Remove ads
From Wikipedia, the free encyclopedia
Unene wa kupindukia (kwa Kiingereza "obesity" kutokana na neno la Kilatini obesitas, linalomaanisha "gumu, nono au nene” [1]; jina la kisayansi kwa Kilatini ni "adipositas") ni hali mbaya ambapo mafuta ya ziada ya mwili hulimbikizana hadi kiwango kinachoweza kuathiri vikubwa afya, ikipelekea ongezeko la maradhi na kupungua kwa matarajio ya kuishi. [2][3]
Kipimo cha mwili kuwa mnene na mzito mno ni uwiano kati ya urefu wa mtu na uzito wake. Watu hutajika kuwa na unene wa kupindukia wakati nambapeo ya mata ya mwili (NMM), kipimo kinachopatikana kwa kugawanya uzito wa mtu kwa kilogramu kwa mraba wa urefu wake katika mita, kimezidi 30 kg/m2.[4]
Kuwa mneme mno kunaleta hatari ningi kwa afya na kusababisha au kuongeza uwezekano wa magonjwa kama vile:
Watu wakinenepa mno hufa mapema na kuwa na magonjwa mengi kuliko watu wembamba wanaokula kiasi tu, jinsi wanavyohitaji chakula. Tatizo la unene duniani hukumba wanaume zaidi ya wanawake.
Unene wa kupindukia mara nyingi husababishwa na ujumuisho wa kula chakula kilicho na nguvu nyingi, ukosefu wa mazoezi ya mwili, na urithi wa jeni maalumu, ingawa visa vichache vina msingi wa jeni, matatizo ya kiendrosini, matibabu au maradhi ya akili.
Ushahidi wa kuthibitisha dhana kuwa baadhi ya watu hunenepa ingawa hula kiasi kidogo hautoshi; kwa wastani, watu wanene hutumia nguvu nyingi kuliko watu wenye mwili mdogo kwa sababu ya nguvu zinazohitajika kuimarisha mata kubwa ya mwili.[6][7]
Chakula bora na mazoezi ya mwili ndiyo njia kuu za kutibu unene wa kupindukia. Ubora wa chakula unaweza kuimarishwa kwa kutumia vyakula vilivyo na nguvu nyingi, kama vile vyakula vilivyo na kiwango cha juu cha mafuta na sukari, na kwa kutumia unyuzi wa chakula kwa wingi zaidi.
Dawa za kukabiliana na unene zinaweza kutumiwa kupunguza hamu ya chakula au kuzuia ufyonzaji wa mafuta, huku mtu akila chakula kinachofaa. Iwapo chakula bora, mazoezi na matibabu hayatoshi, mpira wa utumboni unaweza kusaidia kupunguza uzito wa mwili, au upasuaji unaweza kufanywa ili kupunguza ukubwa na/au urefu wa matumbo. Upasuaji huo hupelekea mtu kushiba upesi na kupunguza uwezo wa kufyonza virutubishi vilivyomo katika chakula.[8][9]
Unene wa kupindukia ni kisababishi kinachozuilika cha kifo kilicho kikuu ulimwenguni kote, huku kiwango chake cha ueneaji kikiongezeka kwa watu wazima na watoto. Viongozi huamini kuwa hili ni mojawapo ya matatizo makuu zaidi ya afya ya umma katika karne ya 21.[10]
Unene wa kupindukia hufedheheshwa katika sehemu nyingi za ulimwengu wa kisasa (hasa katika Ustaarabu wa Magharibi[11]), ingawa hali hii ilitazamwa na watu wengi kama ishara ya utajiri na afya bora katika nyakati za awali za historia, na pia huonekana hivyo katika baadhi ya sehemu za dunia.[3][12]
Unene wa kupindukia ni hali ya kimatibabu ambapo mafuta ya mwili ya ziada hulimbikizana hadi kiwango kinachoathiri afya kwa vikubwa.[2] Hali hii hufasiliwa kwa Kielezo cha Uzani wa Mwili na kukadiriwa zaidi kwa kupima ugawaji wa mafuta kupitia kwa uwiano wa kiuno na nyonga na ujumla wa vipengele hatari vya magonjwa ya mishipa na moyo.[13][14]
Kielezo cha Uzani wa Mwili kinahusiana kwa karibu na asilimia ya mafuta ya mwili na jumla ya mafuta ya mwili.[15]
Katika watoto, uzito ulio bora hutofautiana kwa sababu ya umri na jinsia. Katika watoto na vijana baleghe, unene wa kupindukia hufasiliwa si kwa nambari kamili, lakini kulingana na kundi la kawaida la wakati huo, hivi kwamba unene wa kupindukia ni wa Kielezo cha Uzani wa Mwili kilichozidi asilimia 95 [16]Data ya marejeleo ambayo ilitumiwa kukadiria hesabu hii ni ya kutoka mwaka 1963 hadi 1994, hivyo haijaathiriwa na ongezeko la uzito la hivi karibuni.[17]
BMI | Classification |
---|---|
< 18.5 | underweight |
18.5–24.9 | normal weight |
25.0–29.9 | overweight |
30.0–34.9 | class I obesity |
35.0–39.9 | class II obesity |
≥ 40.0 | class III obesity |
Kielezo cha Uzani wa Mwili hukadiriwa kwa kugawanya uzito wa mtu kwa kipeo cha uzito wake, na kwa kawaida huandikwa aidha kwa Mfumo wa mita au kwa vipimo vya Marekani:
ambapo ni uzito wa mtu katika pauni na ni urefu wa mtu katika inchi.
