Remove ads
nchi katika Ulaya Kusini-Mashariki From Wikipedia, the free encyclopedia
Ugiriki (pia: Uyunani; kwa Kigiriki cha kisasa: Ελλάδα, Ellada, au Ελλάς, Ellas) ni nchi ya Ulaya Kusini-Mashariki iliyopo kusini mwa rasi ya Balkani.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Ελευθερία ή Θάνατος (Eleftheria i thanatos - "Uhuru au mauti") | |||||
Wimbo wa taifa: Ύμνος εις την Ελευθερίαν - "Wimbo la Uhuru" | |||||
Mji mkuu | Athens | ||||
Mji mkubwa nchini | Athens | ||||
Lugha rasmi | Kigiriki | ||||
Serikali Rais Waziri Mkuu |
Jamhuri Katerina Sakellaropoulou (Κατερίνα Σακελλαροπούλου) Kyriakos Mitsotakis (Κυριάκος Μητσοτάκης) | ||||
Uhuru Ilitangazwa Ilitambuliwa |
25 Machi 1821 1829 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
131,957 km² (ya 95) 1.51 | ||||
Idadi ya watu - 2021 kadirio - 2012 sensa - Msongamano wa watu |
10,678,632 (ya 85) 10,816,286 77/km² (ya 120) | ||||
Fedha | Euro (€)2 (EUR ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
EET (UTC+2) EEST (UTC+3) | ||||
Intaneti TLD | .gr 3 | ||||
Kodi ya simu | +30
- | ||||
1 Wananchi walikataza kurudi kwa ufalme tar. 8 Desemba 1974. 2 Prior to 2001: Greek Drachma. |
Imepakana na Albania, Masedonia Kaskazini, Bulgaria na Uturuki. Upande wa kusini-magharibi na kusini-mashariki kuna pwani ndefu kwenye Bahari ya Mediteranea.
Kijiografia huwa na sehemu za Ugiriki bara, rasi ya Peloponesi upande wa kusini inayounganishwa kwa shingo ya nchi nyembamba, halafu visiwa vingi upande wa Bahari ya Aegean, Bahari ya Adria na kwenye Mediteranea yenyewe. Visiwa vikubwa zaidi ni Kreta, Euboea, Lesbo na Rhodos.
Ugiriki ni nchi yenye historia ndefu na maarufu sana, hata inaitwa "nchi mama ya Ulaya" na kitovu cha Ustaarabu wa magharibi, kwa sababu ndipo vilipoanza demokrasia, falsafa ya magharibi, fasihi ya magharibi, historiografia, sayansi ya siasa, tafiti za sayansi na hisabati, tamthilia na michezo ya Olimpiki.
Ugiriki ni nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya tangu 1981.
Lugha ya Kigiriki inaendelea kuandikwa kwa Alfabeti ya Kigiriki inayotumiwa tangu miaka 3000 iliyopita, lakini lugha yenyewe imebadilika. Wagiriki wa leo hawaelewi tena Kigiriki cha Kale moja kwa moja.
Wakazi wengi wanafuata dini ya Ukristo (93%), hasa katika Kanisa la Kiorthodoksi la Kigiriki (90%), halafu Waprotestanti na Wakatoliki. 2% ni Waislamu.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: others (link){{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link), 257 pp.{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link), 376 pp.{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ugiriki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.