From Wikipedia, the free encyclopedia
Shirikisho la Mikronesia ni nchi ya visiwani katika Bahari Pasifiki iliyoko kaskazini kwa Papua Guinea Mpya.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: | |||||
Wimbo wa taifa: Patriots of Micronesia | |||||
Mji mkuu | Palikir | ||||
Mji mkubwa nchini | Weno | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza (kitaifa), Kiulithi, Kiwoleai, Kiyap, Kipohnpei, Kikosrae na Kichuuk (kijimbo) | ||||
Serikali | Jamhuri David W. Panuelo | ||||
Uhuru Tarehe |
3 Novemba 1986 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
702 km² (ya 177) | ||||
Idadi ya watu - Julai 2019 kadirio - 2000 sensa - Msongamano wa watu |
104,468 (ya 198) 107,000 158.1/km² (ya 75) | ||||
Fedha | US Dollar (USD ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC+10) (UTC-) | ||||
Intaneti TLD | .fm | ||||
Kodi ya simu | +691
- |
Ni nchi huru inayoshirikiana na Marekani. Nchi ilikuwa eneo lindwa chini ya Marekani kwa niaba ya Umoja wa Mataifa hadi ikapata uhuru wake mwaka 1986.
Shirikisho linajumlisha sehemu kubwa ya funguvisiwa la Karolini katika Mikronesia, kanda la Pasifiki. Jumla ya visiwa ni 607.
Nchi ina majimbo manne ya kujitawala ambayo ni Chuuk, Kosrae, Pohnpei na Yap.
Visiwa vya Palau pia ni sehemu ya Karolini lakini ni nchi ya pekee.
Mji mkubwa wa nchi ni Weno (wakazi 17,624) kisiwani Chuuk lakini mji mkuu ni Palikir kwenye kisiwa cha Pohnpei.
Kuna majimbo manne kama yafuatayo:
Visiwa vimekaliwa na watu tangu miaka 4,000 iliyopita, hasa kutoka Rasi ya Malay na visiwa vya Indonesia. Wengine wametokea visiwa vya Polinesia.
Kisiwani Yap kulitokea dola na utawala wa kifalme.
Tangu kufika kwa Wahispania katika karne ya 16 visiwa vilikuwa chini ya ubwana wa nje lakini maisha ya kawaida yaliendelea bila mabadiliko makubwa kwa muda mrefu.
Mwisho wa karne ya 19 Hispania iliuza koloni hilo kwa Ujerumani; utawala wa Kijerumani ulikwisha katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ukachukuliwa na Japani hadi mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
Japani ilifuatwa na Marekani iliyoendelea kutawala kwa niaba ya UM hadi uhuru.
Kuna lugha 18 ambazo huzungumzwa katika Shirikisho la Mikronesia. Lugha rasmi ni Kiingereza.
Wakazi wengi ni wa makabila ya asili.
Upande wa dini, wengi ni Wakristo (95.3%), kwanza Wakatoliki (52.6%) halafu Waprotestanti wa madhehebu mbalimbali (41.7%).
Uchumi wa nchi hutegemea hasa kilimo cha kujisukuma na uvuvi. Mapato ya serikali ni kutokana na vibali kwa wavuvi wa nje wanaovua samaki ndani ya maji ya shirikisho.
Kuna pia uchimbaji wa fosfeti.
Shirikisho la Mikronesia pamoja na Nauru vinaongoza duniani kwa asilimia kubwa ya watu wanene.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.