Fasili zinazotumika mara nyingi, ambazo zilitolewa na Shirika la Afya Duniani mwaka wa 1997 na kuchapishwa mwaka wa 2000, hutoa ukadiriaji kama ilivyoorodheshwa katika jedwali lililo upande wa kulia.[4]
Baadhi ya mashirika yamerekebisha kidogo fasili zilizotolewa na SAD. Habari ya kiupasuaji hugawanya unene wa kupindukia wa "daraja la 3" katika vikundi zaidi, ambavyo ukadiriaji wake ungali unakumbwa na utata.[18]
Kwa sababu watu wa asili ya Asia wameendelea kuathiriwa vibaya katika kiwango cha KUM cha chini kuliko kile cha Wazungu, baadhi ya mataifa yamefasili upya unene wa kupindukia; Wajapani wameufasili kama kiwango chochote cha KUM kinachozidi 25[19] huku China ikitumia kipimo cha KUM cha juu ya 28.[20]
Uzito uliozidi huhusianishwa na magonjwa mengi, hasa magonjwa ya moyo na mishipa, kisukari aina ya 2, apnea pingani ya usingizi, aina fulani za saratani, osteoathritisi[3] na pumu[21][3]. Matokeo yake ni kwamba unene wa kupindukia umetambulika kupunguza matarajio ya kuishi.[3]
Unene wa kupindukia ni kati ya visababishi vya kifo vinavyozuilika kote ulimwenguni.[10][23][24] Utafiti mkuu wa Ulaya na Marekani umeonyesha kuwa hatari ya kufa iko chini zaidi katika kiwango cha KUM cha 20–25 kg/m2[22][25] katika watu wasiovuta sigara na 24–27 kg/m2 katika watu wanaoendelea kuvuta sigara, huku hatari hii ikiongezeka na mabadiliko kuelekea pande zote mbili.[26][27]Kipimo cha Kielezo cha Uzani wa Mwili cha zaidi ya 32 kimehusishwa na ongezeko la mara mbili la vifo kwa wanawake kwa muda wa miaka 16.[28] Nchini Marekani, inakisiwa kuwa unene wa kupindukia husababisha zaidi ya vifo 111,909 hadi 365,000 kila mwaka,[3][24] huku milioni 1 (7.7%) ya vifo katika nchi za Ulaya husababishwa na uzito uliozidi.[29][30] Kwa wastani, unene hupunguza muda wa maisha miaka 6 hadi 7:[3][31]Kielezo cha Uzani wa Mwili cha 30–35 hupunguza miaka 2 hadi 4 matarajio ya kuishi[25] ilhali unene uliokithiri (Kielezo cha Uzani wa Mwili > 40) hupunguza miaka 10 matarajio ya kuishi [25]
Unene wa kupindukia huongeza hatari ya hali nyingi za kimwili na kiakili. Ambatani hizi kwa kawaida huonyeshwa sana katika dalili za magonjwa ya metaboli,[3] kama: kisukari aina ya 2, shinikizo la juu la damu, kolestro, and hypertriglyceridemia.[32]
Matatizo aidha husababishwa na unene moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja inayohusiana kupitia utaratibu ulio na sababu sawa kama vile lishe duni au uzembe maishani. Uhusiano mkuu kati ya unene na hali maalum inatofautiana. Mojawapo ni kisukari aina ya 2. Mafuta ya ziada mwilini ndiyo kisababishi cha 64% ya kisukari kwa wanaume na 77% kwa wanawake.[33]
Madhara ya kiafya huwa katika vikundi viwili vipana:
Ingawa madhara ya kiafya ya unene wa kupindukia miongoni mwa jumla ya watu imeungwa mkono na ushahidi uliopo, matokeo ya kiafya katika vikundi mahususi yanaonekana kuboreka kwa kiwango cha Kielezo cha Uzani wa Mwili kinachoongezeka. Tukio hilo linajulikana kama fumbo kuhusu kuendelea kuishi kwa watu walio na unene wa kupindukia.[38]
Mara ya kwanza fumbo hili lilielezwa mwaka 1999, likiwakumba watu wenye unene wa kupindukia waliokuwa wakisafishwa damu,[38] kisha kupatikana katika watu waliokuwa na mshtuko wa moyo na ugonjwa wa ateri za pembeni (UAP).[39]
Katika watu waliokuwa na mshtuko wa moyo, wale wenye kipimo cha Kielezo cha Uzani wa Mwili cha kati ya 30.0. na 34.9 walikuwa na kima cha vifo cha chini kuliko wenye uzito wa kawaida. Hii ni kwa sababu watu mara nyingi hupoteza uzito kadiri wanavyoendelea kuwa wagonjwa.[40]
Matokeo sawa na haya yamepatikana katika aina nyingine za magonjwa ya moyo. Watu walio na unene wa kupindukia wa daraja la 1 na magonjwa ya moyo hawana kima cha matatizo ya moyo kuliko watu walio na uzito wa kawaida ambao wana matatizo ya moyo. Hata hivyo, katika watu walio na viwango vikubwa zaidi vya unene, hatari ya kutokea kwa matatizo ya ziada huongezeka.[41][42] Hata baada ya upasuaji wa kipenyo cha moyo, hakuna ongezeko la vifo linalotambulika katika watu walio na uzito mkubwa.[43]
Utafiti mmoja ulionyesha kuwa ongezeko la muda wa kuishi kwa watu wenye unene wa kupindukia husababishwa na matibabu madhubuti ambao watu hao hupata baada ya tukio la tatizo la moyo.[44] Utafiti mwingine unaonyesha kuwa mtu anapouchukulia kwa makini ugonjwa wa muda mrefu wa kuzibika kwa mapafu (COPD) kwa walio na PDA, manufaa ya unene wa kupindukia hayapo tena.[39]
Katikia kiwango cha mtu binafsi, ujumlisho wa kula chakula kinachotoa nguvu na kutofanya mazoezi ya kimwili hudhaniwa kusababisha visa vingi zaidi vya unene wa kupindukia.[45]Matukio machache sana husababishwa hasa na jeni, sababu za kimatibabu au ugonjwa wa akili.[46] Kinyume na matarajio, inakisiwa kuwa viwango vya unene wa kupindukia vinavyoongezeka katika jamii vinasababishwa na urahisi wa kupata chakula kinachovutia,[47]ongezeko la kutegemea gari na uzalishaji wa bidhaa kwa kutumia mitambo.[48][49]
Uhakiki mmoja wa 2006 ulionyesha mambo mengine kumi yanayochangia katika ongezeko la unene wa kupindukia wa hivi majuzi:
Kima cha ugavi wa nguvu za kimlo kwa kila mtu hutofautiana pakubwa katika maeneo na nchi mbali mbali. Kima hiki pia kimebadilika pakubwa kwa muda mrefu sasa.[51] Kutoka mwanzoni wa miaka ya 1970 hadi mwishoni wa kiaka ya 1990, wastani wa kalori kwa kila mtu kila siku (kiwango cha chakula kilichonunuliwa) uliongezeka katika maeneo yote duniani ila Mashariki mwa Uropa. Nchi ya Marekani ilikuwa na kima cha juu zaidi cha upatikanaji, ikiwa ni kalori 3,654 kwa kila mtu katika mwaka wa 1996. Kima hiki kiliongezeka zaidi hadi 3,754 katika mwaka wa 2003.[51] Katika miaka ya mwisho ya 1990 Uropa ilikuwa na kalori  3,394; kwa kila mtu. Katika maeneo yanayostawi kiuchumi ya Asia kulikuwa na kalori 2,648; kwa kila mtu na katika kusin mwa jangwa la Sahara, watu walikuwa na kalori   2,176;kwa kila mtu.[51][52] Jumla ya kalori inayotumika imetambulika kuwa inahusiana na unene wa kupindukia.[53]
Upatikanaji mkubwa wa vielekezo kuhusu lishe[54]haujafaulu kutatua shida za kula kupita kiasi na uamuzi mbaya kuhusu lishe.[55] Kutoka mwaka wa 1971 hadi 2000, viwango vya unene wa kupindukia viliongezeka kutoka 14.5% hadi 30.9%.[56] Katika kipindi hicho pia, wastani wa matumizi ya chakula kinachotoa nguvu yaliongezeka. Katika wanawake, wastani wa ongezeko hili ulikuwa kalori 335 kwa siku (1,542 mwaka wa 1971 na kalori 1,877 mwaka wa 2004), ilhali katika wanaume, wastani katika ongezeko hilo ulikuwa kalori 168 kwa siku (kalori 2,450 mwaka wa 1971 na kalori 2,618 mwaka wa 2004). Kiwango kikubwa cha nguvu hizi za ziada kilitokana na ongezeko la kutumia kabohidrati badala ya mafuta.[57] Vyanzo vya msingi vya kabohidrati hizi za ziada ni vinywaji vilivyo na sukari ambavyo vinakadiriwa kusababisha karibu 25% ya nguvu za kila siku katika vijana wakomavu Marekani, [58]na chipsi za viazi.[59] Utumiaji wa vinywaji vilivyo na sukari unaaminika kuchangia katika ongezeko la viwango vya unene wa kupindukia.[60][61]
Jinsi jamii nyingi zinavyoendelea kutegemea nguvu nyingi za chakula, viwango vikubwa vya chakula na vyakula duni, ndivyo uhusiano wa utumiaji wa vyakula duni na unene wa kupindukia unavyoendelea kusababisha madhara. [62] Nchini Marekani, utumiaji wa vyakula duni uliongezeka mara tatu huku utumiaji wa chakula chenye nguvu ukiongezeka mara nne kati ya mwaka 1977 na 1995.[63]
Sera za kilimo na ufundisanifu zinazozingatia mazingira nchini Marekani na barani Uropa zimesababisha kushuka kwa bei ya vyakula. Kule Marekani, hatua ya kupunguza bei ya mahindi, soya, ngano na mchele kupitia bili ya ukulima ya Marekani imepelekea kushuka kwa bei ya chakula cha viwandani ikilinganishwa na matunda na mboga.[64]
Wakati mwingi, watu wanene kupindukia hawaripoti vyema jinsi wanavyotumia chakula ikilinganishwa na wale walio na uzito wa kawaida.[65] Utafiti huu ni kwa mujibu wa uchunguzi wa watu uliofanyika katika chumba cha kipima kalori [66] na kwa kutazama moja kwa moja.
