From Wikipedia, the free encyclopedia
Nchi za visiwa ni nchi zilizopo kabisa kwenye eneo la kisiwa au visiwa mbalimbali bila kuwa na eneo barani. Kuna nchi 47 za aina hii duniani ambazo ni robo za nchi zote za dunia. Nchi nyingi za aina hii ni ndogo sana. Kuna nchi za aina hii zilizopo kwenye kisiwa kimoja tu kama Kupro; nyingine zina visiwa vingi kama Indonesia.
Nchi kwenye visiwa vikubwa vinafanana katika mengi na nchi za barani. Eneo linatosha kwa kilimo kinacholisha idadi kubwa ya wakazi. Mifano yake nio nchi kama Japani, Sri Lanka, Ufilipino, Kuba, Uingereza, Iceland na Madagaska. Nchi kubwa kabisa ya visiwani ni Indonesia.
Nchi ndogo za visiwani hasa kama ni ndogo sana zina tabia za pekee. Mara nyingi ardhi haitoshi kulisha watu wengi hivyo idadi ya wakazi ni ndogo na wengi wamehamia nje. Siku hizi nchi nyingi za aina hii zimetegemea hasa utalii. Mifano yake ni Komori, Bahamas, Tonga na Maldivi.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.