From Wikipedia, the free encyclopedia
Lesbo (kwa Kigiriki: Λέσβος, Lésvos) ni kisiwa cha Ugiriki katika Bahari ya Aegean chenye eneo la Km² 1,633.
Kina wakazi 86,436 (2011) wanaotegemea zaidi uvuvi na utalii. Makao makuu yako Mutilene.
Mwaka 58 Mtume Paulo, katika safari yake ya tatu ya kimisionari, aliabiri kutoka huko hadi Samos akielekea Yerusalemu[1].
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.