Mwenendo wa kuzembea huchangia pakubwa katika unene wa kupindukia.[67] Kote ulimwenguni, watu wengi wamegeukia kazi isiyohusisha nguvu nyingi za kimwili[68][69][70] na kwa wakati huu angalau 60% ya idadi ya watu duniani hupata mazoezi yasiyotosheleza.[69] Hii hasa ni kwa sababu ya ongezeko la kutumia mitambo katika uchukuzi, na teknologia inayosaidia sana kikazi huko nyumbani.T[68][69][70] Katika watoto, viwango vya kufanya mazoezi vinaonekana kushuka kwa sababu ya kutotembea sana na kutohusika katika somo la mazoezi ya mwili.[71] Mienendo ya dunia katika burudani ambapo watu huusika moja kwa mojamazoezi ya mwili inaendelea kufifia. Shirika la Afya Duniani linaonyesha kuwa, ulimwenguni kote, watu wanaendelea kuhusika katika burudani isiyohusisha maoezi, ilhali katika utafiti mmoja huko Finland[72] ulionyesha ongezeko, ilhali utafiti mwingine huko Marekani ulionyesha kuwa mazoezi katika burudani hayajabadilika sana.[73]
Katika watoto na watu wazima, kuna uhusiano kati ya kutazama runinga na hatari ya unene wa kupindukia.[74][75][76] Ukaguzi ulitambua kuwa 63 kati ya tafiti 73 (86%) zilionyesha ongezeko katika kiwango cha unene wa kupindukia wa utotoni pindi watoto wanavyofikia vyombo vya mawasiliano, huku viwango hivi vikiongezeka kulingana na muda unaotumika kutazama runinga.ref>"Media + Child and Adolescent Health: A Systematic Review" (PDF). Ezekiel J. Emanuel. Common Sense Media. 2008. Iliwekwa mnamo Aprili 6, 2009.{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)</ref>
Kama magonjwa mengine mengi, unene wa kupindukia hutokana na mwingiliano kati ya vipengele vya kijeni na vya kimazingira. Upolimofi katika jeni nyingi zinazodhibiti [[hamu ya kula[[]] na umetabolihupelekea unene wa kupindukia wakati nguvu za kutosha zinazotoka katika chakula zinapatikana. Katika mwaka wa 2006, zaidi ya 41 za sehemu hizi zimehusishwa na kuendelea kwa unene wa kupindukia wakati mazingira mwafaka yanapokuwepo.[78] Watu walio na aina mbili zajeni ya FTO (jeni inayohusishwa na wingi wa mafuta na unene wa kupindukia) wamepatikana kwa wastani kuwa na uzito wa kilogramu 3-4]] zaidi na huwa katika hatari mara1.67 zaidi ya kukumbwa na unene wa kupindukia wakilinganishwa na wale wasio na hatari hii aleli.[79] Asilimia ya unene wa kupindukia unaoweza kuhusishwa visababishi vya kijeni ni ya kubadilika kutoka 6% hadi 85% kulingana na idadi ya watu waliochunguzwa.[80]
Unene wa kupindukia ni kipengele kikuu katika sindromu kadhaa kama vile sindromu ya Prader-Willi, sindromu ya Bardet-Biedl, sindromu ya Cohen, na sindromu ya MOMO. Neno unene wa kupindukia usiosababishwa na sindromu hutumika wakati mwingine kuzitenga hali hizi.[81] Kwa watu walio na mwanzo mkali wa mapema wa unene wa kupindukia (unaofasiliwa na mwanzo kabla ya umri wa miaka 10 na kielezo cha uzani wa mwili zaidi ya tatu standard deviation zaidi ya kawaida), 7% huwa na kipimo kimoja cha mgeuko papale [82]
Tafiti zilizolenga mitindo ya urithi badala ya jeni maalum zimetambua kuwa asilimia 80 ya watoto wa watu wawili walio wanene kupindukia walikuwa vilevile na unene wa kupindukia, ikilinganishwa na asilimia chini ya 10 ya watoto wa wazazi wawili waliokuwa na uzito wa kawaida.[83]
Nadharia tete ya jeni yenye mafanikio hudai kuwa watu wana uwezekano mkubwa wa kupatwa na unene wa kupindukia kutokana na ukosefu wa chakula wakati wa mageuko ya binadamu. Uwezo wao wa kujinufaisha katika vipindi visivyo vya kawaida vya wingi kwa kuweka nguvu kama mafuta unaweza kuwafaa katika nyakati ambapo upatikanaji wa chakula si yakini na watu walio na hifadhi kubwa ya mafuta wanaweza kuwa na uwezekano mkubwa wa kuongokanjaa. Hata hivyo, huenda jamii zilizo na chakula kwa wingi zisizoee kujiwekea mafuta.[84] Nadharia hii imeweza kukosolewa sana na kupelelea kupendekezwa kwa nadharia zingine za kimageuko kama vile nadharia tete ya jeni isiyo na mkondo nanadharia tete ya fenotipu yenye mafanikiozilizopendekezwa. [85][86]
Maradhi mengine ya mwili na akili na dawa za kifamasia zinazotumiwa kuyatibu zinaweza kuongeza hatari ya unene wa kupindukia. Maradhi yanayoongeza hatari ya unene huo ni sindromu kadhaa za kijenetikia zisizo za kawaida (zilizoorodheshwa hapo juu) na aidha magonjwa mengine ya kuzaliwa nayo au ya kujitokeza baada ya kuzaliwa: uhipothiroidi, Sindromu ya Cushing, kukosa homoni ya kukua,[87] na matatizo ya kula: matatizo ya kula yatokanayo na ulevi na sindromu ya kula usiku.[3].Hata hivyo, unene wa kupindukia hauchukuliwi kuwa tatizo la kiakili na kwa hiyo haujaorodheshwa katika Mwongozo wa Utambuzi na Takwimu za Maradhi ya Akili (DSM-IVR) kama maradhi ya akili.[88] Hatari ya uzito wa kupita kiasi na unene wa kupindukia iko juu kwa wagonjwa walio na maradhi ya akili kuliko kwa watu ambao hawana maradhi ya akili.[89]
Matibabu mengine yanaweza kusababisha kuongezeka kwa uzito au mabadiliko katika mchanganyiko wa mwili; nayo ni insulini, salfonyilurea, thiasolidinedioni, dawa za magonjwa ya kiakili, dawa ya unyogovu, steroidi, aina nyingine za dawa za mitukutiko (fenitoini na valproeati), pisotifeni, na za uzuiaji mimba wa kihomoni.[3]
Ingawa athari za kijenetiki ni muhimu katika kuelewa unene wa kupindukia, haziwezi kuwajibikia mkondo uliopo wa ongezeko katika nchi fulani au duniani.[90] Ingawa imekubalika kuwa utumizi wa nguvu zaidi ya kiasi kinachostahili kutumika husababisha unene wa kupindukia kibinafsi, kisababishi cha mageuko katika vipengele hivi viwili kwa kiwango cha jamii hujadiliwa sana. Kuna nadharia kadhaa zinazohusu visababishi vya unene wa kupindukia. Hata hivyo, nadharia nyingi zimeshikilia kuwa unene husababishwa na mchanganyiko wa vipengele tofauti.
