From Wikipedia, the free encyclopedia
Liberia (yaani Nchi ya watu huru kwa Kilatini) ni nchi iliyoko Afrika ya Magharibi. Imepakana na nchi za Ivory Coast, Guinea, na Sierra Leone.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: The love of liberty brought us here (Upendo wa uhuru ulituleta hapa) | |||||
Wimbo wa taifa: All Hail, Liberia, Hail! | |||||
Mji mkuu | Monrovia | ||||
Mji mkubwa nchini | Monrovia | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza | ||||
Serikali • Rais • Makamu wa Rais |
Jamhuri Joseph Boakai Jeremiah Koung | ||||
Ilianza • Tarehe |
na ACS 26 Julai 1847 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
111,369 km² (103rd) 13.514% | ||||
Idadi ya watu - Julai 2023 kadirio - 2008 sensa - Msongamano wa watu |
5,506,280 (120th) 3,476,608 35.5/km² (180th) | ||||
Fedha | dola ya Liberia (LRD ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
GMT (UTC) - (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .lr | ||||
Kodi ya simu | +231
- |
Ni mojawapo ya nchi za Afrika ambazo hazikutawaliwa na Wazungu. Hata hivyo watu wa Liberia huongea Kiingereza sana.
Liberia ni nchi iliyoundwa na makabila 16 ya asili nchini humo na wahamiaji Weusi toka Marekani na Karibi (5%), mbali na machotara wa aina mbalimbali.
Wamarekani Weusi hao walikuwa watumwa waliopata uhuru ambao kwa kushirikiana na chama cha American Colonization Society waliunda taifa hili na kutangaza uhuru wa nchi hiyo tarehe 26 Julai 1847.
Wamarekani Weusi hao waliichukulia nchi hiyo kama nchi ya ahadi kutokana na asili yao kuwa Afrika, ambako ndiko mababu zao walikotokea kabla ya kupelekwa utumwani Marekani.
Hata hivyo, wahamiaji hao waliendelea kujitambulisha kama Wamarekani na hawakujenga mahusiano ya karibu na wenyeji.
Alama za taifa hili (bendera, kauli mbiu, na nembo) na hata muundo wa serikali vilikuwa vikionyesha mahusiano ya karibu kati ya nchi hizo mbili.
Liberia ilikuwa katika vita ya wenyewe kwa wenyewe kati ya miaka 1989-1996 na 1999-2003.
Hivi karibuni umefanywa kwa mara ya pili uchaguzi kwa amani na kuweza kumchagua George Weah kushika nafasi ya mwanamke wa kwanza kuwa Rais barani Afrika, Ellen Johnson-Sirleaf.
Lugha rasmi ni Kiingereza, ambacho kinatumiwa na asilimia 15 za wakazi. Lugha za taifa ni 4: Kiingereza cha Kiliberia, Kikpelle, Kimeriko na Krioli.
Upande wa dini, wakazi kwa asilimia 85.5 ni Wakristo, hasa Waprotestanti, halafu Wakatoliki (5.8%). Waislamu ni 12.2%. Wanaoendelea kufuata dini asilia za Kiafrika ni 0.5% tu.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link){{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link){{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link){{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)Liberia travel guide kutoka Wikisafiri
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.