Papua Guinea Mpya (Independen Stet bilong Papua Niugini) ni nchi karibu na Indonesia na Australia inayokalia upande wa mashariki wa kisiwa cha Guinea Mpya pamoja na visiwa vya kandokando.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Unity in diversity | |||||
Wimbo wa taifa: O Arise, All You Sons[1] | |||||
Mji mkuu | Port Moresby | ||||
Mji mkubwa nchini | Port Moresby | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza, Tok Pisin, Hiri Motu | ||||
Serikali | Ufalme wa Kikatiba Charles III wa Uingereza Sir Bob Dadae James Marape | ||||
Uhuru Madaraka ya kujitawala Uhuru |
1 Desemba 1973 16 Septemba 1975 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
462,840 km² (ya 54) 2 | ||||
Idadi ya watu - 2011 preliminary census kadirio - Msongamano wa watu |
7,059,653 (ya 102) 15/km² (ya 201) | ||||
Fedha | Kina (PGK ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
AEST (UTC+10) (UTC+10) | ||||
Intaneti TLD | .pg | ||||
Kodi ya simu | +675
- |
Nchi ni mwanachama wa Jumuia ya Madola. Mtawala ni Malkia Elizabeth II.
Mji mkuu ni Port Moresby.
Inakadiriwa kwamba watu wa kwanza walifika huko miaka 42,000-45,000 KK.[2]
Kati ya wakazi, wengi wanaishi katika mazingira asili,[3] ambayo kwa kiasi kikubwa hayajachunguzwa na wataalamu.[4]
Asilimia 18 tu wanaishi mijini.[5]
Nchini Papua Guinea Mpya kuna lugha za asili zaidi ya 800 (angalia orodha ya lugha za Papua Guinea Mpya).[6] Hiyo inaonyesha kwamba ni kati ya nchi zenye tofauti kubwa zaidi katika utamaduni.
Upande wa dini, Ukristo unafuatwa na 96% ya wakazi.[7] kati ya madhehebu, linaongoza Kanisa Katoliki (27.0%), likifuatwa na Walutheri (19.5%).
Wikiwand in your browser!
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.