Uhusiano kati ya hadhi ya kijamii na Kielezo cha Uzani wa Mwili huwa tofauti ulimwenguni. Tathmini katika mwaka wa 1989 ilionyesha kuwa wanawake wenye hadhi ya juu ya kijamii katika nchi zinazostawii walikuwa na uwezekano mdogo wa kukumbwa na unene wa kupindukia. Hakuna tofauti muhimu zilizoonekana miongoni mwa wanaume wa hadhi tofauti za kijamii. Katika nchi zinazostawi, wanawake, wanaume na watoto kutoka katika hadhi ya juu ya kijamii walikuwa na viwango vikubwa vya unene wa kupindukia.[91]. Toleo la tathmini hii uliofanyika mwaka wa 2007 ulionyesha uhusiano uo huo lakini ulikuwa dhaifu. Upungufu katika uthabiti wa uhusiano huo ulihisika kuwa uliotokana na utandawazi.[92] Katika nchi zilizostawi, viwango vya unene wa kupindukia kwa watu wazima, na asilimia ya watoto waliobalehe walio na uzani wa kupindukia vinahusiana na tofauti za kimapato. Uhusiano kama huu hunekana katika majimbo ya Marekani: watu wengi wazima, hata walio katika matabaka ya juu katika jamii wana unene wa kupindukia hata katika majimbo yaliyo na tofauti za kimapato.[93]
Maelezo mengi yametolewa yakilinganisha Kielezo cha Uzani wa Mwili na hadhi ya kijamii. Inadhaniwa mwilia mwilizo wa kumudu vyakula bora zaidi, nao huwa katika shinikizo zaidi la kusalia wembamba kutoka kwa jamii, na wana nafasi na matumaini makubwa ya kudumisha siha njema ya kimwili. Katika nchi zisizostawi inaaminika kuwa uwezo wa kumudu chakula, utumizi mkubwa wa nguvu katika kufanya kazi za sulubu, na tamaduni zinazothamini miili mikubwa huchangia katika kuleta mitindo hii.[92] Mitazamo inayoshikiliwa na watu kuhusu ukubwa wa mwili maishani pia inaweza kuchangia unene wa kupindukia. Uhusiano wa mabadiliko katika Kielezo cha Uzani wa Mwili kwa muda mrefu umeonekana miongoni mwa marafiki, ndugu na wachumba.[94] Stress and perceived low social status appear to increase risk of obesity.[93][95][96]
Uvutaji sigara huathiri pakubwa uzani wa mtu. Watu wanaokoma kuvuta sigara huongeza uzito kwa wastani wa kilo 4.4 9.7 lb) katika wanaume na kilo 5.0 (11.0 lb) katika wanawake kwa muda wa miaka kumi.[97] Hata hivo mabadiliko katika viwango vya uvutaji yamekuwa na matokeo duni kwa viwango vya jumla vya unene wa kupindukia.[98]
Nchini Marekani, idadi ya watoto alionao mtu inahusiana na hatarisho lao la unene wa kupindukia. Hatari ya mwanamke huongezeka kwa 7% kwa kila mtoto, ilhali hatarisho la mwanamume huongezeka kwa 4%.[99] Hii inaweza kuelezwa kwa kiasi fulani kutokana na ukweli kwamba kuwa na watoto wanaokutegemea hupunguza shughuli za kimwili kwa wazazi katika nchi za Ulaya na Marekani.[100]
Katika nchi zinazostawi, ukuaji wa miji unachangia katika kiwango kinachoongezeka cha unene wa kupindukia. Nchini Uchinaviwango vya jumla vya unene wa kupindukia viko chini ya asilimia 5; hata hivyo, katika miji mingine, viwango vya unene wa kupindukia ni zaidi ya asilimia 20.[101]
Utapiamlo mwanzoni mwa maisha umeaminika kuchangia katika viwango vinavyoongezeka vya unene wa kupindukia katikanchi zinazostawi.[102]Mabadiliko ya endokrini yanayotokea katika vipindi vya utapiamlo yanaweza kuendeleza uhifadhiwaji wa mafuta mara tu chakula zaidi kiletacho nguvu kinapopatikana.[102]
Sawa na data za epidemiolojia tambuzi, na tafiti nyingi huthibitisha kuwa unene wa kupindukia unahusiana na upungufu katika utambuzi. [103] Iwapo unene wa kupindukia husababisha upungufu katika utambuzi kwa vyovyote vile bado haijulikani kwa sasa.
