From Wikipedia, the free encyclopedia
Turkmenistan ni nchi ya Asia ya Kati.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: | |||||
Wimbo wa taifa: Wimbo wa taifa huru na huria | |||||
Mji mkuu | Ashgabat | ||||
Mji mkubwa nchini | Ashgabat | ||||
Lugha rasmi | Kiturkmeni | ||||
Serikali | Udikteta Serdar Berdimuhamedow | ||||
Uhuru Ilitangazwa Ilitambuliwa |
27 Oktoba 1991 8 Desemba 1991 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
491,210 km² (ya 53) 4.9 | ||||
Idadi ya watu - Desemba 2020 kadirio - Msongamano wa watu |
6,031,187 (ya 113) 10.5/km² (ya 221) | ||||
Fedha | Manat (Turkmenistan) (TMM ) | ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
TMT (UTC+5) (UTC+5) | ||||
Intaneti TLD | .tm | ||||
Kodi ya simu | +993
- |
Jina limetokana na lugha ya Kiajemi, likimaanisha "nchi ya Waturkmeni".
Imepakana na Afghanistan, Uajemi, Uzbekistan, Kazakhstan na Bahari Kaspi.
Nchi ina eneo la km² 488,100, karibu sawa na Kamerun.
Sehemu kubwa (80 %) ni jangwa, hasa jangwa la Karakum.
Milima ya Kopet Dag kusini magharibi inafikia kimo cha mita 2,912.
Kati ya mito mikubwa ni Amu Darya, mto Murghab na mto Hari Rud.
Hali ya hewa si baridi sana lakini kuna joto kali wakati wa kiangazi.
Mvua ni chache; zanyesha hasa kati ya Januari na Mei.
Miji muhimu ni Ashgabat, Turkmenbashi (zamani Krasnovodsk) na Dashoguz.
Turkmenistan ilitwaliwa na Urusi tangu mwisho wa karne ya 19 ikaingia hivyo katika Umoja wa Kisovyeti baada ya mwaka 1917 na kuwa jamhuri ndani yake kwa jina la Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiturkmeni hadi mwaka 1991.
Wakati wa kusambaratika kwa Umoja wa Kisovyeti, kiongozi wa chama cha kikomunisti Saparmirat Niyasov akaendelea kushika uongozi akitawala kama rais hadi kifo chake mwaka 2006.
Niyasov alibadilisha utawala wa chama cha kikomunisti kuwa udikteta wake mwenyewe. Akaanza kutumia jina la "Turkmenbashi" (Baba wa Waturkmeni wote) na sanamu zake zikasimamishwa kote nchiniː mara nyingi zilikuwa sanamu za dhahabu hata kama wananchi walikuwa na maisha magumu.
Mapato kutoka gesi na mafuta ya petroli yalimwezesha kuendesha uchumi wa nchi kwa hiari yake bila mabadiliko makubwa jinsi ilivyokuwa kawaida wakati wa anguko la ukomunisti kwingineko.
Zaidi ya nusu ya wananchi walikuwa hawana ajira na kuishi maisha ya umaskini, lakini wanapewa chumvi, umeme na maji bure. Mkate na petroli zinauzwa kwa bei ya chini sana, lakini kuna uhaba wa mara kwa mara.
Baada ya kifo cha Niyasov kamati ya viongozi ilimteua makamu wa waziri mkuu Gurbanguly Berdimuhammedov kuwa rais mpya ingawa kadiri ya katiba mwenyekiti wa bunge alitakiwa kuchukua nafasi hiyo.
Mwenyekiti wa bunge alishtakiwa mahakamani juu ya makosa fulani na Berdimuhammedov alithibitishwa katika uchaguzi wa tarehe 11 Februari 2007 kwa 89% za kura. Watazamaji walidai kura ilikuwa ya uwongo.
Mwaka 2013 kwa mara ya kwanza ulifanyika uchaguzi wa vyama vingi.
Waturkmeni wenyewe ni 81.8% za wakazi wote, wakifuatwa na Wauzbeki (9.4%), Warusi (2.2%), Wakazaki (1.6%) na Waarmenia (1.1%).
Lugha rasmi na ya kawaida ni Kiturkmeni (72%). Kinafuata Kirusi (12%).
Wakazi walio wengi ni Waislamu; kuna kadirio ya Waislamu asilimia 96.1 kati ya wakazi wote lakini haijulikani ni wangapi wanaofuata kweli dini yao. Wakristo ni 3.6%, hasa Waorthodoksi.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.