From Wikipedia, the free encyclopedia
Jamhuri ya Zimbabwe (iliyojulikana wakati wa ukoloni kama Rhodesia ya Kusini) ni nchi isiyo na bahari iliyoko upande wa kusini wa Bara la Afrika, kati ya mto Zambezi na mto Limpopo.
| |||||
Kaulimbiu ya Taifa Unity, Freedom, Work (Kiingereza: Umoja, Uhuru, Kazi) " | | |||||
Wimbo wa Taifa | |||||
Location of Zimbabwe | |||||
Lugha rasmi | Kiingereza na 15 nyingine | ||||
Mji Mkuu | Harare | ||||
Mji mkubwa | Harare | ||||
Rais | Emmerson Mnangagwa | ||||
Eneo - Jumla -Maji -Eneo kadiriwa |
km² 390,757 1% ya 60 duniani | ||||
Umma - Kadirio - Sensa, - Msongamano wa watu |
15,178,979 ya 66 duniani (2022) ; 32/km² ; ya duniani | ||||
Chumo cha uchumi - Jumla - kwa kipimo cha umma |
$24.99 billion (Orotha ya nchi GDP (kidogo)) $2,100 (Orodha ya nchi kulingana na GDP kwa umma) | ||||
Uhuru - Kadirifu - Barabara |
(kama Rhodesia) 11 Novemba 1965 (kama Zimbabwe) 18 Aprili 1980 | ||||
Fedha | Dolar ya Marekani| | ||||
Saa za Eneo | UTC +2 | ||||
Intaneti TLD | .zw | ||||
kodi za simu | 263 |
Imepakana na Afrika ya Kusini upande wa kusini, Botswana upande wa magharibi, Zambia upande wa kaskazini-mashariki, na Msumbiji upande wa mashariki.
Jina Zimbabwe linatokana na neno "dzimba dzamabwe" linalomaanisha "nyumba ya mawe" kwa lugha ya Kishona. Nyumba hiyo ya mawe, ambayo imehifadhiwa kama eneo la kihistoria, ilikuwa makao ya Ufalme wa Mutapa ambaye mfalme wake aliongoza eneo hilo miaka ya kale.
Zimbabwe imegawiwa katika mikoa 8 na miji 2 yenye hadhi ya mikoa. Imegawiwa zaidi katika wilaya 59 na kata 1,200.
Miji minne mikubwa ya Zimbabwe ni:
Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani.
Katika karne za kwanza BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi.
Tangu karne ya 11, Zimbabwe ya leo imekuwa na falme imara kwenye njia muhimu ya biashara, hasa ufalme wa Mutapa.
Kampuni ya British South Africa ya Cecil Rhodes iliweka mipaka ya sasa katika miaka ya 1890.
Koloni la Uingereza lilianzishwa mwaka 1923 kwa jina la Southern Rhodesia.
Mwaka 1965, serikali ya walowezi Wazungu ilijitangazia uhuru kwa jina la Rhodesia tu.
Baada ya miaka 14 ya kutengwa kimataifa na kupigana na raia Waafrika katika miaka ya 1970, mapatano ya mwaka 1979 yalikubali wakazi wote wawe na haki ya kupiga kura na nchi ikawa huru kweli kwa jina la Zimbabwe mwaka 1980.
Rais Robert Mugabe alipata umaarufu katika siasa kama mpiganaji dhidi ya ukoloni lakini pia kama aina ya dikteta aliyerudisha nyuma uchumi wa nchi.
Baada ya yeye kulazimishwa na wanajeshi kujiuzulu, tarehe 24 Novemba 2017 Emmerson Mnangagwa amekuwa rais mpya wa Zimbabwe.
Wakazi wengi (82%) ni wa kabila la Washona, 14% ni Wandebele, 2% ni wa makabila mengine ya Kiafrika, 1% ni machotara, Wahindi, Wazungu n.k.
Kwa sasa lugha rasmi ni 16. Lugha kubwa ni Kishona (70%) na Kindebele (20%). Kiingereza ni lugha ya kwanza ya chini ya asilimia 2.5% za wakazi.
Upande wa dini, 84.1% ni Wakristo (hasa Waanglikana, Wakatoliki 8%, Wasabato na Wamethodisti). Waliobaki ni wafuasi wa dini asilia za Kiafrika (4.5%), ni Waislamu (0.7%), au hawana dini (10.2%) .
Mawasiliano ya simu na mitambo yake yanaendeshwa na Tel-One0, kampuni ya serikali.
Kuna kampuni 3 za simu za mikononi: Econet Wireless, Net*One na Telecel.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.