Utafiti wa jinsi vikolezo viambukizi vinavyoathiri umetaboli ungali katika hatua zake za kwanza. Flora ya utumbo imeonekana kutofautiana kati ya watu wembamba na wale walio na unene wa kupindukia. Kuna ishara kuwa flora ya utumbo katika watu wanene kupindukia na wale wembamba inaweza kuathiri uwezo wa umetaboli. Mabadiliko haya dhahiri katika uwezo wa umetaboli yanaaminika kuchangia kwa kiwango kikubwa katika kuvuna nguvu zinazosababisha unene wa kupindukia. Iwapo tofauti hizi ndizo visababishi vya moja kwa moja au ndiyo matokeo ya unene wa kupindukia, bado haijabainishwa kwa kiasi kisichopotosha[104]
Uhusiano kati ya virusi na unene wa kupindukia umeonekana kwa wanadamu na spishi kadhaa za wanyama. Kiasi ambacho ushirikiano huu unaweza kuwa umechangia katika kuongezeka kwa kiwango cha unene wa kupindukia bado hakijabainishwa.[105]
Flier anafupisha taratibu nyingi za pathofiziolojia zinazohusika katika ukuaji na udhibiti wa unene wa kupindukia.[106] Kitengo hiki cha utafiti kilikuwa hakijaangaziwa hadi mwaka wa 1994leptini ilipogunduliwa. Tangu ugunduzi huu ulipofanyika, taratibu zingine nyingi za homoni zinazohusika katika udhibiti wa hamu ya kula na ulaji, mitindo ya uhifadhi ya tishu ya mafuta na ukuaji wa ukinzani kwa insulini zimefumbuliwa. Tangu kuvumbuliwa kwa leptini, grelin, insulini, oreksini, PYY 3-36, kolesistokinini,adiponektini, na vipengele vinginevyo zimechunguzwa. Adipokini ni chembe zinazoundwa na tishu ya mafuta; utendakazi wake unadhaniwa kubadilisha magonjwa mengi yanayohusiana na unene wa kupindukia.
Inachukuliwa kuwa leptini na grelini hufanya kazi pamoja katika jinsi zinavyoathiri hamu ya kula; huku grelini, inayotolewa na tumbo, ikirekebisha uthibiti wa muda mfupi wa hamu ya kula (yaani kula wakati ambapo tumbo liko tupu na kukoma tumbo inapotanuka). Leptini hutolewa na tishu ya mafuta kuchochea hifadhi za mafuta mwilini na kupatanisha uthibiti wa muda mrefu wa hamu ya kula (yaani, kula kwa wingi ambapo hifadhi za mafuta ziko chini na kula kiasi kidogo zinapokuwa juu). Ingawa utoaji wa leptini unaweza kufaa katika kikundi kidogo cha watu wenye unene wa kupindukia walio na upungufu wa leptini, watu wengi wenye unene huu hufikiriwa kuwa wenye ukinzani wa leptini na wamepatikana kuwa na viwango vya juu vya leptini.[107] Ukinzani huu hufikiriwa kueleza kwa kiasi fulani sababu inayofanya utoaji wa leptini usionekane kufaa katika kukandamiza hamu ya kula kwa watu wengi walio na unene wa kupindukia.[106]
Ingawa leptini na grelini hutolewa pembezoni, zinadhibiti hamu ya kula kupitia jinsi zinavyoathirimfumo mkuu wa neva. Hasa, leptini na grelini, na homoni zingine zinazohusiana na hamu ya kula huichochea hipothalamasi, sehemu ya ubongo iliyo muhimu zaidi katika kudhibiti ulaji na utumiaji wa nguvu. Kuna mizunguko kadhaa katika hipothalamasi inayochangia kwenye jukumu lake katika kuongeza na kudumisha hamu ya kula, ambapomelanokotini ndiyo njia inayoeleweka vizuri sana.[106] Mzunguko huu huanzia katika sehemu ya hipothalamasi iitwayo kiini akueti, ambayo matokeo yake huenda kwenye hipothalamasi ya pembeni na hipothalamasi inayotambua shibe, sehemu za ubongo zinazodhibiti kula na shibe mtawalia.[108]
Kiini akueti kina makundi mawili tofauti ya nyuroni.[106] Kundi la kwanza hudhirisha nuropeptaidi Y na peptaidi inayohusiana na agouti kwa pamoja na kuchangia katika kuichochea hipothalamasi ya pembeni na kuikandamiza hipothalamasi inayotambua shibe. Kundi la pili hudhihirisha pro-opiomelanokotini na nakala inayodhitiwa na kokeni na amfetamini (NIKA) na huchangia katika kuichochea hipothalamasi inayotambua shibe na kuikandamiza hipothalamasi ya pembeni. Kwa hiyo, nyuroni za nuropetaidi Y/peptaidi inayohusiana na agouti (NPY/AgRP) huchochea kula na kuzuia kushiba, ilhali nuroni za POMC/NIKA huchochea kushiba na kuzuia kula. Makundi yote mawili ya nuroni za kiini akueti nuroni hudhibitiwa kwa kiasi fulani na leptini. Leptini hukandamiza kundi la nuropetaidi Y/peptaidi inayohusiana na agouti (NPY/AgRP) huku ikilichochea kundi la POMC/NIKA. Kwa hivyo, ukosefu wa uchochelezi wa leptini, iwe ni kutokana na ukosefu wa leptini au ukinzani kwa leptin, hupelekea kula zaidi na inaweza kusababisha unene wa kupindukia wa kijenetikia na wa kupatikana maishani.[106]
Shirika la Afya Duniani (WHO) linatabiri kuwa hivi karibuni, uzito wa kupita kiasi na unene wa kupindukia unaweza kuchukua nafasi ya matatizo ya jadi ya afya ya umma kama vile utapiamlo na magonjwa ya kuambukiza kama visababishi vikuu vya afya duni.[109] Unene wa kupindukia ni tatizo la afya ya umma na la kisera kwa sababu yaueneaji wake, gharama na athari za kiafya.[110] Juhudi za afya ya umma hulenga kuelewa na kurekebisha mazingira yanayochangia kukithiri kwa unene wa kupindukia miongoni mwa watu. Suluhisho hutazamia kubadilisha mambo yanayosababisha utumiaji zaidi wa vyakula viletavyo nguvu na kukandamiza shughuli/mazoezi ya mwili. Juhudi ni programu za milo zinazofadhiliwa na serikali katika shule, kupunguza uuzaji wachakula visivyo bora kwa watoto, [111] na kupunguza upatikanaji wa vinywanji vyenye sukari katika shule.[112] Juhudi zimefanywa katika uundaji wa mazingira ya miji ili kuongeza ufikiaji wa bustani na kutengeneza njia za waendao kwa miguu.[113]
