Remove ads
nchi huru barani Afrika From Wikipedia, the free encyclopedia
Gine ya Ikweta (pia: Ginekweta au Guinea ya Ikweta), kirasmi Jamhuri ya Gine ya Ikweta, ni nchi mojawapo ndogo ya Afrika iliyopo upande wa magharibi wa Afrika ya Kati.
Jamhuri ya Gine ya Ikweta | |
---|---|
República de Guinea Ecuatorial (Kihispania) République de Guinée équatoriale (Kifaransa) República da Guiné Equatorial (Kireno) | |
Kaulimbiu ya taifa: Unidad, Paz, Justicia (Kihispania) "Umoja, Amani, Haki" | |
Wimbo wa taifa: Caminemos pisando las sendas de nuestra inmensa felicidad (Kihispania) "Tutembee tukifuata njia za furaha yetu kubwa" | |
Mahali pa Guinea ya Ikweta | |
Ramani ya Guinea ya Ikweta | |
Mji mkuu | Malabo |
Mji mkubwa nchini | Bata |
Lugha rasmi | Kihispania Kifaransa Kireno |
Serikali | Udikteta |
• Rais | Teodoro Obiang |
Eneo | |
• Eneo la jumla | km2 28 050[1] |
Idadi ya watu | |
• Kadirio la 2023 | 1 737 695[1] |
Pato la taifa | Kadirio la 2023 |
• Jumla | USD bilioni 10.041[2] |
• Kwa kila mtu | USD 6 502[2] |
Pato halisi la taifa | Kadirio la 2023 |
• Jumla | USD bilioni 28.356[2] |
• Kwa kila mtu | USD 18 362[2] |
Maendeleo (2021) | 0.596[3] - wastani |
Sarafu | Faranga ya CFA |
Majira ya saa | UTC+1 |
Msimbo wa simu | +240 |
Msimbo wa ISO 3166 | GQ |
Jina la kikoa | .gq |
Imepakana na Kamerun upande wa kaskazini, Gabon upande wa kusini na mashariki, na Ghuba ya Gine upande wa magharibi, ambapo visiwa vya São Tomé na Príncipe vinapatikana kusini-magharibi mwa Guinea ya Ikweta.
Jina la nchi linatokana na kuwa karibu na Ghuba ya Guinea na Ikweta.
Nchi ina sehemu mbili kuu. Eneo kubwa liko kwenye bara la Afrika katika kanda ya Rio Muni. Ndipo walipo wakazi wengi zaidi.
Sehemu iliyoendelea zaidi, pamoja na mji mkuu, iko kwenye kisiwa cha Bioko. Pamoja na visiwa vingine, hasa Annobon, hiyo kanda ya Visiwa ni sehemu ya pili ya nchi.
Ilikuwa koloni la Hispania kwa jina la Guinea ya Kihispania likiwa na maeneo mawili ambayo yalijulikana kama Río Muni (bara na visiwa vidogo kadhaa), na kisiwa cha Bioko (zamani: Fernando Poo) ambako uko mji mkuu, Malabo (ambayo iliitwa awali Santa Isabela).
Guinea ya Ikweta imegawiwa katika mikoa 8 iliyopo katika kanda mbili:
Wananchi wengi (80%) ni wa kabila la Wafang, ambao ni wa Kibantu.
Ni nchi pekee ya Afrika ambapo lugha ya Kihispania ndiyo lugha rasmi na ya taifa, hasa ukiacha Ceuta na Melilla (maeneo ya Hispania yaliyozungukwa na Moroko) na Jamhuri ya Sahara ya Kidemokrasia ya Kiarabu (nchi isiyotambulika kimataifa). Pamoja nacho, Kifaransa na Kireno pia ni lugha rasmi.
Wananchi wengi wanafuata Ukristo katika Kanisa Katoliki (88%) na madhehebu mbalimbali ya Uprotestanti (5%). Wanaofuata dini asilia za Kiafrika na Baha'i ni 5%. Waislamu ni 2%.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.