Remove ads
From Wikipedia, the free encyclopedia
Utandawazi (kwa Kiingereza globalization) ni neno lililoanza kutumika miaka ya 1990, likimaanisha kukifanya kitu kuwa katika kiwango cha kimataifa, na kukihamisha nje ya mipaka na kukifanya kuwa cha wazi na kikafanywa na watu wa aina zote duniani.
Utandawazi ni njia ambayo wenyeji au taifa hufanya mambo kuwa ya kimataifa, kufanya mambo pamoja duniani. Inahusu suala zima la uchumi au biashara, teknolojia, siasa na utamaduni vilevile.
Utandawazi pia una maana ya jambo linalolenga umiliki wa kifikra na wa kiutamaduni juu ya tamaduni nyingine zilizo dhaifu, kwa ajili ya kusaidiana na kuungana yaani kuwa kitu kimoja, kuondoa mipaka na masafa kati ya nchi na nchi, kukusanyika pamoja na kuleta kitu kinachoitwa "kijiji-ulimwengu" [1]
Watu wana msimamo tofauti sana kuhusu suala hilo la utandawazi: baadhi wanahisi kwamba unasaidia kila mtu, wakati kuna wengine wanafikiria kwamba unaumiza baadhi ya watu. Kati ya madhara ya utandawazi katika jamii fulani kuna kuiga utamaduni wa kigeni (kwa mfano kuvaa nguo fupi) bila kufanya tathmini kwanza kama unafaa au sio.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.