Lugha ya Kiebrania (עברית ‘Ivrit, matamshi ya kisasa ?) ni moja ya lugha za kisemiti na moja kati ya lugha mbili za kitaifa nchini Israel (pamoja na Kiarabu). Ni kati ya lugha za kale zaidi duniani.
Kiebrania kwa kawaida huandikwa kwa herufi za Kiebrania. Mwandiko huu ni wa konsonanti hasa, kwa kuwa mara nyingi vokali haziandikwi kutokana mfumo wa lugha yenyewe.
Kiebrania ni lugha iliyotumika kuandikia Torati na sehemu kubwa ya maandiko mengine ya Biblia ya Kiebrania. Sehemu hiyo ya Kiebrania pamoja na sehemu ndogo ya Kiaramu huitwa "Tanakh" katika mapokeo ya Kiyahudi na imo katika Agano la Kale ya Biblia ya Kikristo.
Lugha za Kisemiti
Lugha ya Kiebrania pamoja na zile za Kiarabu, Kiaramu na Kiamhari (Ethiopia) zinatokana na asili moja ya lugha ya Kisemiti. Kuna lugha nyingi ambazo zinatokana na asili hiyohiyo kama Kiashuru, Kifoinike, Kikaldayo na kadhalika.
Mwandiko wa Kiebrania
Makala Kuu: Mwandiko wa Kiebrania
Mwandiko wa lugha hiyo hufanywa kwa mwandiko wa pekee unaojulikana tangu miaka 3,000. Mwandiko huu ni wa konsonanti hasa, kwa kuwa mara nyingi vokali haziandikwi. Tabia hii ni sawa na alfabeti nyingine za Kisemiti kama Kiaramu au Kiarabu.
Mfano: Jina la Abrahamu huandikwa "אַבְרָהָ֛ם" ambazo ni herufi "aBRHM" pekee; Alef ambayo ni herufi la kwanza tena si "a" kwa hakika. Vokali zinaweza kuonyeshwa kwa nukta na mistari chini ya herufi lakini mara nyingi haziandikwi.
Alef | Bet/Vet | Gimel | Dalet | He | Waw | Zayin | Khet | Tet | Yod | Kaf/Khaf |
א | ב | ג | ד | ה | ו | ז | ח | ט | י | כ |
ך | ||||||||||
Lamed | Mem | Nun | Samekh | Ayin | Pe/Fe | Tsadeh | Qof | Resh | Shin/Sin | Taw |
ל | מ | נ | ס | ע | פ | צ | ק | ר | ש | ת |
ם | ן | ף | ץ |
Historia
Kiebrania kilikuwa lugha ya Israeli ya Kale wakati wa Biblia kuanza kuandikwa. Baada ya Uhamisho wa Babeli Wayahudi walianza kutumia Kiaramu, na polepole Kiebrania hakikuzungumzwa tena, lakini kilifundishwa kama lugha ya kidini. Wayahudi wa kawaida walikitumia katika ibada na wataalamu waliandika vitabu kwa lugha hiyo.
Katika karne ya 20 Wayahudi wa Ulaya waliamua kukifufua kama lugha hai. Kimekuwa lugha ya nchi mpya ya Israel tangu 1948. Watu waliohamia Israel kutoka mahali pengi duniani walijifunza Kiebrania na watoto wao wameishika kama lugha yao ya kawaida.
Viungo vya nje
- Ghil'ad Zuckermann (2003), Language Contact and Lexical Enrichment in Israeli Hebrew. Palgrave Macmillan. ISBN 978-1403917232 .
- makala za OLAC kuhusu Kiebrania Archived 17 Mei 2015 at the Wayback Machine.
- lugha ya Kiebrania katika Glottolog
- Muhtasari kuhusu Kiebrania kwenye Ethnologue
- Modern Hebrew resources
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kiebrania kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Wikiwand in your browser!
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.