Remove ads

Gine ya Ikweta (pia: Ginekweta au Guinea ya Ikweta), kirasmi Jamhuri ya Gine ya Ikweta, ni nchi mojawapo ndogo ya Afrika iliyopo upande wa magharibi wa Afrika ya Kati.

Ukweli wa haraka Jamhuri ya Gine ya Ikweta, Mji mkuu ...
Jamhuri ya Gine ya Ikweta
República de Guinea Ecuatorial (Kihispania)
République de Guinée équatoriale (Kifaransa)
República da Guiné Equatorial (Kireno)
Thumb
Bendera
Thumb
Nembo
Kaulimbiu ya taifa:
Unidad, Paz, Justicia (Kihispania)
"Umoja, Amani, Haki"
Wimbo wa taifa:
Caminemos pisando las sendas de nuestra inmensa felicidad (Kihispania)
"Tutembee tukifuata njia za furaha yetu kubwa"
Thumb
Mahali pa Guinea ya Ikweta
Thumb
Ramani ya Guinea ya Ikweta
Mji mkuuMalabo
3°44 N 8°46 E
Mji mkubwa nchiniBata
01°51 N 09°46 E
Lugha rasmiKihispania
Kifaransa
Kireno
SerikaliUdikteta
  RaisTeodoro Obiang
Eneo
  Eneo la jumlakm2 28 050[1]
Idadi ya watu
  Kadirio la 20231 737 695[1]
Pato la taifaKadirio la 2023
  JumlaPunguko USD bilioni 10.041[2]
  Kwa kila mtuPunguko USD 6 502[2]
Pato halisi la taifaKadirio la 2023
  JumlaPunguko USD bilioni 28.356[2]
  Kwa kila mtuPunguko USD 18 362[2]
Maendeleo (2021)Ongezeko 0.596[3] - wastani
SarafuFaranga ya CFA
Majira ya saaUTC+1
Msimbo wa simu+240
Msimbo wa ISO 3166GQ
Jina la kikoa.gq
Funga

Imepakana na Kamerun upande wa kaskazini, Gabon upande wa kusini na mashariki, na Ghuba ya Gine upande wa magharibi, ambapo visiwa vya São Tomé na Príncipe vinapatikana kusini-magharibi mwa Guinea ya Ikweta.

Jina

Jina la nchi linatokana na kuwa karibu na Ghuba ya Guinea na Ikweta.

Jiografia

Makala kuu: Jiografia ya Guinea ya Ikweta

Nchi ina sehemu mbili kuu. Eneo kubwa liko kwenye bara la Afrika katika kanda ya Rio Muni. Ndipo walipo wakazi wengi zaidi.

Sehemu iliyoendelea zaidi, pamoja na mji mkuu, iko kwenye kisiwa cha Bioko. Pamoja na visiwa vingine, hasa Annobon, hiyo kanda ya Visiwa ni sehemu ya pili ya nchi.

Thumb
Bioko inavyoonekana kutoka Kamerun.

Historia

Ilikuwa koloni la Hispania kwa jina la Guinea ya Kihispania likiwa na maeneo mawili ambayo yalijulikana kama Río Muni (bara na visiwa vidogo kadhaa), na kisiwa cha Bioko (zamani: Fernando Poo) ambako uko mji mkuu, Malabo (ambayo iliitwa awali Santa Isabela).

Siasa

Makala kuu: Siasa za Guinea ya Ikweta

Uchumi

Makala kuu: Uchumi wa Guinea ya Ikweta

Mikoa

Thumb
Mikoa ya Guinea ya Ikweta

Guinea ya Ikweta imegawiwa katika mikoa 8 iliyopo katika kanda mbili:

  1. Mkoa wa Annobón (mji mkuu wa mkoa: San Antonio de Palé)
  2. Mkoa wa Bioko Norte (Malabo)
  3. Mkoa wa Bioko Sur (Luba)
  4. Mkoa wa Centro Sur (Evinayong)
  5. Mkoa wa Kié-Ntem (Ebebiyín)
  6. mkoa wa Litoral (Bata)
  7. Mkoa wa Wele-Nzas (Mongomo)
  8. Mkoa wa Djibloho (Ciudad de la Paz)

Watu

Makala kuu: Watu wa Guinea ya Ikweta

Wananchi wengi (80%) ni wa kabila la Wafang, ambao ni wa Kibantu.

Lugha

Ni nchi pekee ya Afrika ambapo lugha ya Kihispania ndiyo lugha rasmi na ya taifa, hasa ukiacha Ceuta na Melilla (maeneo ya Hispania yaliyozungukwa na Moroko) na Jamhuri ya Sahara ya Kidemokrasia ya Kiarabu (nchi isiyotambulika kimataifa). Pamoja nacho, Kifaransa na Kireno pia ni lugha rasmi.

Dini

Wananchi wengi wanafuata Ukristo katika Kanisa Katoliki (88%) na madhehebu mbalimbali ya Uprotestanti (5%). Wanaofuata dini asilia za Kiafrika na Baha'i ni 5%. Waislamu ni 2%.

Remove ads

Utamaduni

Makala kuu: Utamaduni wa Guinea ya Ikweta

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.

Remove ads