Mtume Mathayo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mathayo (kwa Kiebrania מַתִּתְיָהוּ, Mattityahu au מתי, Mattay, Zawadi ya Mungu; kwa Kigiriki Ματθαῖος, Matthaios. Labda aliitwa pia Lawi) alikuwa Myahudi wa karne ya 1, mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu anayeheshimiwa hasa kutokana na Injili yenye jina lake ambayo inataka kuthibitisha kwamba Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Abrahamu, ametimiza ahadi za Agano la Kale [1].

Mitume wa Yesu |
---|
|
Maisha
Kabla hajaitwa na Yesu Kristo amfuate, Mathayo alikuwa mtozaushuru, na kwa sababu hiyo alitazamwa na Wayahudi kama msaliti wa taifa na mkosefu.
Hata hivyo Yesu alipomkuta forodhani alimuambia, "Nifuate" (Injili ya Marko 2:14). Ndipo Mathayo akaacha vyote akaanza kuwa mwanafunzi wake. Katika nafasi hiyo alimuandalia karamu kubwa waliyoishiriki watozaushuru wengi, hata kusababisha lawama kwa Yesu toka kwa Mafarisayo.
Inasemekana kwamba baada ya ufufuko wa Yesu, Mathayo alieneza habari njema Ethiopia, ingawa masalia yake yanaheshimiwa huko Salerno (Italia) tangu mwaka 954.
Maandishi
Kuna ushahidi wa zamani kwamba aliwahi kuandika misemo ya Yesu kwa lugha ya Kiaramu. Kitabu hicho kilipotea mapema, na ni vigumu kusema kina uhusiano gani na Injili ya Mathayo iliyoandikwa moja kwa moja kwa Kigiriki fasaha.
Heshima baada ya kifo
Wakristo wa madhehebu yote wanamheshimu kama mtakatifu, hasa tarehe 21 Septemba[2] na 16 Novemba.
Anaheshimiwa kama msimamizi wa watu wa benki, forodha, wahasibu n.k.
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.