Thoma (au Didimo, yaani Pacha) alikuwa Myahudi wa karne ya 1, mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu anayeheshimiwa kama mtakatifu, kwa namna ya pekee na Wakristo wa maeneo yaliyokuwa mashariki kwa Dola la Roma, kuanzia Iraq hadi India.

Kifodini cha Mtume Thomas kilivyochorwa na Peter Paul Rubens.

Inawezekana kwamba sababu yake ni kazi za utume alizozifanya huko hadi kifodini chake huko Chennai mwaka 72 (kaburi lake huonyeshwa katika mji huo wa Tamil Nadu). Mpaka leo kusini-magharibi mwa Bara Hindi wako wanaojiita "Wakristo wa Thoma" ambao kwa muda mrefu walikosa mawasiliano na Wakristo wengine wa mbali.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na madhehebu mengine mbalimbali kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe 3 Julai[1].

Chanzo cha umaarufu wake

Alikuwa mtu mwenye tabia ya pekee iliyomvutia umaarufu hadi leo. Hasa alielekea kukata tamaa, kupinga hoja na kutosadiki kwa urahisi, kama alipokataa kusadiki ushahidi wa mitume wenzake juu ya ufufuko wa Yesu[2].

Mfano mmojawapo ni pale ambapo katika karamu ya mwisho alimjibu Yesu kwa wasiwasi: "Bwana, hatujui uendako; tutajuaje basi njia?" (Yoh 14:5). Ndipo Yesu alipojitambulisha kama njia: "Mimi ndimi njia, ukweli na uzima" (Yoh 14:6).

Hata hivyo, Injili ya Yohane ambayo ndiyo inayomzungumzia zaidi katika Biblia ya Kikristo, inaripoti jibu lake la mwisho kwa Yesu mfufuka kama ifuatavyo (Yoh 20:28): "Bwana wangu na Mungu wangu!" Katika Injili hakuna ungamo la wazi zaidi la umungu wa Yesu Kristo.

Hata hivyo, Yesu alimuambia wana heri zaidi wanaosadiki bila kuona kwanza. Na ndilo lengo la Yohane katika kuandika Injili yake: kuwafanya wasomaji wasioweza tena kumuona Yesu wamuamini na hivyo kupata uzima wa milele.

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.