Bilioni
From Wikipedia, the free encyclopedia
Bilioni (kutoka Kiingereza "billion"[1][2]) ni namba ambayo inamaanisha milioni elfu moja na kuandikwa 1,000,000,000.

Inafuata 999,999,999 na kufuatwa na 1,000,000,001.
Inaweza kuandikwa pia kifupi 1 × 109.
Kiambishi awali giga kinatumika pia kumaanisha mara 1,000,000,000, ingawa katika lugha nyingine nyingi neno linalofanana na "bilioni" linamaanisha milioni milioni (1,000,000,000,000).
Matumizi tofauti
Katika Kiingereza cha Uingereza hadi mwaka 1964 neno "milliard" lilikuwa kawaida kwa namba inayoitwa sasa "bilioni". "Bilioni" ilikuwa kawaida cha Kiingereza cha Marekani tu, lakini ilingia polepole pia katika matumizi ya Kiingereza cha kimataifa.
Mwaka 1974 serikali ya Uingereza ikaamua kutumia umbo hilo.[3]
Kwa Kiingereza mifumo hii miwili kwa kutaja namba kubwa sana huitwa "short scale" (Kimarekani) na "long scale" (Kiingereza cha zamani).
Nchi nyingine, hasa za Ulaya, Afrika na Amerika ya Kilatini zimeendelea kutumia "long scale" kwa lugha kama Kifaransa, Kijerumani au Kihispania. Kwa hiyo katika nchi hizo 1,000,000,000 huitwa kwa neno kama "miliardi" na bilioni ni namba ya "milioni x milioni".
Tofauti inaweza kuleta mara nyingi makosa kama matini inatafsiriwa au kama kitabu cha kale kutoka Kiingereza hutumiwa.

"Short scale", 1,000,000,000 au 109 inaitwa bilioni
Long scale, 1,000,000,000 au 109 inaitwa miliardi
Mifumo yote miwili kandokando
Mifumo tofauti
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.