Mtume Simoni Mkananayo

mtume wa Yesu From Wikipedia, the free encyclopedia

Mtume Simoni Mkananayo

Simoni Mkananayo (alifariki karne ya 1) alikuwa mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu.

Mt. Simoni alivyochorwa na Peter Paul Rubens (1611 hivi), katika mfululizo wake juu ya Thenashara uliopo Museo del Prado, Madrid.
Sanamu iliyoko Bruges inayomuonyesha akiwa na msumeno, chombo ambacho inasemekana kilitumika kumuulia.

Ili kumtofautisha na mtume mwenzake Simoni Petro anaitwa Mkananayo, yaani Mwenye juhudi kwa ukombozi wa Israeli kutoka ukoloni wa Roma.

Jina lake linapatikana katika orodha zote za Mitume, lakini hatuna habari zake zaidi, isipokuwa masimulizi mbalimbali yasiyo na hakika[1].

Inasadikika kuwa kaburi lake liko Komani (Georgia).

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 28 Oktoba pamoja na Yuda Tadei[2][3].

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.