Cabo Verde

From Wikipedia, the free encyclopedia

Cabo Verde

Cabo Verde (Kiingereza: Cape Verde) ni nchi ya visiwa katika bahari ya Atlantiki mbele ya pwani ya Afrika ya Magharibi.

Ukweli wa haraka Jamhuri ya Cabo Verde República de Cabo Verde (Kireno), Mji mkuu na mkubwa ...
Jamhuri ya Cabo Verde
República de Cabo Verde (Kireno)
Thumb
Bendera
Thumb
Nembo
Kaulimbiu:
Unidade, Trabalho, Progresso (Kireno)
"Umoja, Kazi, Maendeleo"
Wimbo wa taifa: Cântico da Liberdade (Kireno)
"Mkarara wa Uhuru"
Thumb
Thumb
Mji mkuu
na mkubwa
Praia
20°54 N 156°22 W
Lugha rasmiKireno
Kikaboverde
SerikaliJamhuri
  Rais
  Waziri Mkuu
José Maria Neves
Ulisses Correia e Silva
Eneo
  Jumlakm2 4 033[1]
Idadi ya watu
  Kadirio la 2023603 901[1]
PLT (PPP)Kadirio la 2023
  Jumla USD bilioni 5.717[2]
  Kwa kila mtu USD 9 909[2]
PLT (kawaida)Kadirio la 2023
  Jumla USD bilioni 2.598[2]
  Kwa kila mtu USD 4 503[2]
HDI (2021) 0.662[3] - kati
SarafuEscudo ya Cabo Verde
Funga

Umbali wake na Senegal ni km 460.

Jiografia

Eneo la visiwa vyake kwa jumla ni km² 4,033.

Funguvisiwa lake lina visiwa 15 katika vikundi viwili:

Miji

Mji mkuu ni Praia katika kisiwa cha Santiago.

Miji mikubwa zaidi ni (takwimu za mwaka 2010): Praia (wakazi 127,832), Mindelo (wakazi 70,468), Santa Maria (wakazi 23,839), Assomada (wakazi 12,026), Pedra Badejo (wakazi 9,345) na São Filipe (wakazi 8,125).

Historia

Hadi kufika kwa Wareno katika karne ya 15 visiwa vya Cabo Verde havikuwa na watu.

Wareno walianzisha mashamba ya miwa na kuleta watumwa kutoka bara la Afrika.

Cabo Verde ilikuwa pia kituo muhimu cha biashara ya watumwa kati ya Afrika na Amerika.

Wahamiaji kutoka Ulaya walikuwa pia Wahispania, Waitalia pamoja na Wayahudi na Waislamu waliokataliwa kukaa kwao Ureno.

Watu

Kutokana na historia hiyo, leo idadi kubwa ya wakazi ni machotara waliozaliwa na Waafrika (waliochangia 56% ya DNA) na Wazungu (waliochangia 44%).

Lugha rasmi ni Kireno, lakini wakazi wanazungumza zaidi aina mbalimbali za Krioli iliyotokana na lugha hiyo.

Upande wa dini, walau 89.1% ya wakazi ni Wakristo, hasa wa Kanisa Katoliki (78.7%), lakini pia wa madhehebu mbalimbali ya Uprotestanti (10.4%).

Kutokana na hali ngumu ya uchumi, wananchi wanaoishi nje ya Cabo Verde ni mara mbili kuliko wale wanaoishi nchini. Kati ya waliohama baada ya uhuru (1975), 500,000 wanaishi Marekani na 150,000 Ureno. Hata hivyo kuna wahamiaji vilevile, hasa kutoka nchi za Afrika bara.

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.