Nchi nyingi pamoja na vikundi vimechapisha ripoti zinazohusu unene wa kupindukia. Mnamo mwaka wa 1998, miongozo ya kwanza ya serikali ya shirikisho ya Marekani ilichapishwa kwa jina "Clinical Guidelines on the Identification, Evaluation, and Treatment of Overweight and Obesity in Adults: The Evidence Report" (Mwongozo wa Kitabibu kuhusu Utambuzi, Utathmini na Matibabu ya Unene na Unene wa Kupindukia katika Watu Wazima).[114] Mnamo mwaka wa 2006 Mfumo wa Unene wa Kupindukia wa Kanada ulichapisha "Canadian Clinical Practice Guidelines (CPG) on the Management and Prevention of Obesity in Adults and Children" [Taratibu za Kitabibu za Kanada zinazohusu Udhibiti na uzuiaji wa Unene wa Kupindukia kwa Watu Wazima na Watoto] Huu ni utaratibu wa kina unaozingatia ushahidi ili kushughulikia udhibiti na uzuiaji wa uzani wa kupita kiasi na unene wa kupindukia kwa watu wazima na watoto.[115]
Mnamo mwaka wa 2004 nchini Uingereza, Chuo cha Mafizishiani cha Royal, Kitengo cha Afya ya Umma na Chuo cha Pediatria na Afya ya Watoto vilitoa ripoti, “Kuhifadhi Matatizo", iliyodokeza kuhusu kuongezeka kwa tatizo la unene wa kupindukia nchini Uingereza. [116] Mwaka huohuo, Kamati Teule ya Afya ya Bunge la Uingereza ilichapisha "uchunguzi wake wa kina zaidi [...] uliowahi kufanywa kuhusu athari ya unene wa kupindukia kwa afya na jamii nchini Uingereza na njia mwafaka zinazoweza kutumiwa katika kutatua tatizo hili.[117] Mwaka wa 2006, Taasisi ya Kitaifa ya Afya na Ubora wa Kitabibu ilitoa utaratibu wa kutambua na kutibu unene wa kupindukia na vilevile athari za kisera kwa mashirika yasiyo ya kiafya kama vile mabaraza ya mitaa[118] Ripoti iliyotolewa na Bwana Derek Wanless mwaka wa 2007 kwa Hazina ya Mfalme ilionya kuwa iwapo hatua zaidi hazitachukuliwa, unene wa kupindukia una uwezo wa kulemaza Huduma ya Afya ya Kitaifakifedha.[119]
Hatua za kina zinabuniwa ili kuthibiti viwango vinavyoongezeka vya unene wa kupindukia. Mfumo wa Sera ya Kukabiliana na Unene wa Kupindukia hugawanya hatua kwa sera za ‘juu’, sera za ‘katikati’ na sera za ‘chini’. Sera za ‘juu’ zinalenga kubadilisha jamii, sera za ‘kati’ hujaribu kubadilisha mienendo ya watutu ili kuzuia unene wa kupindukia nazo sera za ‘chini’ hujaribu kuwahudumia wale ambao tayari wameathirika.[120]
Matibabu makuu ya unene wa kupindukia ni kudhibiti jinsi unavyokula and mazoezi ya mwili.[45]Mipango ya lishe inaweza kupelekea kupoteza uzitokwa kipindi cha muda mfupi[121] lakini kudumisha kiwango hiki cha kupoteza uzito mara nyingi huwa vigumu na hivyo huhitaji kudumisha mwenendo wa maisha ya mazoezi ya kimwili na kula chakula kilicho na kiwango cha chini cha nguvu.[122][123]Kufanikiwa kudumisha kiwango cha kupoteza uzani na mabadiliko katika mienenbo ni chini mno kati ya asilimia 2 - asilimia 20.[124]Mabadiliko ya kilishe na kimienendo ni muhimu katika kudhibiti uongezaji wa kupita kiasi wa uzani katika ujauzito na kuboresha hali ya mama na mtoto.[125]
Aina moja ya dawa, Orlistat (Xenical), inapatikana kwa urahisi na imeidhinishwa kwa matumizi ya muda mrefu. Hata hivyo, kupoteza uzito ni jambo la kadri kwa wastani wa kilogramu 2.9 kg (6.4 lb) kwa mwaka 1 hadi 4 na kuna habari kidogo kuhusu jinsi dawa hizi zinavyoathiri matatizo ya muda mrefu ya unene wa kupindukia.[126] Matumizi yake yanahusiana na viwango vya juu vya athari kwa utumbo [126] and concerns have been raised about negative effects on the kidneys.[127] Aina zingine mbili za dawa pia zinapatikana Lorcaserin(Belviq) hupelekea upotezaji wa uzito kwa wastani kilogramu 3.1 (asilimia 3 ya uzani wa mwili) zaidi ya plasebo kwa muda wa mwaka mmoja.[128] Mchanganyiko wa phentermine na topiramate (Qsymia) pia ni bora kwa kiwango fulani.[129]
Njia mwafaka zaidi ya kutibu unene wa kupindukia ni upasuaji wa kibariatriki. Upasuaji kwa mujibu wa unene mkali wa kupindukia unahusiana na upotezaji wa uzito kwa muda mrefu na upunguaji katika vifo kwa ujumla. Utafiti mmoja ulitambua upotezaji wa uzito wa kati wa asilimia 14 na 25 (kulingana na utaratibu uliofuatwa) kwa miaka 10 na upunguaji wa asilimia 29 katika vifo vitokanavyo na unene huu ikilinganishwa na hatua za kawaida za upotezaji wa uzito.[130] Hata hivyo, kutokana na gharama yake na hatari ya matatizo, watafiti wanatafuta tiba zingine mwafaka ilhali zisizo na madhara.
Kabla ya karne ya 20, unene wa kupindukia ulikuwa wa nadra;[132] in 1997 the WHO formally recognized obesity as a global epidemic.[58] As of 2005 the WHO estimates that at least 400 million adults (9.8%) are obese, with higher rates among women than men.[133] Kiwango cha unene wa kupindukia pia huongezeka kulingana na umri kwa angalau kufikia umri wa miaka 50 au 60 [134] na unene mkali wa kupindukia nchini Marekani, Australia, na Canada unaongezeka haraka kuliko kiwango cha jumla cha unene wa kupindukia.[18][135][136]
