tarehe 24 Februari (Walutheri na wengineo).
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.