Remove ads
From Wikipedia, the free encyclopedia
Wamethodisti ni wafuasi wa Yesu Kristo wanaozingatia mafundisho ya John Wesley (1703-1791) ambaye katikati ya karne ya 18 alianzisha uamsho katika ushirika wa Anglikana akisaidiana na mdogo wake Charles (1707-1788) na George Whitefield (1714-1770).
Mapema wakleri wengi wa Anglikana walijiunga nao wakaitwa Methodists.
Ni baada ya kifo cha John Wesley tu kwamba wao wakawa madhehebu ya kujitegemea.
Kupitia umisionari wa nguvu Umethodisti ulienea katika Dola la Uingereza, Marekani na kwingine.
Kwa sasa wanakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 70 duniani kote.
Karibu jumuia zao zote zinaunda pamoja kiungo cha mashauriano kinachoitwa World Methodist Council, chenye makao makuu huko Lake Junaluska, North Carolina, Marekani.
Hata hivyo Umethodisti una tofauti kubwa ndani yake upande wa mafundisho, ibada n.k.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.