Ijapokuwa uliwahi kuchukuliwa kama tatizo la nchi zilizo na mapato ya juu pekee, viwango vya unene wa kupindukia vinaongezeka ulimwenguni kote na kudhuru nchi zilizostaw na aidha zinazostawi[29].Ongezeko hili limeonekana sana katika maeneo ya miji.[133] Sehemu inayobakia ulimwenguni ambayo unene wa kupindukia sio jambo la kawaida nimataifa ya kusini mwa sahara.[3]
Wagiriki ndio waliokuwa wa kwanza kutambua unene wa kupindukia kama tatizo la kiafya.[132] "Hippocrates aliandika kuwa "Unene wa kupindukia si ugonjwa kivyake tu, bali ni dalili ya magonjwa mengine".[3] Daktari Mhindi wa upasuaji Sushruta (karne ya 6 BCE) alihusisha unene wa kupindukia na kisukari na matatizo ya moyo.[138] He recommended physical work to help cure it and its side effects.[138]Katika historia ya watu, wanadamu wamekumbwa sana na ukosefu wa chakula.[139]Kwa hivyo, kihistoria, unene wa kupindukia umeonekana kama ishara ya utajiri na ustawi. Ulikuwa umekithiri kwa maafisa wakuu barani Uropa katika Enzi za Kati na Kipindi cha Mvuvumko[137] as well as in Ancient East Asian civilizations.[140]
Kwa kuwepo kwa mwanzo wa mvuvumko wa viwanda, iligunduliwa kuwa uwezo wa kijeshi na kiuchumi wa mataifa ulitegemea ukubwa wa mwili na nguvu za wanajeshi na wafanyikazi.[58] Kuongeza wastani wa kielezo cha uzito wa mwili kutoka kile kinachofikiriwa kuwa uzito wa chini hadi kwa kile kilicho anuwai ya kawaida kulichangia pakubwa katika ustawi wa jamii zilizo na viwanda.[58] Kutokana na hayo, kimo na uzito viliongezeka katika karne ya 19 katika nchi zilizostawi. Katika karne ya 20, watu walipofikia kikamilifu uwezo wao wa kijenetiki wa kimo, uzito ulianza kuongezeka sana zaidi ya kimo na kupelekea unene wa kupindukia.[58]Katika miaka ya 1950, kuongezeka kwa utajiri katika nchi zilizostawi kulipunguza vifo vya watoto. Hata hivyo, uzito ulipoongezeka, ugonjwa wa moyo na figo ulikithiri.[58][141] Katika kipindi hiki, kampuni za bima ziligundua uhusiano kati ya uzito na matarajio ya muda wa kuishi na hivyo basi zikaongeza malipo ya bima kwa walio na unene wa kupindukia.[3]
Tamaduni nyingi katika historia zimeona unene wa kupindukia kama ambayo inatokana na makosa ya kimienendo. Mwigizaji aliyekuwa na obesus au mafuta katikauigizaji wa Kigriki aliwakilisha ulafi na utani. Katika nyakati za Ukristo, chakula kilichukuliwa kama njia inayoelekeza kwenye dhambi za uzembenatamaa.[12] Katika tamaduni za kisasa za Ulaya na Marekani, unene wa kupita kiasi unachukuliwa kama jambo lisilovutia na unene wa kupindukia mara nyingi huhusishwa na mambo kadhaa mabaya yasiyo na uasili. Watu wa umri tofauti wanaweza kufedheheshwa na kulengwa na wadhalimu au kutengwa na wenzao. Unene wa kupindukia kwa mara nyingine ni sababu ya ubaguzi[142]
Fahamu za umma katika jamii ya Ulaya na Marekani kuhusu uzito bora wa mwili zinatofautiana na zile zinazohusu uzito unaofikiriwa kuwa bora – na zote zimebadilika tangu mwanzo wa karne ya 20. Uzito unaochukuliwa kuwa bora umekuwa chini tangu miaka ya 1920. Marekani uliongezeka kwa asilimia 2 kutoka mwaka wa 1922 hadi 1999 ilhali wastani wa uzito wao ulipungua kwa asilimia 12.[143] Kwa upande mwingine, mitazamo ya watu kuhusu uzito bora imebadilika na kuchukua mkondo pinzani. Nchini Uingereza, uzito ambapo watu walijiona kuwa na uzito wa kupita kiasi ulikuwa juu kwa kiasi cha haja katika mwaka wa 2007 kuliko 1999.[144] Mabadiliko haya yanaaminika kusababishwa na viwango vinavyoongezeka vya uadiposi (unene), hali inayopelekekea ukubalifu wa mafuta ya ziada mwilini kama jambo la kawaida.[144]
Unene wa kupindukia ungali unachukuliwa kuwa ishara ya utajiri na ufanisi katika sehemu nyingi za Afrika. Hili limekuwa jambo la kawaida hasa tangu kuzuka kwa janga la VVUlilianza. [3]
Sanaa ya kwanza ya uchongaji iliyoleta mfano wa mwili wa binadamu kati ya miaka 20,000 - 35,000 iliyopita ilionyesha wanawake walio na unene wa kupindukia. Baadhi ya watu huihusisha sanamu ya Zuhurana juhudi za kusisitiza uwezo wa kuzaa ilhali wengine huhisi kuwa wao husimamia “unene” kwa watu wa wakati huo.[12] Hata hivyo, unene wa kupindukia haupo katika sanaa ya Wagiriki na Waroma, yamkini kwa kudumisha ulimbwende wao kwa mujibu wa kiasi. Haya yaliendelea katika sehemu kubwa ya historia ya ukristo barani Uropa ambapo wale tu walio na mapato ya chini wakichukuliwa kuwa wenye unene wa kupindukia.[12]
Katika Kipindi cha Mvuvumko, baadhi ya watu katika tabaka la juu walianza kuuringia ukubwa wao jinsi inavyoonekana katika picha za Henry wa nane na Alessandro del Borro.[12]Rubens (1577–1640) alionyesha wanawake wenye miili mikubwa katika picha zake, ambapo anatoa neno Rubenesque. Hata hivyo, wanawake hawa bado walilidumisha umbo la shisha na uhusiano wake na uwezo wa kuzaa.[145] Katika karne ya 19 mitazamo kuhusu unene wa kupindukia ilibadilika katika nchi za Ulaya na Amerika. Baada ya karne kadhaa ambapo unene wa kupindukia ulihusiana na mali na hadhi ya kijamii katika jamii, wembamba ulianza kuonekana kama kipimo kifaacho.[12]
Pamoja na athari zake za kiafya, unene wa kupindukia husababisha matatizo mengi yakiwemo ugumu katika ajira [146][147] na gharama za juu za biashara. Athari hizi zinazikumba sekta zote za jamii kutoka kwa watu binafsi, hadi kwa mashirika, na hadi kwa serikali.
