Remove ads
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ustaarabu wa magharibi ni utamaduni wenye taratibu za kijamii, maadili, desturi, sheria, falsafa, imani, siasa, sanaa na teknolojia maalumu ambavyo asili yake ni Ulaya hata kame vimezidi kustawi sehemu nyingine za dunia ambazo historia yake ilikuwa na uhusiano wa pekee na bara hilo.
Kwa kiasi kikubwa ni urithi wa Ugiriki wa Kale, Roma wa Kale, Uyahudi,[1] na utamaduni wa makabila mengine[2][3]lakini hasa wa Ukristo na madhehebu yake ya kwanza, Kanisa Katoliki,[4][5][6][7][8][9][10][11] pamoja na Makanisa ya Kiorthodoksi[12][13].
Baada ya Matengenezo ya Kiprotestanti, athari yake imekuwa kubwa pia, hasa Ulaya Kaskazini na makoloni yake, kama yale yaliyounda Marekani, ambayo katika karne ya 20 imeshika uongozi wa dunia na kuzidi kusambaza ustarabu huo.[14][15]
Tabia yake ya msingi ni kujali na kustawisha akili badala ya kutegemea visasili na mapokeo. Ilikuwa hivyo kuanzia falsafa ya Shule ya Athene, ikaendelea baada ya uenezi wa Ukristo kupitia Teolojia ya Shule, Renaissance, Mapinduzi ya Kisayansi hadi Falsafa ya Mwangaza. Hiyo ilisaidia kutambua tunu kama haki za binadamu, usawa na demokrasia. [16]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.