Remove ads
From Wikipedia, the free encyclopedia
Utapiamlo ni hali ambayo hutokana na kupata chakula ambacho virutubishi vyake havitoshi au viko vingi hadi kusababisha matatizo upande wa afya.[1][2]
Hutumika mara kwa mara kurejelea hasa ukosefu wa lishe ambapo hakuna kalori, proteni au lishe vya kutosha; hata hivyo, hujumuisha pia kupata lishe kupita kiasi.[3][4]
Kwa njia ya chakula mwili unapokea virutubishi vya lazima kama vileː
Uhaba au wingi mkubwa wa vitu hivyo kwa muda fulani unasababisha utapiamlo.
Hivyo kuna aina mbili za utapiamlo: kukosa kiwango cha kutosha cha chakula na kukosa uwiano wa virutubishi katika chakula.
Utapiamlo
Kukosa lishe ya kutosha hutokana na kukosa chakula kizuri cha kutosha.[5] Hii hutokana na bei ya juu ya chakula na umaskini.[2][5] Kukosa kunyonya matiti mapema kunaweza kuchangia, pia maradhi ya kuambukiza kama vile: homa ya matumbo, nimonia, malaria na ukambi ambao huongeza mahitaji ya lishe.[5]
Ikiwa ukosefu wa lishe utatokea wakati wa ujauzito au kabla ya umri wa miaka miwili huenda ukasababisha matatizo ya kudumu katika ukuaji wa mwili au akili.[2] Ukosefu mkali wa lishe, unaojulikana kama kukosa chakula, unaweza kuwa na dalili ambazo zinajumuisha: kimo cha chini; wembamba; viwango vya chini sana vya nguvu; na miguu na tumbo kuvimba.[2][3] Watu hawa hugonjeka na kuwa baridi mara kwa mara. Dalili za ukosefu wa lishe hutegemea lishe ambayo inakosekana.[3]
Kuna aina mbili kuu za ukosefu wa lishe: ukosefu wa lishe ya protini inayoleta nguvu na ukosefu wa lishe.[4] Ukosefu wa protini inayoleta nguvu ni ya aina mbili: nyongea (ukosefu wa protini na kalori) na unyafuzi (ukosefu wa protini tu).[3]
Ukosefu wa kawaida wa lishe ni pamoja na: madini, aidini na vitamini A.[3] Wakati wa ujauzito, kwa sababu ya hitaji lililoongezeka, ukosefu huo hutokea sana.[6]
Katika baadhi ya nchi zinazoendelea lishe kupita kiasi kwa njia ya unene imeanza kutokea katika jamii sawa kama za walio na upungufu wa lishe.[7]
Sababu nyingine za utapiamlo hujumuisha anorexia nervosa na bariatric surgery.[8][9]
Kwa wazee utapiamlo hutokea zaidi kwa sababu ya mambo ya kimwili, kisaikolojia na ya kijamii.[10]
Juhudi za kuboresha lishe ni kati ya njia nzuri zaidi za kusaidia kukua.[11] Kunyonyesha kunaweza kupunguza viwango vya utapiamlo na vifo katika watoto,[2] na juhudi za kukuza tabia hii hupunguza viwango vya utapiamlo.[12]
Katika watoto wadogo kuwapa chakula kwa kuongezea maziwa ya matiti kati ya miezi sita na miaka miwili huboresha matokeo.[12] Kuna pia ushahidi mzuri unaounga mkono virutubishi vya lishe kadhaa wakati wa ujauzito na kati ya watoto wadogo katika nchi zinazoendelea.[12] Njia zinazofaa ni kuwapa chakula watu wanachokihitaji sana, kuwasilisha chakula na kutoa pesa ili watu waweze kununua chakula katika masoko yao.[11][13]
Kuwalisha watu shuleni tu hakutoshi.[11] Kudhibiti utapiamlo mkali mtu akiwa nyumbani kwa kutumia vyakula vya matibabu ambavyo viko tayari kutumiwa]] inawezekana wakati mwingi.[12]
Kwa wale ambao wana utapiamlo mkali unosababishwa na matatizo mengine ya afya wanapendekezwa kupata matibabu hospitalini.[12] Mara kwa mara hii uhusisha kudhibiti kiwango cha chini cha sukari kwenye damu, halijoto ya mwili, ukosefu wa maji, na kupata lishe polepole.[12][14]
Viuavijasumu vya mara kwa mara vinapendekezwa kwa sababu ya hatari ya juu ya maambukizo.[14]
Hatua za muda mrefu zinajumuisha: kuboresha kilimo,[15] kupunguza ufukara, kuondoa uchafu katika mazingira, na kuwawezesha wanawake.[11]
Kulikuwa na watu milioni 925 waliokuwa na utapiamlo duniani katika mwaka wa 2010, ongezeko la milioni 80 tangu 1990.[16][17]
Watu wengine bilioni moja wanakadiriwa kukosa vitamini na madini.[11]
Katika mwaka wa 2010 utapiamlo wa protini inayoleta nguvu ulikadiriwa kusababisha vifo 600,000, vilivyo chini kutoka vifo 883,000 katika mwaka wa 1990.[18]
Ukosefu mwingine wa lishe, ambao unaweza kujumuisha ukosefu wa aidini na anemia kutokana na ukosefu wa madini, ulisababisha vifo vingine 84,000.[18]
Ukosefu wa lishe hadi mwaka wa 2010 ulikuwa sababu ya 1.4% ya miaka ya maisha iliyobadilika kwa sababu ya ulemavu.[11][19]
Takriban theluthi moja ya vifo katika watoto huaminika kutokana na utapiamlo; hata hivyo, vifo havisemekani kutokana na hiyo.[5]
Katika mwaka wa 2010 ilikadiriwa kwamba ilichangia takriban vifo milioni 1.5 katika wanawake na watoto,[20] ijapokuwa baadhi ya makadirio ya idadi hiyo huenda yanatakiwa kuwa zaidi ya milioni 3.[12]
Watoto wengine milioni 165 wana matatizo ya kukua kutokana na ugonjwa huu.[12]
Ukosefu wa lishe ni wa kawaida sana katika nchi zinazoendelea.[21] Takwimu zaonyesha kwamba Afrika ni mojawapo ya bara ambazo watoto wachanga wako na shida ya kurefuka pamoja na kuwanda kupindukia kwa sababu ya utapiamlo. Kulingana na Global Nutrition report Ilihifadhiwa 23 Januari 2018 kwenye Wayback Machine., bara la Afrika lakumbana na shida nyingi za lishe. Licha ya shida ya kutorefuka kupiganwa nayo, watoto millioni sitini wa bara hili hawakui vizuri. Lishe anayopata mtu hutegemea na umri wake kwa sababu watoto wachanga hawawezi kula chakula kinacholiwa na wazee.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.