From Wikipedia, the free encyclopedia
Tuvalu ni nchi ya visiwani ya Polynesia katika Bahari ya Pasifiki kati ya Hawaii na Australia. Nchi jirani katika bahari ni Kiribati, Samoa na Fiji.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Tuvalu mo te Atua (Kituvalu ya "Tuvalu kwa ajili ya Mola") | |||||
Wimbo wa taifa: Tuvalu mo te Atua | |||||
Mji mkuu | Vaiaku (kijiji), Fongafale (kisiwa), Funafuti (atolli) | ||||
Mji mkubwa nchini | -- | ||||
Lugha rasmi | Kituvalu, Kiingereza | ||||
Serikali | Ufalme wa kikatiba Charles III wa Uingereza Tofiga Vaevalu Falani Feleti Teo | ||||
Independence kutoka Uingereza |
1 Oktoba 1978 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
26 km² (ya 227) (kidogo sana) | ||||
Idadi ya watu - [[]] kadirio - 2017 sensa - Msongamano wa watu |
(ya 196) 11,192 476/km² (ya 27) | ||||
Fedha | Dollar ya Tuvalu Dollar ya Australia ( AUD ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC+12) (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .tv | ||||
Kodi ya simu | +688
- |
Jina la Tuvalu lamaanisha "visiwa vinane" kwa sababu kiasili kulikuwa na visiwa 8 tu vilivyokaliwa na watu. Kisiwa cha tisa kimepata wakazi tangu mwaka 1943.
Eneo lake ni visiwa vinne na atolli tano; kwa jumla eneo lina 26 km².
Kati ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa Tuvalu ni nchi yenye wakazi wachache kabisa.
Tuvalu ina visiwa (na atolli) vifuatavyo:
Kama nchi mbalimbali za visiwani Tuvalu iko katika hatari ya kupotea katika miaka 50 inayokuja. Kimo cha juu cha visiwa vyake ni mita 5 pekee juu ya UB. Kubadilika kwa hali ya hewa duniani na kupanda kwa uwiano wa bahari kutamaanisha ya kwamba sehemu kubwa sana la eneo lake litazama polepole chini ya maji.
Serikali imeshaomba majirani wakubwa kama Australia na New Zealand kuwapokea wenyeji wake.
New Zealand imekubali na kwa sasa kila mwaka watu 75 wanahamia New Zealand ambayo ni tayari kuwapokea pia wengine itakapokuwa lazima. Kuna mipango ya kuwapa makazi ya pamoja kwa kusaidia kuhifadhi utamaduni wao.
Tuvalu imekaliwa na watu wa Polynesia tangu zamani (miaka 3,000 hivi iliyopita).
Iliwekwa chini ya usimamizi wa Uingereza katika karne ya 19 kwa jina la "Ellis Islands".
Kati ya 1892 hadi 1916 ilikuwa eneo lindwa na baadaye sehemu ya koloni la Gilbert and Ellice Islands hadi 1974.
Mwaka ule wenyeji walipigia kura pendekezo la kuwa pekee, mbali na visiwa vya Gilbert vilivyokuwa Kiribati baadaye. Tuvalu ikapata uhuru wake mwaka 1978.
Kuna lugha tatu tu ambazo huzungumzwa nchini Tuvalu, yaani Kiingereza, Kituvalu na Kikiribati.
Upande wa dini, karibu wakazi wote ni Waprotestanti (97%).
Nchi_na maeneo ya Australia na Pasifiki |
Australia | Fiji | Guam | Hawaii | Kaledonia Mpya | Kiribati | Kisiwa cha Pasaka | Mikronesia | Nauru | Nyuzilandi | Niue | Pitcairn | Polinesia ya Kifaransa | Palau | Papua Guinea Mpya | Samoa | Samoa ya Marekani | Visiwa vya Cook | Visiwa vya Mariana ya Kaskazini | Visiwa vya Marshall | Visiwa vya Solomon | Tonga | Tuvalu | Vanuatu | Wallis na Futuna |
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.