Mataifa ya G20 ya viwanda
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kundi la Mawaziri wa Fedha ishirini na Magavana wa Benki Kuu (linalojulikana kama G-20, G20 au Group of Twenty) ni kundi la mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu kutoka nchi zenye uchumi mkubwa duniani: nchi 20, kuongezea Umoja wa Ulaya.
Nchi zenye rangi ya buluu nzito ni wanachama wa G-20; zenye rangi ya samawati ni wanachama wa Umoja wa Ulaya wasio na uwakilishi wa pekee. | |
Limeanzishwa | 1998* |
---|---|
Membership | 01. Argentina 02. Australia 03. Marekani 04. Brazil 05. Ufaransa 06. Italy 07. Meksiko 08. Misri 09. Ujerumani 10. Iran 11. Uturuki 12. Indonesia 13. Kanada 14. Japan 15. Korea Kusini 16. Urusi 17. China 18. Hispania 19. Afrika Kusini 20. Ufalme wa Muungano .: |
G-20*/21* Chairman.: | Chairman; President ,etc.: |
Main organ | United Nations.; |
Staff | 350 Million +PR, of China= 1.4 Billion.: |
Volunteers | Group of Seven & BRICS group.: |
Kwa pamoja, uchumi wa G-20 unajumuisha 85% ya[1] bidhaa jumla zinazotoka katika nchi[1] ulimwenguni, 80% ya biashara duniani (pamoja na biashara ya EU ya ndani) na theluthi mbili ya idadi ya watu duniani.[2]
G-20 ni kama ukumbi wa ushirikiano na kushauriana kuhusu masuala ya mfumo wa fedha wa kimataifa. Husoma, kupitia upya, na kukuza majadiliano kati ya nchi muhimu za viwanda na soko zinazoibukia kuhusu masuala ya sera zinazohusu uendelezaji wa udhibiti wa fedha kimataifa, na hutaka kushughulikia masuala ambayo yako juu ya majukumu ya shirika lolote.
Kwa G-20 kuongeza nguvu tangu kongamano la Washington la mwaka 2008, viongozi wake walitangaza tarehe 25 Septemba 2009, kwamba kundi hilo lingechukua pahala pa G8 kama halmashauri kuu ya kiuchumi ya mataifa tajiri.[3]
Viongozi wa mataifa wanachama wa G-20 hukutana kila mwaka mara mbili katika Kongamano la G-20.