Katika mwaka wa 2005, gharama za kimatibabu zinazoweza kuhusishwa na unene wa kupindukia nchini Marekani zilikuwa takribani dola bilioni 190.2 au asilimia 20.6 ya gharama zote za kimatibabu,[148] [149][150] while the cost of obesity in Canada was estimated at CA$2 billion in 1997 (2.4% of total health costs).[45] Jumla ya gharama ya unene wa kupindukia nchini Kanada ilikuwa imekadiriwa kuwa dola bilioni 2 za Australia katika mwaka wa 2005. Waustralia walio na uzito wa kupita kiasi na wanene kupindukia pia walipokea dola za Australia bilioni 35.6 kama ruzuku kutoka kwa serikali.[151] Kadiri ya gharama ya bidhaa za lishe imekadiriwa kuwa kati ya dola bilioni 40 hadi dola bilioni 100  nchini Marekani pekee.[152]
Miradi ya kuzuia unene wa kupindukia imezinduliwa ili kupunguza gharama ya kutibu magonjwa yanayohusiana na unene huu. Hata hivyo, jinsi watu wanavyoendelea kuishi ndivyo wanavyogharamika zaidi. Kwa hivyo, watafiti huafiki kuwa kupunguza unene wa kupindukia kunaweza kuidumisha afya ya umma lakini huenda isipunguze gharama ya jumla ya afya..[153]
Unene wa kupindukia unaweza kusababisha fedheha ya kijamii na ugumu katika ajira.[146] Wakilinganishwa na wenzao walio na uzito wa kawaida, wafanyikazi walio na unene wa kupindukia kwa wastani wana viwango vya juu vya kutokuwa kazini kwao na huchukua likizo ya udhaifu mara kwa mara na kupelekea kuongezeka kwa gharama upande wa waajiri na kupunguka kwa tija.[155] Utafiti wa kuwachunguza wafanyikazi wa chuo kikuu cha Duke ulionyesha kuwa watu walio na kielezo cha uzito wa mwili zaidi ya 40 walijiandikisha kufidiwa katika fidia ya wafanyikazi mara mbili zaidi ya wale ambao kielezo chao cha uzito wa mwili kilikuwa 18.5-24.9. Pia siku zao za kutofika kazini kwao zilikuwa zaidi ya mara 12 ikilinganishwa na wenzao wasio na kielezo cha juu cha uzito wa mwili. Majeraha ya mara kwa mara katika kikundi hiki yalitokana na kuanguka na kunyanyuka hivyo ikiathiri miguu, vifundo vya mikono au mikono, na migongo.[156] Bodi ya Bima ya Wafanyikazi katika Jimbo la Alabama nchini Marekani iliidhinisha mpango tata wa kuwatoza wafanyikazi walio na unene wa kupindukia dola 25 kila mwezi iwapo hawachukui hatua za kuupunguza uzito wao na kudumisha afya yao. Hatua hizi zilianza Januari 2010 na zinalenga wale walio na Kielezo cha Uzito wa Mwili cha zaidi ya kilo 35 kwa kila mita 2 wanaokosa kuboresha afya yao baada ya mwaka mmoja.[157]
Utafiti fulani umeonyesha kuwa watu walio na unene wa kupindukia wana uwezekano mdogo wa kuajiriwa na pia wana uwezekano mdogo wa kupandishwa cheo.[142] Watu hawa pia hulipwa mshahara wa chini kuliko wenzao wasio na unene huu wa kupindukia kwa kazi sawa. Wanawake na wanaume walio na unene wa kupindukia kwa wastani hupata asilimia 6 na 3 chini mtawalia.[158]
Nyanja mahususi kama vile shirika la ndege, afya na nyanja za vyakula, zina matatizo maalumu. Kutokana na viwango vinavyoongezeka vya unene wa kupindukia, mashirika ya ndege yanakumbwa na gharama ya juu ya mafuta na shinikizo la kuongeza upana wa viti.[159] Katika mwaka wa 2000, uzito wa ziada wa abiria wenye unene wa kupindukia uliyagharimu mashirika ya ndege dola za Marekani milioni 275 .[160] Ulimwengu wa afya umelazimika kuwekeza katika vifaa maalumu vya kuwashughulikia wagonjwa walio na unene zaidi wa kupindukia vikiwemo vifaa maalumu vya kunyanyua na ambyulensi ya kibariatrikis.[161]Gharama za hoteli zimeongezwa na mahakama kwa shutma za kusababisha unene wa kupindukia.[162] Mnamo mwaka wa 2005, bunge la Marekani lilijadili utungaji sheria ya kuzuia kesi za raia dhidi ya sekta ya vyakula kwa mujibu wa unene wa kupindukia; hata hivyo, haikufanikiwa kuwa sheria..[162]
Lengo kuu la vuguvugu la ukubalifu wa unene ni kupunguza ubaguzi dhidi ya watu walio na unene na uzito wa kupindukia.[163][164] Hata hivyo, wengine katika vuguvugu hilo pia wanajaribu kupinga uhusiano uliothibitishwa kati ya unene wa kupindukia na athari mbaya za kiafya.[165]
Kunayo mashirika kadhaa yanayoendeleza ukubalifu wa unene wa kupindukia. Umaarufu wa mashirika haya umeongezeka katika nusu ya hivi karibuni ya karne ya 20 .[166]Shirika la Kitaifa la Kuendeleza Ukubalifu wa Unene]] nchini Marekani [[lilianzishwa mwaka wa 1969 na hujieleza kama shirika la haki za raia linalolenga kukomesha ubaguzi wa ukubwa.[167] Hata hivyo, uhamasishaji juu ya unene umebaki harakati za pembeni.[168]
Shirika la Kimataifa la Ukubalifu wa Ukubwani shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa mnamo mwaka wa 1997. Shirika hili ni la kimataifa na hueleza lengo lake kama kuendeleza ukubalifu wa ukubwa na kusaidia kukomesha ubaguzi kwa misingi ya uzito.[169] Vikundi hivi mara nyingi hupigania kutambulika kwa unene wa kupindukia kama ulemavu chini ya Sheria ya Wamarekani Walio na Ulemavu Hata hivyo, mfumo wa kisheria wa Marekani umeamua kuwa gharama zitakazokuwa za afya ya umma zinazidi faida za kueindeleza sheria hii ya dhidi ya ubaguzi kujumlisha unene wa kupindukia.[165]
Kielezo cha Uzito wa Mwili mwafaka hutofautiana kulingana na umri na jinsia ya mtoto. Unene katika watoto na vijana huelezwa kama Kielezo cha Uzito wa Mwili cha zaidi ya asilimia.[16]95. Data ya marejeo yenye ndio mzingi wa asilimia hizi ni kutoka 1963 hadi 1994 na hivyo haijaathiriwa na ongezeko la kiwango cha unene cha hivi karibuni.[17] Unene wa utotoni umefika kiwango cha mlipuko katika karne ya 21 , kukiwa na ongezeko la kiwango katika nchi zimeendelea na zinazoendelea. Kima cha unene kwa wavulana chini Kanada imeongezeka kutoka 11% miaka ya 1980s hadi zaidi ya 30% miaka ya 1990, bali kwa kipindi cha muda huu kiwango kiliongezeka kutoka 4 hadi 14% katika watoto wa Brazili.[170]
Kama ilivyo na unene katika watu wazima, hali nyingi tofauti huchangia kwa viwango vingi ongezeko la unene utotoni. Ubadilishaji wa lishe na upungufu wa mazoezi ya mwili huaminika kuwa ndizo visababishi viwili vya hivi karibu muhimu zaidi vya ongezeko la viwango.[171] Kwa sababu unene wa utotoni huendelea hadi wakati wa utu uzima na unahusishwa na magonjwa mengi yanayodumu, watoto walio wanene mara nyingi huchunguzwashinikizo la juu la damu, Ugonjwa wa kisukari, hipalipidimia, na ini yenye mafuta.[45] Matibabu yanayotumika kwa watoto hasa ni hatua ya hali ya maisha na mbinu za mwenendo, hata hivyo bidii za kuongezea mazoezi kwa watoto zimekuwa na mafanikio madogo.[172]Nchini Marekani, dawa hazikubaliwi na Muungano wa Chakula na Dawa kutumika katika kikundi hiki cha umri.[170]
Unono katika mifugo ni jambo la kawaida katika nchi nyingi. Kiwango cha unono uliozidi katika mbwa kule Marekani ni kutoka 23% hadi 41%, 5.1% yao wakiwa ni wanono.[173]Rates of obesity in cats was slightly higher at 6.4%.[173]Nchini Australia kiwango cha unene wa kupindukia katika mbwa kwa muktadha wa utabibu wa mifugo imepatikana kuwa 7.6%.[174] Hatari za unono kwa mbwa inahusiana na unene wa wamiliki; hata hivyo, hakuna uhusiano kama huo baina ya paka na wamiliki.[175]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.