Vitamini

From Wikipedia, the free encyclopedia

Vitamini

Vitamini ni kirutubishi kinachohitajika na mwili kwa kujenga afya yake. Kwa lugha nyingine, kampaundi ogania zilizo lazima kwa shughuli za mwili lakini haziwezi kutengenezwa na mwili wenyewe ni lazima kuzipata kupitia chakula. Viumbehai wanaweza kuishi bila matata wakikosa vitamini kwa muda mfupi lakini uhaba wa muda mrefu unaleta magonjwa.[1]

Thumb
Matunda ni chanzo muhimu cha vitamini

Vitamini inaitwa mara nyingi kwa herufi kama vitamini A, vitamini B, vitamini C na kadhalika.

Vitamini hutofautiana kati ya viumbe maana kama kemikali huitwa "vitamini" inategemea kama kiumbe fulani anaweza kutengeza kemikali hiyo ndani ya mwili wake au la. Kwa mfano vitamini C ni asidi askobini na wanyama wengi wanaitengeneza ndani ya miili yao; lakini sehemu ya mamalia, hasa nyani wakubwa (primates) pamoja na binadamu, hawawezi kuitengeneza hivyo wanahitaji chakula chenye asidi hiyo ambayo hupatikana hasa kwenye matunda kama limau au chungwa.

Leo hii vitamini nyingi kwa mahitaji ya binadamu hutengenezwa viwandani na kupatikana kama vidonge.

Aina

  • Vitamini A (all-trans-retinols, all-trans-retinyl-esters, pamoja na all-trans-β-carotene na carotenoids zingine za provitamin A)
  • Vitamini B1 (thiamine)
  • Vitamini B2 (riboflavin)
  • Vitamini B3 (niacin)
  • Vitamini B5 (pantothenic acid)
  • Vitamini B6 (pyridoxine)
  • Vitamini B7 (biotin)
  • Vitamini B9 (folic acid na folates)
  • Vitamini B12 (cobalamins)
  • Vitamini C (ascorbic acid na ascorbates)
  • Vitamini D (calciferols)
  • Vitamini E (tocopherols na tocotrienols)
  • Vitamini K (phylloquinones, menaquinones, na menadiones)

Uainishaji

Vitamini zimegawanywa katika makundi mawili: zile zinazoyeyuka katika maji na zile zinazoyeyuka katika mafuta. Kwa binadamu, kuna jumla ya vitamini 13. 4 zinazoyeyuka katika mafuta (A, D, E, na K) na 9 zinazoyeyuka katika maji (vitamini 8 za kundi B na vitamini C).

Vitamini zinazoyeyuka katika maji huyeyuka kwa urahisi ndani ya maji na kwa kawaida hutolewa mwilini kwa haraka, kiasi kwamba kiwango cha vitamini kinachotolewa kupitia mkojo kinaweza kuwa kiashiria kizuri cha matumizi ya vitamini. Kwa sababu hazihifadhiwi kwa urahisi mwilini, ni muhimu kuzitumia mara kwa mara.

Vitamini zinazoyeyuka katika mafuta hufyonzwa kupitia njia ya mmeng'enyo wa chakula kwa msaada wa lipidi (mafuta). Vitamini A na D zinaweza kujilimbikiza mwilini, jambo ambalo linaweza kusababisha hali hatari ya hypervitaminosis. Upungufu wa vitamini zinazoyeyuka katika mafuta unaosababishwa na matatizo ya ufyonzaji wa chakula ni tatizo kubwa hasa kwa wagonjwa wa cystic fibrosis.

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.